Ajali ya Dr. Mwakyembe na yatokanayo

Ajali ya Dr. Mwakyembe na yatokanayo

Good news: Kwa mujibu wa taarifa ya habari ya TBC, 30 minutes ago, Dr Mwakyembe ameruhusiwa kutoka hospitalini baada ya dakatari aliyekuwa anamtibu kuridhika kwamba anaendelea vizuri.
 
Wasi wasi wangy unakuwa kwa kauli ya polisi Nyombi, ina maana yeye wakati wa tukio alikuwepo? kwani alijuaje kama taili lilichomoka? alielezwa na habari hiyo na nani?
Eh Mungu mponye mtumwa wkoo haraka.
 
Mheshimiwa Mwakyembe ameweza kuongea leo, yeye amesema amemwachia Mungu kwa maana yeye ni Mkristo na kama ilikuwa ni ajali ya kawaida basi anamwachia Mungu na kama kuna mkono wa mtu yaani hiyo ajali ilikuwa planted basi anamshitakia Mungu, ameweza kudeclair yeye mwenyewe kuwa gari lake liligongwa kwa nyuma ingawa anasema liligongwa kidogo kwenye taa ya nyuma so likaongeza motion ya gari lae na dereva waka akapanic baada ya kuona hawezi kulimudu ndo akalitoa nje ya road reserve sasa hapa nafurahi mno kusikia yeye mwenyewe amesema hivyo sijui kamanda Nyombi ataendelea kushikilia msimamo wake kuwa tairi imechomoka dah... Namuamini sana huyu mtu maana anasimama kwenye ukweli daima... Go Mwakyembe Gooo tupo nyuma yako

Shukran kwa taarifa Waga,inaweza ikawa ajali na pia inaweza ikawa ni mbinu za mafisadi,haiwezekani sisi tuseme moja kwa moja kuwa gari hilo jingine liliwagonga kwa bahati mbaya tu,maelezo ya dereva pamoja na mazingira ya ajali yenyewe yanaonyesha kuwa ni kama walikuwa wanafukuzwa na gari lililokuwa nyuma yao.
Kwa wale wanaojuwa utaalam wa polisi kwenye high speed chasing,utagunduwa kuwa huwa wanaligonga gari kwenye kona ya taa ya nyuma na gari hupoteza mwelkeo,wala huwa hawagongi kwa nguvu,kidogo tu na gari inaspin ama kupinduka...Who knows thats what happened? Anything is possible.
 
Je Mh Mwakyembe naye keshaongea? Aliyoyasema ni sawa na dereva? Tuwekee hapa maelezo ya alichosema kama ukiweza. Maana kama unafutilia mjadala huu utaweza kuona kuwa tunasubiri Mwakyembe apate nafuu ili na yeye aseme yaliyowasibu.
Mh. ameongea na driver wake ameeleza vizuri tu.
Wamesema bada yakupita Ifunda, kulikua na semi trailer inatembea polepole wakaomba kupita, driver akawaruhusu lakini waliposogea mbele driver akasogea kwao, driver wa Mh alibidi aongeze mwendo kukwepa wakagongwa kidogo taa ya nyuma. Wakati ameongeza mwendo ndio akaingia lile shimo aka lose mwelekeo wakapinduka.Mbele kwambali kuna coaster ilikua inakuja.
 
Ni muhimu tuendelee kupeana taarifa kuhusu hali ya huyu mpiganaji wetu. Pia tunahitaji kuhimiza na kufuatilia uchunguzi wa ajali yenyewe. Kwa mfano kuna taarifa (e.g. Mwananchi newspaper ya 22/5/2009) kuwa wakati gari ya Mwakyembe inaingia shimoni na kuanza kupinduka, kuna lori liliigonga kwa nyuma. Je, dereva wa lori hilo amefuatiliwa ili kusaidia kutoa taarifa za ajali? Ni muhimu kuondoa mashaka ya watu kuhusu uwezekano wa 'mkono wa mtu' katika ajali kama hii.
 
... pia inaweza ikawa ni mbinu za mafisadi,haiwezekani sisi tuseme moja kwa moja kuwa gari hilo jingine liliwagonga kwa bahati mbaya tu,maelezo ya dereva pamoja na mazingira ya ajali yenyewe yanaonyesha kuwa ni kama walikuwa wanafukuzwa na gari lililokuwa nyuma yao.


Hapo huamini?

