Ajali ya Dr. Mwakyembe na yatokanayo

Ajali ya Dr. Mwakyembe na yatokanayo

JF HOME OF GREAT THINKERS.

Wewe unafikiri hao matrafiki wanatumia nguvu za Mungu au GIZA? yaani sipati picha hapa unamaanisha nini wangewezaje kuzuia ajali isitokee kutoka kwenye gari tofauti?

Hivi kwenye speed ya 120km/hr unashindwa kukwepa LORI? du madereva tusaidie isijekuwa huyu dreva aliover take bila ya kuwa makini alafu mnataka kusingizia yaani kila tukio mnataka kulihusisha na mafisadi? KESHO MVUA ZITAKOSA NJI NZIMA NA MTASEMA KUNA MKONO WA MTU

WAKE UP PLEASE!!!!!

Mimi nadhani wangeweza kusoma hata namba za lile lori iliitusaidie kulitafuta baadae!
 
Mr Mwakyembe explained that a lorry was overtaking his car and suddenly a minibus appeared on the opposite direction.

“That is when my driver decided to accelerate so that he could allow the lorry to go back. But the lorry kept on accelerating as well and knocked my car from the back causing it to lose direction before knocking a tree and overturned,” he said.

Gari ya Mh Mwakyembe ilikuwa katika mwendo wa kasi.
Dereva wa mwakyembe hakufanya maamuzi sahihi, kitendo chake cha kuongeza mwendo kingeweza kusababisha lorry kugongana na basi la abiria.
Kwa mantiki hiyo basi, inawezekana dereva wa lorry alipoona kuwa gari la Mwakyembe linaongeza mwendo njia sahihi ya kuepusha ajali na basi ni kuilazimisha land cruiser isalimu amri.
Huo uamuzi una hasara na faida zake, kwa hiyo tunaweza kuangalia ni zipi hasara na je zipi ni faida.
Bottom line kama lorry tayari lilikuwa limeruhusiwa kuipita gari ya mheshimiwa basi hakukuwa na sababu za dereva wa mheshimiwa kuongeza mwendo.
 
Duuu!!! hawa ma-expert tulionao hapa JF nafuu hata ya sheikh Yahaya...
 
Ndio maana kuna mdau humu ndani kapendekeza kuwepo kwa jukwaa la falsafa ili watu wawe wanaongea mambo kwa hoja!!!Naamini wale watakaohisi hivyo, basi watawashuku mafisadi kuwa ndio walio nyuma ya pazia!! Nahisi leo hii endapo RA akiulizwa kati ya Mwakyembe na Mengi ni nani auawe basi bila shaka atampendekeza Mengi kwavile ndie anayewashupalia zaidi!!! Mwakyembe aliagizwa na bunge kufanya kazi aliyofanya ;lakini Mengi anawasakama mafisadi kwa utashi wake!! Kama tukiamua kutumia neno kimbelembele, je ni nani hapo kimbelembele kati ya RA na RM?
 
Hata mimi nilipatwa na mstuko kusikia kwamba baada ya kulipita lori na kukanyaga kakorongo kadogo (niliona kupitia TV korongo lenyewe) eti tairi likachomoka. Mara ngapi mavx yanapita full mwendo kwenye njia zenye mahandaki na yasing'oke tairi walakubiduka na iwe rahisi kwenye lami??? Ichunguzwe hii. Mh! naiogopa siasa kama ukoma. na ubongo wangu unakataa kuwa ajali hii n ajali tu!
 
Wakuu,

Hivi hii sio sawa na -Road rage!

Madai ya Derava na Dr yote yanaelekea kuonyesha walikuwa wanafukuzana. Yaani Dereva wa Mwakyembe na dereva wa lori.

What is the fuss?

Ajali ni ajali.
 
Majasusi waliofuzu kuuwa kwa ajali it's the last resort [tena zamani ] and risky kwani mara nyingi target wanakuwa na uwezekano wa kupona.

Eyewitness wanaweza kutokea, na pia inampa target muda wa kuwasiliana kuomba msaada pale anapohisi gari inamfuatilia na haitaki kupita au kupitwa... na hawawezi kutumia lori ambalo halina maneuvering flexibility ku-escape baada ya tukio... na zaidi ya yote ku-eliminate kwa kutumia gari kuna risky pia kwa agent kuwa involved kwenye accident [refer kifo cha Sokoine gari ya Dube iliyosababisha ajali ilishindwa kuondoka, iliumia, target mwenyewe (kama kweli) hakuweza kufa na inahisiwa alijaribu kukimbia akawa hit from the back (chest)]....

