Ajali ilyoua RAS wa Kilimanjaro na Dereva wake: Kwanini serikali inamlilia RAS tu je Dereva hakuwa mtumishi wake?

Tulimumu

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2013
Posts
14,409
Reaction score
13,262
Toka ajali iliyosababisha vifo vya Katibu Tawala - RAS wa mkoa wa Kilimanjaro na Dereva wake tumeshuhudia ubaguzi mkubwa unaoganywa na serikali kwenye misiba hii. Tumeshuhudia na tunaendelea kushuhudia serikali nzima ikiomboleza na kutumia nguvu kubwa kushughulika na Kifo cha RAS ikimpamba kwa sifa nyingi kwamba ameacha pengo kubwa kana kwamba Dereva hakuwa mtumishi wa serikali na hajaacha pengo.

Mpaka sasa haijulikani msiba wa dereva umebebwa na nani kwakuwa habari zake hazisikiki tena katika vyombo vyote vya habari na mitandao ya kijamii na pia kwa viongozi wote wa serikali kuanzia serikali ya mkoa hadi serikali kuu.
Tumeona na kusikia Rais ametuma salam za rambi rambi kwa mkoa na familia kutokana na kifo cha RAS. Zaidi ya hapo katoa ndege ya kumsafirisha marehemu RAS kutoka Kilimanjaro hadi Dsm nyumbani kwake na kutoka Dsm hadi kwao Songwe - Mbeya, Makamu wa Rais kafika Moshi kuhani familia ya RASm hapa Dsm jana Waziri mkuu ndiye alikwenda nyumbani kwa marehemu RAS kuwakilisha serikali na huko Mbeya serikali nzima ya mkoa imejipanga leo kwaajili ya mazishi yake.

Sasa tunajiuliza katika harakati zote hizi mbona hatusikii hatima ya marehemu dereva kwamba naye anasitiriwaje na serikali. Au hakuwa mtumishi wake kwamba alikuwa Deiwaka kiasi kwamba imsahau kiasi hiki? Hivi familia ya marehemu dereva inajidikiaje kutengewa na serikali kiasi hiki?

Kweli ukipata majanga na mtu mkubwa wewe mdogo usasahaulika kabisa.
 
Neno pengo kubwa ni unafiki sana wataleta RAS mwingine mke ataolewa na mwingine sasa sijui pengo hilo la nini!
 
Comments reserved
 
Back
Top Bottom