Kwa wale wanaojuwa utaalam wa polisi kwenye high speed chasing,utagunduwa kuwa huwa wanaligonga gari kwenye kona ya taa ya nyuma na gari hupoteza mwelkeo,wala huwa hawagongi kwa nguvu,kidogo tu na gari inaspin ama kupinduka...Who knows thats what happened?

hapa unaamini?
 
A new story:

[FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif]•[/FONT]Mwakyembe apata ajali (Uhuru) NA ANITA BOMA, IRINGA

MBUNGE wa Kyela, Dk. Harrison Mwakyembe (CCM), amenusurika kifo katika ajali ya barabarani iliyotokea jana asubuhi katika eneo la Ihemi, Iringa Vijijini.

Ajali hiyo iliyotokea saa 1.10 asuhuhi, pia ilimhusisha dereva wake Joseph Msuya (36), ambapo gari walilokuwa wakisafiria kutoka Mbeya kuelekea Dar es Salaam liligonga mti na kupinduka.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Iringa, Advocate Nyombi, alisema Dk. Mwakyembe alipata ajali akiwa kwenye gari lake lenye namba za usajili T 362 ACH, Toyota Land Cruiser.

Kwa mujibu wa Kamanda Nyombi, chanzo cha ajali hiyo ni dereva kutaka kulipita lori, ambapo ghafla gurudumu la mbele lilitumbukia kwenye shimo lililokwa katikati ya barabara, hivyo tairi kuchomoka na baadaye gari kuacha njia na kugonga mti kabla ya kupinduka. (gademu!! we could call this the Unified Theory of all Tanzanian Accidents! M.M.)

Baada ya ajali hiyo, Dk. Mwakyembe na Msuya walipelekwa katika hospitali ya mkoa wa Iringa kwa matibabu.

Nyombi alisema Msuya alipata majeraha kichwani, ambapo alitibiwa na kuruhusiwa.

Akizungumzia hali ya Dk. Mwakyembe jana mchana kabla ya kuhamishiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Mganga Mkuu Mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Iringa, Dk. Oscar Gabon, alisema hali yake si mbaya kwani alikuwa akizungumza.

Dk. Gabon alisema Dk. Mwakyembe amepata michubuko usoni na ameumia taya la upande wa kushoto. (kuna mataya mangapi? M.M.)

Wakati huo huo, Hamis Shimye anaripoti kuwa, madaktari katika Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI), baada ya kumuhudumia Dk. Mwakyembe jana jioni, walishauri ahamishiwe hospitali ya Regency Mikocheni kwa matibabu zaidi, ushauri ambao ulitekelezwa.

Katibu wa Bunge Dk. Thomas Kashilillah, alithibitisha kuhamishwa kwa Dk. Mwakyembe.

Alisema Waziri Mkuu Mizengo Pinda, leo atakwenda kumjulia hali Dk. Mwakyembe na kwamba, alishindwa kufanya hivyo jana ili kutoa nafasi kwa madaktari kufanya kazi yao.

Akizungumza katika hospitali ya MOI, mke wa Dk. Mwakyembe, Lina, alisema hali ya mumewe jana jioni ilikuwa ikiendelea vizuri tofauti na ilivyokuwa muda mfupi baada ya ajali.

“Namshukuru Mungu, hali yake inaridhisha, anaongea ni jambo la kutia moyo,” alisema Lina.

Kwa upande wake, Dk. Francis Nyabusani wa hospitali ya mkoa wa Iringa, aliyefuatana na Dk. Mwakyembe kutoka Iringa, alisema hali yake ilikuwa mbaya alipompokea baada ya kupata ajali. (pamoja na hayo angesimama na kuonesha uongozi! according to somebody..)

Mbunge wa Viti Maalumu, Hilda Ngoye, alisema amepata mshtuko mkubwa baada ya kusikia habari za kutokea kwa ajli hiyo na kuwa, ni jambo la kumshukuru Mungu kuwa Dk. Mwakyembe ametoka akiwa hai.

Kwa upande wake, mfanyabiashara Reginald Mengi, alisema anaomba Mungu amsaidie Dk. Mwakyembe apone haraka ili aendelee na kazi za ujenzi wa taifa.

Wabunge wengine waliofika hospitalini hapo ni Wilson Masilingi, Victor Mwambalaswa, Lucas Selelii, Beatrice Shellukindo, Kilontsi Mporogomyi na Aloyce Kimaro.

Dk. Mwakyembe alihamishiwa Dar es Salaam kutoka Iringa alikopata ajali kwa ndege ya kampuni ya TanzanAir iliyokodiwa na Bunge, ambayo ilitua Dar es Salaam saa 9.50 alasiri.

