FMES,
Huku Kyela wakati wa matatizo wananchi wote wanaungana kwa pamoja na hata sasa kila mtu amefurahi kusikia mbunge wao yu salama. Kwa kifupi wanamtakia heri mwanao apate nafuu.
Ila kuna jambo ambalo linaongelewa mara nyingi ambalo ni la Mwakyembe kupenda kutembea usiku. Kila mtu anasema hivyo hivyo, ashauriwe aache kusafiri usiku. Mimi sikujua hili lakini ndilo linaongelewa zaidi.
Kitu ambacho labda waandishi wetu pamoja na polisi wameshindwa kufanya uchunguzi, ni je ni kweli Mwakyembe alilala Makambako? Kama alilala makambako waliondoka hapo saa ngapi? Kutoka Makambako mpaka Ifunda kisheria ni masaa sio chini ya matatu, kama walifika Ifunda kwenye saa moja, kuna mawili, waliondoka mapema sana au walikuwa wanakimbia sana.
Pia inasemekana waliondoka Kyela saa mbili usiku; kutoka Kyela mpaka Makambako ni kama masaa matano kama unafuata sheria za barabarani. Sasa kama ni kweli ina maana walifika Makambako masaa ya saa saba, watafute guest na kulala na kuondoka kama saa kumi asubuhi, je ina make sense?
Kitu kingine ambacho inatakiwa kujua mnapochangia hili jambo ni kwamba Mwakyembe anamwamini sana huyo dereva wake. Kwenye mikutano yake mingi hudiriki hata kusema kuna watu wamejaribu kumpa mamilioni huyo dereva ili amwue lakini dereva siku zote anakataa. Huwa najiuliza kama kuna hayo mambo kwanini hawaendi polisi? Labda ni maneno ya kisiasa zaidi kuliko ukweli. Kilicho ukweli ni kwamba Mwakyembe anamwamini sana huyo dereva wake na ningetegemea kabisa afanye lolote lile kujaribu kumwokoa asiingie matatizoni.
Jambo lingine ambalo sio muhimu sana lakini wote tunajua mzee akiwa na pressure, familia yote mpaka wafanyakazi wote wanakuwa na pressure kubwa. Wiki mbili zilizopita mheshimiwa alipata pressure kubwa sana baada ya kuona ghafla upepo umebadilika Kyela. Mwakyembe ni msomi na anajua kusoma alama za wakati, kwa kweli kilichotokea kwenye hicho kikao cha halmashauri ya CCM na yaliyofuatia baada ya hapo yalimchanganya sana. Kwa kifupi ni kwamba ali panic kuona watu wamepata courage ya kusema mambo ambayo miezi michache huko nyuma wasingediriki kusema. Kwahiyo mpaka Mwakyembe anaondoka Kyela juzi, alikuwa ni mtu mwenye pressure hata kwa kumwangalia tu. Alifanya mikutano kadhaa na kutembelea baadhi ya kata kama njia ya kukabiliana na mashambulizi lakini alionekana kuwa na wasiwasi na kutumia muda mwingi kuongelewa kuandaliwa kwa milioni 400 za kummaliza yeye kisiasa. Lakini wilaya ya Kyela ni ndogo sana, mtu akimwaga hata milioni 10 itaonekana tu.
Pia sikujua kumbe Mwakyembe na dereva wake wote huwa wanatembea na pistol muda wote, kwanini? labda ndio kulinda usalama wake. Kutembea na silaha ni hatari sana, afadhali hata waheshimiwa waajiri walinzi kama wanaona maisha yao yako hatarini, vinginevyo tusije tukashangaa tukisikia yale ya Dotto. Kyela watu wengi kumbe wanajua hilo la kutembea na silaha muda wote.
Muhimu kwasasa ni kumwombea mwakyembe apone kabisa na tuendelee na mambo ya kujenga nchi yetu kuelekea uchaguzi 2010. Nimjuavyo Mwakyembe sitashangaa kusikia kwenye mikutano yake ya Kyela hasa huko vijijini akisema kulikuwa na mkono wa mafisadi na walitaka kumwua.