Ajali haina hodi.. siamini kilichotokea leo asubuhi

Ajali haina hodi.. siamini kilichotokea leo asubuhi

mambo45

Member
Joined
Jul 13, 2026
Posts
12
Reaction score
18
Mi huwa naendesha gari ya shule frani iv iko maeneo ya kinyerezi leo katika mizunguko yangu ya kila siku bhna nikakutana na mwalimu mkuu nilivyo nishamaliza kuwafikisha wanafunzi nataka kupark gari. Akanambia toa gari kunasehmu nataka twende unisindikize tukaenda njiani akawa anani shawishi nimwelekeze gari

Me nikampa highlights kidogo then akaanza kuwana kitete baadae aka kaa sawa na tukaanza kufundishana

Aisee tuko road tunaenda pole pole si akajisahau namwambia punguza speed yeye akashindwa kabisa kuli control gari huku anakanyaga mafuta badala ya break tukaenda kuingia kwenye mtaro wapembeni

Niwashauri tu wadau kama kunamtu anataka kujifunza gari nibora tu aende driving school kuna elimu pana sana tunaikosa tunavyo fundishwa na watu tu juu juu na kuingia barabarani
 
Back
Top Bottom