Ajali Tanzania: Mawazo mbadala kuhusu udhibiti wa ajali Tanzania

Hivi kamanda Mpinga yupo humu JF?? Huyu mheshimiwa anatakiwa humu tumuulize maswali. Ana mengi sana ya kutuelimisha,na kufafanua.
Tunao viongozi na wafanyakazi wengi tu humu wa hizo idara ma vitengo nilivyotaja hapo juu ambao ni members humu
Tunahitaji maoni yao ushauri wao na nini kifanyike kukabiliana na hii hali ya sasa
si kwamba watu wanaendesha magari mbovu la hasha, magari mengi ya nayo pata ajali sasa hivi ni mapya/yaliyo katika hali nzuri
Shida kubwa ipo kwenye nidhamu ya barabarani, kuzifuata sheria kanuni na taratibu za barabarani! Kuzisoma na kuzielewa
TANROADS tena nao ni wadau wakubwa kabisa kwenye hili wasiishie kujenga na kuhimiza utunzaji wa barabara hata hili la elimu kwa madereva juu ya usalama wa barabara kwa muktadha wao inahitajika sana
 
Mkuu picha nyingine si nzuri kuweka humu hasa hiyo aliyokatika mguu pliiiiizzzz.... Naunga mkono hoja hasa kwa sisi vijana sijui kwa nini hatuheshimu vyombo vya moto
 
Mkuu picha nyingine si nzuri kuweka humu hasa hiyo aliyokatika mguu pliiiiizzzz.... Naunga mkono hoja hasa kwa sisi vijana sijui kwa nini hatuheshimu vyombo vya moto
Nimezingatia sana hilo Patrickn lakini sikuwa na namna ndio maana nikachagua hizi zenye afadhali kidogo na nyuso zao hazionekani
 
Hizo picha. Ajali hizi inapoteza wapendwa wetu. Watu wanakuwa walemavu. Tujifunze kupitia wengine sio mpaka yakukute.

We need to change. Hasa sisi vijana tuache mambo ya kutaka sifa mbele za watu.
 
Mkuu picha nyingine si nzuri kuweka humu hasa hiyo aliyokatika mguu pliiiiizzzz.... Naunga mkono hoja hasa kwa sisi vijana sijui kwa nini hatuheshimu vyombo vya moto
Nimezingatia sana hilo Patrickn lakini sikuwa na namna ndio maana nikachagua hizi zenye afadhali kidogo na nyuso zao hazionekani
Mkuu ni kweli hizi picha kidogo sio nzuri,zitakimbiza baadhi ya wachangiaji, labda ungeweka picha za magari yalivyoharibika tu, mimi mwenyewe nikifungua na scroll down haraka sana.
 
Mkuu ni kweli hizi picha kidogo sio nzuri,zitakimbiza baadhi ya wachangiaji, labda ungeweka picha za magari yalivyoharibika tu, mimi mwenyewe nikifungua na scroll down haraka sana.
Moderator aione hii kwakuwa ni ngumu tena mimi kutoa hizo picha! Natanguliza kuomba radhi
 
Kwa uchunguzi wangu mdogo sana hapa DAR nimegundua ajali nyingi hutokea kuanzia ijumaa usiku hadi jumapili alfajiri, kwa haraka haraka shughuli za weekend usiku ndio chanzo cha hizi ajali,na shughuli hizo huwa hazikamiliki bila pombe,guys please DO NOT DRINK AND DRIVE.
 
Breakdowns wanakwambia ndio siku za kazi na hata watu wa bima na magereji pamoja na traffic na vehicle inspectors ndio kipindi cha 'ulaji'
Ajali pia huongezeka kila wiki ya mwisho wa mwezi na kupungua sana katikati ya mwezi
 
Sio kila ajali ni mapenzi ya Mungu ajali nyingi ni uzembe na kutozingatia sheria za barabarani
 
Kampeni kama hizi zitiliwe mkazo na umakini zaidi ikibidi ziwepo siku maalum za kuhamasisha kufundisha na kuelekezana
Wiki ya nenda kwa usalama isiwe mara moja kwa mwaka
 
Breakdowns wanakwambia ndio siku za kazi na hata watu wa bima na magereji pamoja na traffic na vehicle inspectors ndio kipindi cha 'ulaji'
Ajali pia huongezeka kila wiki ya mwisho wa mwezi na kupungua sana katikati ya mwezi
khee makubwa kumbe ndiyo hivyo
 
mimi naona zile namba za itv wanazotangaza kwenye runinga Sumatra wangafanya zikabandikwa kwenye kila basi sehemu ambayo abiria wataona
maana watu huwa hawazikariri wala kusave ila zitasaidia kumuogopesha dereva apunguze mwendo
 
ila mkuu mshana picha zako ni very graphic, hakuna namna nyingine ya kufikisha point yako bila kuweka graphic pictures?
 
Angalia vichwa vya madereva wetu....hapo kuna kibao kabisa kuwa kuna kona kali lakini wanapitana hapo hapo! Ikitokea ajali kuna watu watasema ni kwasababu ya barabara na Mungu kapenda

Angalia vichwa vya madereva wetu....hapo kuna kibao kabisa kuwa kuna kona kali lakini wanapitana hapo hapo! Ikitokea ajali kuna watu watasema ni kwasababu ya barabara na Mungu kapenda

Au huyu hapa
Kwanza
-haruhusiwi ku overtake
-mbele kuna magari yanakuja
-kuna msururu wa wanao overtake na ku overtekiwa
Halafu wote wako kasi
 
Mkuu ni kweli hizi picha kidogo sio nzuri,zitakimbiza baadhi ya wachangiaji, labda ungeweka picha za magari yalivyoharibika tu, mimi mwenyewe nikifungua na scroll down haraka sana.

Inaonyesha wapenda sana dunia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…