Najiuliza tu maelezo ya Mkuu wa Wilaya, anadai gari lililokuwa limebeba makaa ya mawe, hivi hayo makaa ya mawe yalikuwa yanasafirishwa kwenda wapi? Je Waandishi wameona hilo gari la makaa ya mawe?
Kingine anadai dereva wa gari kubwa aliumia japo si saana, lakini baadae akaruhusiwa aende akajitibie hospitali kubwa baada ya kuanza kutapika damu kidogo.
Hivi hospitali ya Handeni haiwezi tibu mtu anae tapika damu kidogo? Dereva alikuwa ana traffic case, iweje mmruhusu bila kufuata taratibu kupata maelezo yake na kuwa chini ya ulinzi?
Hata msaidizi wa dereve hatujaelezwa alikuwa nani na jina la huyo dreva kama ilivyo katika ajali nyingine.
Waandishi wa habari wafuatilie kujua alipo dereva wa gari kubwa lililogongana na gari ya balozi, na waihoji serikali, daktari wa Handeni, na polisi ni vipi dereva wa gari hilo kubwa ati kuruhusiwa kwenda kupata matibabu zaidi bila taratibu za kipolisi, na hospitali walishindwa nini kumtibia?
Hospitali ya wilaya ya Handeni ni kubwa haiwezi shindwa mtibu mtu anaeanza tapika damu. Huyu Dreva na msaidizi wake wajulikane tafadhali!
Mkuu wa wilaya kawa msemaji wa Polisi, Msemaji wa Daktari, ndo maana hajatoa habari kamili kwa umma, jina la dereva, yupo wapi, na nini kinafanyika kwa mujibu wa sheria juu ya ajali iliyotokea. Ni kama vile balozi kafa basi kwisha habari yake, serikali haina muda.