So who wants to risk?... Refer uuaji wa the most feared UGANDA RESEARCH BUREAU..... Mara zote ajali walizokuwa waki plant targets walipona ..na iliwalazimu kuyapindua magari na kuyachoma moto... kiasi hata mtoto mdogo akiangalia alijuwa ni USR involved!!! ...angalia kifo cha Princess Diana cha ajali hadi leo kimeacha doa kwa M15.. [wengi wanadhani mapaparazi waliwakimbiza wakijuwa along the way wangeweza kupata ajali, na pia inaaminika kuwa ambulance ya kwanza kufika ilichelewesha kutoa huduma ya kwanza iliyohitajika kwani walikuwa hawajakata roho]. Inakuwa rahisi sana watu kugundua.

Ingekuwa ajali ya Mwakyembe ni ujasusi lazima kungekuwa na gari la surveillance nyuma ambao jukumu lao lingekuwa kujifanya wanatoa msaada baada ya ajali na jukumu lao ni kumalizia kazi kama wangekuta bado asingepona.!

Nafikiri tuache speculations kwani hali ya barabara zetu inajulikana tena ni bahati sana kwa barabara za highland ...huwa kuna maporomoko marefu sana ambako gari ikiingia hata kuinasua ni kazi na msaada wa majeruhi labda mlete helicopter...

Kuna uwezekano kwamba ajali ile ilipangwa lakini unajua tena jamaa ndo wanaimarisha kikosi chao cha majasusi wa kuua. Kilicho wachanganye ni kwamba Dk. mwakyembe alishaambiwa wakati anakwenda kulala makambako kwamba abadilishe muda wa kuondoka bila kumjulisha yoyote hata dereva wake.

Lori lililo wagonga lililala njiani kwenye kijiji fulani, surveillance walipoona gari la mwakyembe limeondoka mapema nadhani wali wasiliana na jamaa kwamba watembee jamaa anakuja. Kisa cha kukataa kuwapisha ni ili wasogee kwenye bonde ambalo liko km 3 kutoka pale walipopata ajali na pale angefanya anawapisha na kisha kuwaporoshea shimoni, hapo nobody could escape.

Kikosi hicho cha wauaji zamani kilikuwa kinakodiwa lakini sasa wanajaribu kukiunda kiwe imara hapa hapa TZ.
 
Wakuu,

Naomba kuelimishwa, hawa majasusi ni wanani?

Waserikali?

Majasusi tuu?

Mafisadi?

Wapinzani?

Ni wa nani hawa majasusi katika hao hapo juu?

Hivi kulogana nao ujasusi?
 
Mr Mwakyembe explained that a lorry was overtaking his car and suddenly a minibus appeared on the opposite direction.

“That is when my driver decided to accelerate so that he could allow the lorry to go back. But the lorry kept on accelerating as well and knocked my car from the back causing it to lose direction before knocking a tree and overturned,” he said.

Maelezo ya awali na hayo hapo juu yanasigana. hii inaonyesha something wrong ktk maelezo ya driver. Ni nani aliyekuwa akimpita mwenzie? ni dereva wa lorry au ni dereva wa Dr.?

IT IS CONFUSSING!!!!!
 
from mroki blog
 
Attachments

  • 3.JPG
    3.JPG
    34.6 KB · Views: 34
  • 4.JPG
    4.JPG
    58.2 KB · Views: 30
Maelezo ya awali na hayo hapo juu yanasigana. hii inaonyesha something wrong ktk maelezo ya driver. Ni nani aliyekuwa akimpita mwenzie? ni dereva wa lorry au ni dereva wa Dr.?

IT IS CONFUSSING!!!!!

Gari la Dk. mwakyembe lilikuwa likilipita lori ndo kabla hawajalipita kabisa, dereva wa lori akaongeza mwendo wakawa kama wako sambamba ndo dereva wa lori akarudi kulia hivyo kuigonga landcruiser kwenye taa ya kushoto (upande alikokuwa Dk mwakyembe) hivyo likaserereka, kupoteza mwelekeo na kupinduka.
 
Nimepata fununu kuwa ajali ya Mh Mwakyembe ilikuwa imepagwa kwa makusudi ya kumuondoa. Tz ni nchi yenye fununu nyingi na mwanzoni nilipomsikia RPC wa Iringa akizungumzia ajali hiyo kwenye vyombo vya habari niliamini ni ajali ya kawaida.

Jana, dereva wa Mwakyembe alikaririwa akidai kuwa aligongwa kwa nyuma na lori na kusababisha ajali tofauti na RPC wa Iringa. Kauli ya dereva wa Mwakyembe niliipuuza na kuona labda kachanganyikiwa au alikuwa anaona 'mauza-uza' ambayo baadhi ya madereva hydai kukutana nayo kabla ya ajali na badala yake nikamwamini RPC wa Irainga.

