Mkuu Mpita Njia naungana nawe kwamba shimo linaloonekana kwenye picha ni dogo sana kusababisha ajali mbaya kama hiyo hasa kwa gari ya kazi kama landcruiser. Hata hivyo maelezo ya dereva anasema kuwa, wakati yupo kwenye jitihada za kukwepa shimo, lori likagonga kwa nyuma na kusababisha gari kupinduka mara 4. (Hii ni kwa mujibu wa bbc/swahili
Na kama ni kweli tairi lilichomoka, basi clue ya mahali lilipolala gari (Makambako) ni muhimu.
Shangaa kuwa licha ya first insight kutoka kwa wana JF kuhusiana na ajali hii,bado kuna contradictions nyingi sana tu.
Sasa hapo juu ina maana kuwa ni magari matatu yamehusika kwenye ajali ama ni mawili tu? Maana inawezekana vipi kugongwa kwa nyuma na gari ambalo uko kwenye process ya kuli overtake?
No wonder dereva yuko chini ya ulinzi wa polisi kwasababu inawezekana ana ya kujibu kutokana na stories tofauti tofauti anazozitoa kuhusiana na nini haswa kilichosababisha ajali hiyo,na inconstencies kama hizo hupelekea mawazo ya wanachi kuwander na kujiuliza how come?
Dillunga,kama unajuwa,then ni wazi utaelewa ninachotaka kusema,kipindi cha nyuma na pengine hadi sasa,matajiri wakipata taarifa ya ajali ya gari ama lori lake,basi kitu cha kwanza wanachouliza ni hali ya gari na si hali ya dereva,ilikuwa ni kama utamaduni na baadhi yao waliligunduwa hilo na kuanza kuulizia hali ya dereva na konda,then hali ya gari. Mfano huu hapo juu hauko directly linked na uliyasema hapo nyuma kuwa Mwakyembe alitakiwa amtake care dereva. Ikija kwenye ajali,wote ni victims tu. MKJJ keshaelezea kwenye posting yake na hivyo sioni umuhimu wa kuendeleza yale yale ambayo yameshasemwa,cha msingi ni kwamba wote walikuwa wakihitaji huduma za matibabu na wako under control huku madaktari wakiwa monitor na kuwapa ushauri wa hapa na pale kama kumpumzika,kutoongea nk. Kuna uwezekano mkubwa sana kuwa Mwakyembe alimuulizia mgonjwa/victim mwenzake,mara nyingi sana victims waliopata ajali pamoja huwa wanaulizia kuhusu wenzao.
Nguvu unayotaka aitumie Mwakyembe haina anything to do with hospital's rules and regulations na ushauri wa madokta,labda kama ulijisahahu ukadhani yuko bungeni na kwahivyo anatakiwa kupiga kelele.
Dokta pamoja na udokta na ubunge wake, hawezi kuingilia shughuli za profeesionals na wakati na wakati hawezi kujifanyia uchunguzi wenyewe ili kuweza kujua ni madhara kiasi gani amepata. Hata alipopelekwa MOI,si yeye aliamuwa ni madaktari,kwa maana kwamba anaweza akawa alivunjika ama kupata fracture. Kujaribu kusema Mwakyembe alitakiwa kutoa uamuzi wa nini kifanyike kimatibabu kwa dereva wake ni uonevu usiokuwa na mpango.