Miye natofautiana kidogo na weye mshana jr. Ajali nyingi ni za kuchonga tu. Msilete mambo ya shule ya udereva. Miye nilijifunzia vichochoroni leo nina miaka 30 haijapita siku 7 bila miye kuendesha gari. Leseni yangu saaafiiii. Mbona waliokwenda shule hao madereva wa mabasi wote ndo hao wanaua watu kwa kishindo?? Kuanzia 10 kwenda juu on the spot??? Walipobadili leseni walisema ndio mtambo wa kupunguza ajali. Naona ni njia walibuni ya kuongeza ajali kwani ndipo zimezidi
Jamani, kiini hakipo kwenye leseni. Kiini ni mtu mwenyewe. Madereva Wasiendeshe gari wakiwa wamelewa ulevi wowote ule. Iwe bangi, au pombe au madawa. Ukishaona unayahitaji hayo, tafadhali, jali maisha ya watu uliobeba. Nadhani watu wazuri hapo ni wana saikolojia wabobevu, wenye uwezo wa kuijua tabia ya mtu mapema. Hao walevi wawachambue wawaweke kando.
Jingine ni malipo kwa madereva hao. Tajiri unamkabidhi mali ya mamilioni huyo dereva, anakupelekea mizigo halafu weye unaweka kibindoni mamilioni unamlipa senti. Haki iko wapi?? Serekali ianzishe ajira ya madereva wa magari ya abiria na magari makubwa. Kiwe ni kitengo rasmi na yeyote anayetaka dereva, aende huko akapewe dereva mtaalam. Nasema; Serekali ili iweze kuwadhibiti.
Jingine: Njia zetu/ barabara zetu. Haya ni makaburi wazi kabisa. Ukitaka kumpisha huyo kichaa anayekuja mbele yako, tiyari umetumbukia mtoni/korongoni. Gari ikiacha njia kidogo tu, kuirudisha barabarani ni shida. HATUNA MAINJINIA TZ. Hao ni vioo tu vya kujiangalia. Wapate 10% yao baasi.
Serekali, itengeneze barabara sio hivi vichochoro. Umeona hapo hayo magari yanavyo ovatekiana?? Mpaka vioo vya kuangalia nyuma kidogo ving'olewe! Hiyo ni njia au uchochoro??
Vichaa wapo kila sekta, hivyo yule mstaarab anayekuja mbele yako, achepukie kando apishe huyo kichaa apite. Lakini barabara haimruhusu, hivyo anajikuta ni uso kwa uso tu.
Nadhani hizi ni baadhi tu ya sababu. Naomba barabara zetu zipanuliwe, hata kama sio kwa lami lakini zijazwe moramu kando kando kuruhusu gari ichepukie huko kuepesha uso kwa uso lakini gari isitumbikie isikoweza kutoka