Leo Dk Mwakyembe kazungumza. Nimemsikia akisema kuwa walikuwa wakijaribu kumpita dereva wa lile lori lakini wakati dereva wa lori lile hakuwa anataka apitwe na gari ya Mwakyembe! Na walipokuwa wakimpita aliongeza mwendo na kusababisha kugongwa na lori kwa nyuma na hivyo kusukumwa na kupinduka. MAelezo ya Dk Mwakyembe yanashabihiana na maelezo ya Dereva wake ambyo niliyachukia kama ni kujitetea tu kwa uzembe wake.

Maelezo haya ya Mwakyembe ndiyo yananipelekea nianze kuchukulia kwa uzito tetesi za uwezekan wa kupangwa kwa ajaili hiyo. HAdi sasa sijasikia kukamatwa kwa dereva wa lori lile wa lori lenyewe azidi ya kusikia kuwa Dereva wa Mwakyembe aliwekwa chini ya ulinzi wa polisi! Je, dereva wa lori na lori lenyewe yuko wapi?

Mwaka jana ajali ya namna hiyo ilimpoteza Mbnge Salome Mbatia Iringa na tuliambiwa kuwa dereva wa lori alikamatwa (sijui kesi ilienda na kuisha vipi). LAkini baada a ajali hiyo tukasikia kuwa mlengwa alikuwa Mh. Zitto abaye ndiye aliyewasaidia majeruhi wa ajali hiyo Zito mwenyewe akathibitisha hayo.

Ni vema tusiichulie ajali hiyo kirahisi rahisi ikizingatia kuwa mwaka jana ilisemekana Mwakyembe alilishwa sumu (ingawa haikuthibitishwa na yeyote) na wazee wa Kyela wakasema watapambana na yeyote anayetishia uhai wa Mbunge wao kupitia njia za giza. Pia tukumbuke kauli ya Mengi kuwa Mafisadi wanamtishia kifo (tukumbuke pia kuwa Mengi na Mwakyembe na Selelii walikuwa mikoa ya Ziwa kwenye ziara ambazo walizungumzia sana mapambano dhidi ya ufisadi).

Wana JF ni vema tuchukulie tetesi hizi kwa uzito unaostahili,
Hakuna lolote lililopangwa.Dreva alitaka kulipita gari lililo na trela hakuweza kutambua kuwa kulikuwa na ufinyu wa barabara.Ukeli barabara za mkoa wa iringa ni mbaya sana ku-overtake kwani pembeni kuna mashimo.Dereva wa ROLI ALIKWEPA SHIMO ILIHALI NA DEREVA WA mWAKYEMBE ALIKUWA ANA-OVERTAKE KATIKA KUKWEPA NAYE AKAINGIA SHIMO LA UPANDE WA PILI.MIMI MWENYEWE NILINUSURIKA ENEO HILO NIKIWA NJIANI KWENDA NJOMBE TOKA DAR
 
Huu ushabiki wa kupindukia utaharibu uwezo wetu wa kufikiria na kuchambua mambo,gari la Mwakyembe ndilo lililokuwa linaipita lori na walikuwa wanaelekea upande mmoja na maelezo ya dereva wa Mwakyembe yanajitosheleza-aliingia shimo kando ya barabara akiwa kwenye mwendo wa kasi na kupoteza umiliki wa gari-FULLSTOP!
 
- Wakuu Nsaji, Engineer na Lazaro vipi jamani tupeni uptodates au? Mana naona maneno mengi sana hapa, damn hebu tupeni dataz huko wakuu!

- Nsaji Mpoki vipi mkuu hakuna habari za uhakika huko? Binafsi nitaanza kuzitafuta rasmi dataz kuanzia kesho, otherwise tupeni dataz wakuu!.

FMEs!

FMES,

Huku Kyela wakati wa matatizo wananchi wote wanaungana kwa pamoja na hata sasa kila mtu amefurahi kusikia mbunge wao yu salama. Kwa kifupi wanamtakia heri mwanao apate nafuu.

Ila kuna jambo ambalo linaongelewa mara nyingi ambalo ni la Mwakyembe kupenda kutembea usiku. Kila mtu anasema hivyo hivyo, ashauriwe aache kusafiri usiku. Mimi sikujua hili lakini ndilo linaongelewa zaidi.

Kitu ambacho labda waandishi wetu pamoja na polisi wameshindwa kufanya uchunguzi, ni je ni kweli Mwakyembe alilala Makambako? Kama alilala makambako waliondoka hapo saa ngapi? Kutoka Makambako mpaka Ifunda kisheria ni masaa sio chini ya matatu, kama walifika Ifunda kwenye saa moja, kuna mawili, waliondoka mapema sana au walikuwa wanakimbia sana.

