Tetesi: Ajali Lucky Vincent School: Uzembe, Tamaa, Ubadhirifu na Kutokujali Usalama wa Wanafunzi

Tetesi: Ajali Lucky Vincent School: Uzembe, Tamaa, Ubadhirifu na Kutokujali Usalama wa Wanafunzi

Hapa naona tunalumbana inatakiwa tuwaombe kwa Mungu awapumzishe kwa Amani
Hao wote ndo ilikuwa siku yao imefika ndo mana hayo yote yametokea na ilipagwa kuwa hiyo ndo itakuwa sababu ya vifo vyao
 
Kabla ya kuhukumu vipi miundo mbinu ya barabara zetu maana kwa kiasi kikubwa ndo chanzo kikuu cha ajari... Poleni ndugu na wazazi
 
inasikitisha sana ni sahihi ulichokiandika lakini mkuu kaa ukijua ajari haina kinga gari linaweza kuwa na hayo yote na dreva ni mzoefu wa miaka mingi ninachoweza kusema yawezekana dreva alikuwa mzembe sawa lakini! ! mazingira yalichangia kwa kiasi kikubwa kutokea kwa ajari yani mvua, ukungu na mahali penyewe yote kwa yote tunapata fuzo kubwa sana sisi tuliobaki Mungu awalaze mahali pema watoto wetu majeruhi awaguse pole kwa kwawalio fikwa na msiba

kinachonipa shida ni mtoto alietoka akiwa hana ana mchubuko zinazunguka picha 2 tofauti za jinsia tofauti sijui ninani kati yao muhusika
napia wanasema aliepona alikuwa kwenye gari la nyuma tofauti na lile lililo pata ajari maana gari zilikuwa wengine wanasema 4 inasikitisha sana kwakweli
Ukweli ni kuwa, watoto wpte waliokuwa kwenye ile gari iliyopata ajali wameathirika. Licha ya wale waliofariki, kuna watoto wawili wamejeruhiwa na wamelazwa. Hivyo Hanna mtoto aliyetoka clean bila majeraha. Tujitahidi kufuatilia taarifa rasmi kutoka Arusha.
 
Nimejiuliza sana hilo
Sawa Tuache mambo ya magari. KULIKUWA NA UMUHIMU GANI KWA WANAFUNZI KUSAFIRI KWA AJILI YA KWENDA KUFANYA JOINT EXAMS. WANGEWEZA KUTUNGA MTIHANI WAPAMOJA NA WATOTO WAKAFANYA BILA KUSAFIRI.
 
Magari mengi yanayobeba wanafunzi ni mabovu sana mengi yao yanatembelea tairi kipara
 
Watanzania tungekuwa wamoja tuhakikishe wahusika wa shule hii wanawajibishwa kwa vifo hivi Na ukizingatia hata RPC anatoa taarifa za uongo kuwa ni wanafunzi 30 wakati ni zaidi ya 33
Acha undezi wewe,wawajibishwe kwa kosa gani?kwani wao ndiyo waliosababisha ajali?
 
Sawa Tuache mambo ya magari. KULIKUWA NA UMUHIMU GANI KWA WANAFUNZI KUSAFIRI KWA AJILI YA KWENDA KUFANYA JOINT EXAMS. WANGEWEZA KUTUNGA MTIHANI WAPAMOJA NA WATOTO WAKAFANYA BILA KUSAFIRI.
Very stupid idea
 
Ajali ya ukweli ilitokea morogoro gari la abiria na kichwa cha Lori liendalo Rwanda nyang'anyang'a lakini abiria na dereva wa Lori wazima hilo la lucky Vincent kuna damu ilihitajika na waovu sishawishiki kwa hili
 
Hili jambo nadhani lingekuwa fundisho na kujifunza, lakini mkuu wetu mwenyewe Alisha sema "yeye hapangiwi wala hashairiwi" sasa na watendaji wake naimani hawapangiwi na hawashauriwi. We Gari linabeba wanafunzi viti vyenyewe ni chuma tupu, hakuna sponji, kazi IPO,
 
Humu ndani kuna mpumbavu mmoja anajiita bandu bandu kazi yake ku quote Na kuandika ujinga namshauri aache umbwa wake atulie wanaume wachangie mada
 
Sio kiasi mkuu hizo zote points,ukitaka kuamini kama wewe mkazi wa mji wa Dar angalia zile school buses zinazozunguka mjini zinavyojaza watoto.unakuta zimepakia tutoto twingi mpaka twingine tumepakatana madereva wenyewe nusu wendawazimu maana unakuta dereva anakimbizana na madereva wa daladala gari yenyewe model za 90's inatembea upande upande kama imekatika center bearing huku kabeba watoto wadogo wa shule inayotamba kutoa elimu nzuri sasa hapo likitokea la kutokea ndo kama hivi.
nimekupata mkuu wahusika waliangalie hilo
 
Wazazi poleni kwa msiba huu uliowapata watoto wetu wapendwa wa Lucky Vicent na walimu wao! Hakika ni majonzi makubwa sana! Lakini yafaa tutafakari kwa kina kwanini janga kama hili liwafike watoto hawa, tumaini la maisha yetu! Maswali ni mengi, na kwa kweli yana hitaji majibu ya kina.

