Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwanza kama Mwananchi na mdau wa usafiri ninaumizwa sana na hizi ajali ambazo zinaendelea kuchukua uhai wa ndugu, jamaa na marafiki huku zikiacha wengi wakiwa na ulemavu.
Mkuu wa kitengo cha Usalama barabarani jana ametoa kauli ya kutoa matumaini sana kwa watanzania.
Kwa uzoefu uliopo ajali nyingi zinatokana na madereva wasio na elimu na kazi waifanyayo na kukosekana mikataba ya kazi na si mwendo kasi kama tunavyoamini sasa.
Mpinga ametangaza kuanzia jumatatu kila dereva atembee na cheti chake kilichomwezesha kupata leseni ya udereva kwa ajili ya ukaguzi.
Tuwe wakweli na wawazi madereva wengi wa haya magari ya abiria hawana sifa ya kuendesha hayo magari ila wanalindwa na askari wa Usalama barabarani hatimae kusababisha ajali na vifo.
Magari yanayokimbia sana yanajulikana, lakini ni nadra sana kusikia hizo bus kupata ajali Sababu madereva wanaelewa jukumu lao wakiwa barabarani.
Mwisho niombe tu wote kwa pamoja tushirikiane kuwafichua madereva wanaotumia vilevi njiani.
Khaa!! ©[® Basi tuendelee kufa tu kama kuku kama tunawategemea wanasiasa waje watuletee hali nzuriHiyo ni long term plan Mkuu, wanasiasa kwenye ilani za vyama vyao watakua nazo hizo..ila sasa itachukua 25 years ku implement hilo kwa viongozi wetu.Ngoja tujadili kinachowezekana sasa maana Vifo kila kukicha vinatokea wala havisubiri hizo barabara pana,treni za kisasa,ndege na Meli.
Mkuu umejaribu kueleza maoni yako kwa ufasaha ukimaanisha kua ndio dawa ya kutokomeza kabisa hili janga sugu la ajali za barabarani.Naomba unijibu maswali haya ili nijue kua umewaza mbali! 1.Je, kwanini nchi nyingi zilizoedelea huwezi kusikia ajali za magari zaidi ya matetemeko ya ardhi, moto,vimbunga, mafriko n.k? 2.Je,Mamlaka husika hutafuta angalao ushuari toka nchi zilizoendelea ili kulinusuru taifa na hili janga? 3 Kama wamepewa ushauri impact yake iko wapi? 4.Je, kama kuna taasisi zimelifanyia hili suala utafiti wa kutosha report ni kwa manufaa gani? 5.Je,nani alaumiwe?6.Ivi ni kwanin Tz imeshafikia sasa mtu ukisafiri usala wa maisha yako unakua"Fifty fifty"?
Hapo umesema kweli, lakini tujiulize nani wa kumshughulikia mwenzie, Labda kiundwe chombo kingine cha kuwachukulia hatua hawa askari.
Unapozungumzia nchi zilizoendelea ina imply vitu vingi sana kwanza vyombo vyao vya usafiri ni bora na salama kuliko vyetu, Mianya ya rushwa ni kidogo ukilinganisha na sisi hivyo si rahisi kumuhonga traffic hata kama gari lako lina makosa,Mamlaka zinazosimamia masuala ya usafiri ni makini na zinachukua hatua kuliko sisi ...yaani huwezi kukuta kiongozi anamiliki chombo cha usafiri hivyo ni rahisi kwa mmiliki wa chombo cha usafiri kuchukuliwa hatua endapo ataenda kinyume,Barabara zao ni bora na salama zaidi kuliko sisi, madereva wao wanalipwa mishahara mizuri kuliko sisi na wala hawaokotwi tu mtaani kama ilivyo kwetu, et al., Mamlaka husika hata kama ikipata ushauri ni kazi bure mpaka nilichokisema hapo juu kizingatiwe..Wakulaumiwa hebu na wewe fikiria kwa makini kwa sababu nilizotoa hapo kisha utamjua ni nani anafaa kulaumiwa.
ni kweli madereva wanachangia ajali ila kwa upande wa pili miundombinu yetu sio rafiki haimpi driver alternatives za kutosha anapokutana hali ya hatari.
barabara zikiboreshwa ajali zitapungua kwa kiac kikubwa mno.
serikali ilitumia kodi zetu nyingi kujenga mkongo wa taifa wa internet lakini bado haujatusaidia sana. Tuutumie huu mfumo kufunga camera barabarani kama zifanyavyo nchi zilizoendelea. Hii manpower ya kikosi cha usalama barabarani kutwa kushinda barabarani ingetumika kushinda kwenye computer na ku-monitor madereva wasiotii sheria za barabarani