Pia inasemekana waliondoka Kyela saa mbili usiku; kutoka Kyela mpaka Makambako ni kama masaa matano kama unafuata sheria za barabarani. Sasa kama ni kweli ina maana walifika Makambako masaa ya saa saba, watafute guest na kulala na kuondoka kama saa kumi asubuhi, je ina make sense?

Kitu kingine ambacho inatakiwa kujua mnapochangia hili jambo ni kwamba Mwakyembe anamwamini sana huyo dereva wake. Kwenye mikutano yake mingi hudiriki hata kusema kuna watu wamejaribu kumpa mamilioni huyo dereva ili amwue lakini dereva siku zote anakataa. Huwa najiuliza kama kuna hayo mambo kwanini hawaendi polisi? Labda ni maneno ya kisiasa zaidi kuliko ukweli. Kilicho ukweli ni kwamba Mwakyembe anamwamini sana huyo dereva wake na ningetegemea kabisa afanye lolote lile kujaribu kumwokoa asiingie matatizoni.

Jambo lingine ambalo sio muhimu sana lakini wote tunajua mzee akiwa na pressure, familia yote mpaka wafanyakazi wote wanakuwa na pressure kubwa. Wiki mbili zilizopita mheshimiwa alipata pressure kubwa sana baada ya kuona ghafla upepo umebadilika Kyela. Mwakyembe ni msomi na anajua kusoma alama za wakati, kwa kweli kilichotokea kwenye hicho kikao cha halmashauri ya CCM na yaliyofuatia baada ya hapo yalimchanganya sana. Kwa kifupi ni kwamba ali panic kuona watu wamepata courage ya kusema mambo ambayo miezi michache huko nyuma wasingediriki kusema. Kwahiyo mpaka Mwakyembe anaondoka Kyela juzi, alikuwa ni mtu mwenye pressure hata kwa kumwangalia tu. Alifanya mikutano kadhaa na kutembelea baadhi ya kata kama njia ya kukabiliana na mashambulizi lakini alionekana kuwa na wasiwasi na kutumia muda mwingi kuongelewa kuandaliwa kwa milioni 400 za kummaliza yeye kisiasa. Lakini wilaya ya Kyela ni ndogo sana, mtu akimwaga hata milioni 10 itaonekana tu.

Pia sikujua kumbe Mwakyembe na dereva wake wote huwa wanatembea na pistol muda wote, kwanini? labda ndio kulinda usalama wake. Kutembea na silaha ni hatari sana, afadhali hata waheshimiwa waajiri walinzi kama wanaona maisha yao yako hatarini, vinginevyo tusije tukashangaa tukisikia yale ya Dotto. Kyela watu wengi kumbe wanajua hilo la kutembea na silaha muda wote.

Muhimu kwasasa ni kumwombea mwakyembe apone kabisa na tuendelee na mambo ya kujenga nchi yetu kuelekea uchaguzi 2010. Nimjuavyo Mwakyembe sitashangaa kusikia kwenye mikutano yake ya Kyela hasa huko vijijini akisema kulikuwa na mkono wa mafisadi na walitaka kumwua.
 
Engineer asante sana kwa mukhtasari wa habari kuhusiana na Mwakyembe na upepo wa kisiasa huko Kyela.

Dereva anaweza kuwa anajua siri za nyumba ndogo pia, hazivujishi, ndio maana anaaminiwa na boss wake (ni mtazamo wangu, msijenitoa macho bure). Ni dereva mzuri.
 
mbona maneno yooote in bold lakini kwenye hisia zako umeweka maneno madooogo...kuna balaa unataka zua?

engineer story yako seems prejudiced mara mwakyembe kaondoka na pressure? mara hachelewi kusema mafisadi wanataka kumuua...(wewe upo kichwani kwake au?)
 
Kapinga,

Ungekuwa umewahi kuhudhuria hata mkutano mmoja wa Mwakyembe huku vijijini labda ungejua ukweli. Nimesema sitashangaa, time will tell kama niko sahihi au la.

Nimeandika ninayojua na jinsi ninavyoona mimi. Sikumpima Mwakyembe na kuona kama kweli alikuwa na pressure ila kwa nilivyomwona mimi alionekana kuwa na pressure na hata Kyela watu walio wengi wakiwemo wapambe wake wanasema hivyo hivyo kwamba mkubwa kapata pressure ila wanaamini atajibu mapigo.
 
hapa sawa, even the tone of ur wording zipo assuring but not as confirming kama mwanzo...tuwe makini tunapoanza kuongelea hadi mawazo ya watu! inakuwa ngumu kumeza.
 
Katika hili lolote linawezekana, nashangaa mafisadi tunaowapigia kelele kila siku hutasikia wamepatwa na ajali!

Ama kweli Dua la kuku halimpati mwewe!
 
Back
Top Bottom