Kwa tunaozunguka kutwa barabarani, mtakubaliana na mimi kuwa, vipo viashiria vingi hatarishi kwa watoto wetu wanapotumia mabasi ya shule zao. Shule nyingi zinatumia mabasi ambayo zamani yalitumika kama daladala, na baada ya kuchoka yakabadilishwa na kuwa mabasi ya shule. Huku madereva wakiendesha kwa mwendo usiostahili kabisa kubeba watoto.

Hatari zaidi, mabasi haya ya shule hubeba idadi kubwa ya wanafunzi kuzidi uwezo halisi wa gari, na kutokuzingatia taratibu zote za kiusalama kama vile kufunga mikanda. Mfano wa hili ni hii ajari ya Lucky Vicent. Wanasema "eti gari lili feli breki" ndo sababu ya ajari! Binafsi sikubaliani nalo.

Kwa wale ambao wameendesha magari makubwa kwa weledi na kwa kipindi kirefu, watakubaliana na mimi kuwa, kubeba uzito zaidi ya uwezo wa gari pamoja na mwendo kasi husababisha mfumo wa breki za gari kushidwa kuhimili, hivyo kutokukamata pale dereva anapozitumia.

Sababu nyingine ya kujiuliza, je ni kweli haya mabasi ya shule yanafanyiwa matengenezo na ukaguzi wa mara kwa mara, kwa maana ya motor vehicle service! Hapa inatiashaka! *A motor vehicle service is a series of maintenance procedures carried out at a set time interval or after the vehicle has travelled a certain distance.* Shule ya Lucky Vicent lazima ithibitishe kwa kuonyesha *service na log books* za hilo gari, majibu utayaona, hakuna kumbukumbu ya service.*The completed services are usually recorded in a service book which is rubber stamped by the service centre upon completion of each service.* Mashule mengi yanahuo udhaifu, na hii inatokana na uzembe, tamaa, ubadhirifu wa watendaji wao, kutokujali maisha ya wanafunzi na kutokuwa waangalifu huku wakiweka mbele masilahi yao na kupata faida.

Matengenezo muhimu na ya mara kwa mara kwa gari *motor vehicle service* ni kama ifuatavyo;
-Change the engine oil & oil filter
-Replace the air filter & fuel filter
-Tune the engine
-Check level & refill brake fluid/clutch fluid
-Check Brake Pads/Liners, Brake Discs/Drums, and replace if worn out.
-Check level and refill power steering fluid
-Refill Manual Transmission Fluid,Grease and lubricate components inspect.
-Check condition of the tires
-Check for proper operation of all lights, wipers etc.

Vipuri vingine vyote vinavyo weza kulifanya gari lisiwe salama kwa matumizi ya barabara hukaguliwa na kubadilishwa wakati wa kufany *service* je mashule yetu wanafanya haya! Kama haya hayafanyiki ni wakati sasa wazazi wa watu wote wenye matashi mema kuchukua hatua za kuwawajibisha wahusika wote ili kuokoa maisha ya watoto wasio na hatia.
Kumbe walioelimika bado wapo wengi tu, safi mleta uzi.
 
Ajali ya ukweli ilitokea morogoro gari la abiria na kichwa cha Lori liendalo Rwanda nyang'anyang'a lakini abiria na dereva wa Lori wazima hilo la lucky Vincent kuna damu ilihitajika na waovu sishawishiki kwa hili
Una safari ndefu sana kufika uendako kwa kuwa na mawazo mgando.
 
Yaani mkuu naona Sasa Umeingilia kazi ya Mola wako wale vijana pamoja na Walimu wao siku yao ilikuwa imeshafika kwaiyo Ajali walioipata imekuwa ndio sababu ya kuondoka kwao hakuna uzembe wala ubadhirifu wangapi wanapata Ajali na wanatoka salama tena hata miongoni mwa hao watoto wapo walio salimika kwaiyo acha Jazba ikiwa dereva mwenyewe amekufa ivi unaweza kuthubutu kusema amekufa kwa Uzembe wake? Mkuu sio kiivyo sisi tumshukuru tu Mola wetu Kazi yake siku zote haina makosa!!!
Una busara sana
 
Back
Top Bottom