Tetesi: Ajali Lucky Vincent School: Uzembe, Tamaa, Ubadhirifu na Kutokujali Usalama wa Wanafunzi

ulishawahi kuwa dereva mkuu
 
Ninaungana nawe Gentamycine
Umeongea kwa busara sana.
Sidhani kuwa ajali hii imetokana na mwendo kasi uliopitiliza (maana walioshuhudia ajali na magari waliyoongozana wangeshasema)..au kubeba uzito mkubwa kuliko uwezo wa gari ukizingatia abiria wengi ni wanafunzi ambao kwa wastani wa uzito hawazidi 50kg.

Hii ni ajali mbaya na ni hulka ya binadam kutafuta pa kutupa lawama baada ya maafa.
Tujizuie sote. Tuomboleze kwa amani.
 
baada ya msiba tunaomba Jeshi la Polisi lifanye uchunguzi wa kina na litoe taarifa juu ya chanzo na sababu ya ajali hii mbaya!!
 
 
Pale ilipojipigiza nyuma yake kuna mti mkubwa tu lakini basi ilipaa juu ya huu mti na kutua mbele yake.
 
Kwa kiasi flani yaweza kuwa kweli juu ya utunzaji wa kumbukumbu za service lakini kwa uzi wako mzima si lazima ikawa hivyo. Zipo sababu nyingi za kiufundi na kimazingira ambazo zinaweza kusababisha ajali. Kwa muda mwingine ajali haingalii umefanya service leo au jana, mazingira husika yanaweza kukufanya pia ukapata ajali. Cha msingi kila mtu atimize wajibu wake japo kila mtu atakufa kwa muda wake na style yake.
 
Imetokea,tunahitaji kujifunza hakuna haja ya kutuhumu watu....R.I.P
 

Gereji yako iko wapi mkuu
 
Hivi mwili wa dereva ulitambuliwa na kufanyiwa uchunguzi kujua kuwa alilewa au la? Sijui kuna utaratibu gani wa kiuchinguzi unaofanyika kujua hasa chanzo cha ajali ili ikiwezekana tahadhari zichukuliwe siku za usoni.
 
Ni kweli wamiliki wanaangalia faida kuliko usalama wa wateja wao
Ajali hii imenikumbusha Mwaka 74 kabla ya tv na internet huko Arusha ilitokea ajali pale Usa River ikaua watu 70. Walikuwa kwenye bus la kampuni ya TTBS. Watu wakapachika magari hayo Twende Tukafe Bila Sababu. Ulikuwa ni msiba wa kitaifa. RIP Our Little Angels. Sikumbuki vema jinsi serikali ilivyohandle huo msiba nilikuwa bado ufahamu si sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…