Ajali mbaya Dar yachukua uhai wa Kelvin Kavishe (Kaloosh)

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2012
Posts
6,067
Reaction score
10,938
Ajali hii imetokea jijini Dar, karibu na Ubalozi wa Kenya usiku wa kuamkia leo.

Pole sana wafiwa na wote walioguswa na msiba hasa mabinti wauza sura wa mjini (Wadada wa mjini).

Binafsi nimesikitika maana marehemu nimesoma nae japo nilikuwa darasa moja mbele yake.

RIP Kelvin Kaloosh


Gari baada ya kupata ajali (Eneo la Tukio)



Marehemu enzi za uhai wake

Majeruhi aliyekuwa na marehemu kwenye gari



 

Attachments

  • 12662462_1375711852446097_2914563462953588181_n.jpg
    18.4 KB · Views: 519
Duuuh hatari sana hii... Tujifunze kitu hapa waungwana...tu vijana na labda wengine tunafamilia; kumuacha mke, Watoto, ndugu jamaa na marafiki hiyo huumiza zaidi. Tuchukue tahadhari na kukwepa kuhatarisha maisha yetu kwa sababu zinazoweza epukika!

Tunywe kwa kiasi chetu. Zikikolea sana basi tusitafute kushindana na pedo ya mafuta na kukimbiza geji kuwahi home ama kuhama kiwanja kingine. Tuwe tunakumbushana wakati wa kupata kinywaji. Ikibidi mgombane kwa kumkataa aliyezidiwa kuwa dereva...hata kama gari ni lake. Uhai kwanza, Urafiki tutajenga upya.

Muwe na J2 njema na pole kwa wafiwa.
 
Mkuu unasema mabinti wauza sura ndiyo wameguswa zaidi una maana gani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…