Kwanza kabisa nikupongeze kwa kuguswa na hili na kutuletea mada yanye tija kwa kila mmoja wetu,nategemea kuwaona watu mkiweka maoni yenu hapa kuliko kushabikia siasa zinazojadili watu badala ya mijadala yenye tija kama hii.
Naungana na yote uliyoyasema isipokuwa hilo la mabasi kusafiri na Askari.
Mawazo yangu ili kudhibiti ajali ni lazima kwanza kutambua vyanzo vya ajali,
pamoja na vyanzo kuwa vingi lkn mwendo kasi na uzembe wa madereva ndio chanzo kikuu cha ajali za barabarani.
Suluhisho ni kuwapangia muda madereva kufika kwenye vituo.
Mfano mabasi yaondoke Dar saa 12.00 alfajiri na yafike morogoro saa 4:00 yafike Dodoma saa 8:00,yafike manyoni saa 9:30,Singida Saa 11:00,Misigiri saa 12.30, Igunga saa 1:50,Nzega Saa 2:30 na hatimae kahama saa 4:00.
Masaa hayo yapangwe kitaalamu na watu wa sumatra baada ya kujiridhisha umbali toka eneo moja kwenda eneo jingine,
Kila kituo kiwe na askari ambao wapo serious na kuwepo na utaratibu kama ule wa treni wa kupewa line clear,hivyo mtu atachukua kibali maalum mahala anapoanzia safari kinachoonyesha muda na atapaswa kukabidhi kibali hicho kwenye kituo cha mbele na kupewa kingine kinachomruhusu kuendelea na safari,afanye hivyo mpaka mwisho wa safari yake,.
ili kuepusha usumbufu maeneo vinapotolewa vibali pawepo na vyoo pamoja na hotel za kula chakula,lengo ni kutumia mudaa wa kuonyesha kibali huku abiria wakiruhusiwa kuchimba dawa na kupata chakula,hivyo hakutakuwa na malalamiko,
Kama hilo halitoshi tunaweza kuyatumia maeneo mizani kama check point ya muda wa kuwasili eneo husika.
tukifanya hivi italeta self control ya madereva ,adhabu yake iwe kuahirishwa safari na abiria kuwekwa katika mabasi mengine kwa kibali maalum na dereva kuwekwa ndani mwezi mmoja na gari kufungiwa kusafirisha abiria kwa muda wa mwezi mmoja.
kama tutafanya hayo hakika hakuna dereva wala mmiliki wa gari atakaefika eneo husika kabla ya wakati.
Kufanya hivyo kutawafanya madereva kutembea mwendo wa kawaida na hivyi kupunguza ajali kwa kiwango kikubwa.
Pendekezo hili ni baada ya safari yangu toka Dodoma,gari ya kwanza kufika Dodoma ilikuwa campuni ya KISBO ikiduatiwa na Leina na CITY BOY.
Hizi ni basi zilizojizolea umaarufu kwa kukimbia kupita kiasi kiasi cha kufika kahama saa 12:30 badala ya saa tatu usiku.
Tulipofika manyoni walisimama petrol station na kutueleza abiria kuwa tunasubiri muda wa kufika Singida.
ilikuwa saa 7:20 za mchana na singida tulipaswa kuingia kuanzia saa 10.30 au zaidi ya hapo.
Hivyo tulilazimika kukaa muda wa saa moja na nusu ndipo tukaendelea na safari,
Gari zoote zilizotoka Dar zilikuwa kama msafara na hakuna aliethubutu kukimbia,waliogopa faini kubwa ambayo hutozwa singida endapo Gari itafika kabla ya muda uliopangwa.
Mwisho ni kwetu wapiga kura ambao ndio wahanga wa ajali hizi,tusiwachague tena wafanyabishara kuwa wabunge wetu,maana wengi wao hutumia fursa ya vyeo vyao kuwafanya hata askari Polisii wayaogope magari yao.