mkuu hii dhana imeleta shida na vifo vingi sana Africa, kwa kuendelea kwetu kuendekeza huu ujinga na upumbavu tumeshindwa kutatua matatizo mengi ambayo yametufanya tuendelee kuwa masikini na kuachwa nyuma kwa kila kitu na dunia inayokimbia....
KUANZIA ASIA,ULAYA MPAKA AMERICA huwa hakuna kitu kinaitwa bahati mbaya, ila watu wa AFRICA tunaamini kuna bahati mbaya katika uzembe..
Uzembe huwa ni uzembe tu na hakuna namna nyingine,, huwezi ukawa na maisha duni wakati ulipata hela ukatombea, ukalewea na ujinga mwingi halafu ukawaambia watu wewe kuwa na maisha duni ni bahati mbaya, huwezi kuzembea shuleni na ukasumbua wale waliokulazimisha usome kwa bidii halafu siku za usoni mambo yako yakiwa magumu eti ukasema ni bahati mbaya...
hata vifungu vya bible vilishasema mahali "watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa" pia binadamu amepewa akili ili aitawale dunia...
ukifa kwa uzembe lazima watu wengine waambiwe MAREHEMU ALIKUWA MZEMBE, hii itasaidia watu wasirudie makosa ya Marehemu...
pia uzembe unaweza ukawa haujasababishwa na Marehemu ila kifo cha Marehemu kinaweza kuwa ni matokeo ya uzembe uliosababishwa na mzembe au wazembe wengine....
MKUU, WE ARE IN THE SAME BOAT, LETS WORK HARD....TUSIAMINI KWENYE BAHATI MBAYA, TUSIRUHUSU UZEMBE KWENYE MAISHA YETU...