Uwanjani hapo kulikuwa na viongozi mbalimbali wakiwemo wabunge ambao waliongozana na Dk. Mwakyembe aliyekuwa kwenye gari la wagonjwa la kampuni ya Ultimate Security hadi Muhimbili alikofika saa 10.20.

Msafara wa magari zaidi ya 30 yakiongozwa na lile la polisi wa TAZARA yalimsindikiza Dk. Mwakyembe kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere hadi hospitali ya Muhimbili, ambako pia kulikuwa na watu wengi waliokuwa wakimwangalia akiingizwa MOI.

Wakati huo huo, Estherina Kilasi (Mbarali– CCM) pia alipata ajali juzi, mkoani Morogoro na hali yake inaendelea vizuri.

Katibu wa Bunge Dk. Kashilillah alithibitisha mbunge huyo kupata ajali, lakini hakuweza kueleza kwa undani kuhusu tukio hilo.

Hata hivyo, habari zilisema baada ya mbunge huyo kupata ajali, vibaka walifika eneo la tukio na kumpora mbunge huyo vitu vyote.

Mbali na kupora, vibaka hao wanadaiwa kumpiga na kumjeruhi dereva wa mbunge huyo, ili kufanikisha uporaji. (hii nayo mbona hatukusikia, btw sikujua kuna mbunge anaitwa Kilasi! M.M)

Hii habari ya gazeti la uhuru (gazeti la CCM) mbona ipo tofauti sana na magazeti mengine? Jamani mambo mengine yanasababisha tuanze kutilia shaka ajali hiyo.

ona Tanzania Daima
Mwakyembe apata ajali mbaya Iringa
• Akimbizwa hospitali Iringa akiwa hajitambui

na Francis Godwin, Iringa


amka2.gif
MBUNGE wa Kyela, Dk. Harrison Mwakyembe, amenusurika kifo baada ya gari lake alilokuwa akisafiria kutoka Kyela kwenda Dar es Salaam kuacha njia na kupinduka katika eneo la Ihemi, karibu kilomita 40 kutoka Iringa Mjini.
Dk. Mwakyembe aliyekuwa akiendeshwa na dereva wake Joseph Msuya (30), katika gari lake aina ya Toyota Land Cruiser VX lenye namba za usajili T 362 ACH, alifikwa na mkasa huo jana majira ya saa 1:00 asubuhi.
Taarifa kutoka kwa watu walioshuhudia ajali hiyo, na wale waliofika eneo la tukio, zinatoa maelezo yanayotofautiana kuhusu chanzo cha ajali hiyo na namna ilivyotokea.
Kwa mujibu wa mashuhuda hao, ambao maelezo yao yamechukuliwa na polisi, ajali hiyo ilitokea muda mfupi baada tairi la mbele la gari hilo kutumbukia katika shimo lililo barabarani na kusababisha lichomoke, kabla ya kuacha njia na kuingia porini upande wa kushoto likiparamia miti na vichaka umbali wa mita 70 na kupinduka likilalia upande aliokuwa amekaa Mwakyembe.
Mmoja wa mashuhuda hao, Isaya Ng'ande, ambaye ni mkazi wa kijiji hicho, alisema alilishuhudia gari la Dk. Mwakyembe likiyumba wakati likijaribu kulipita lori na baadaye kupoteza mwelekeo kabla ya kuingia vichakani na kupinduka.
“Wakati ajali inatokea mbali ya lori hilo kuwa mbele, pia kulikuwa na basi la Marafiki ambalo wakati huo lilikuwa likipandisha mlima na ndani kulikuwa na askari wawili wa usalama barabarani.
“Baada ya kuona gari la mbunge limepoteza mwelekeo, basi hilo lilisimama ili kuepuka kugongana nalo uso kwa uso na kama si dereva wa basi hilo kusimama, ajali hiyo ingekuwa mbaya zaidi,” alisema Ng’ande.
Dereva wa Dk. Mwakyembe aomba msaada kwa Bastola
Kwa mujibu wa Ng’ande, askari na wasafiri wa basi la Marafiki, walitoa msaada wa kuwaokoa majeruhi, ndipo walipobaini kuwa aliyepata maumivu zaidi alikuwa Dk. Mwakyembe.
Alisema wakati wakiwa kwenye harakati za kutafuta usafiri wa kumkimbiza katika Hospitali ya Mkoa, lilitokea gari dogo lililokuwa likiendeshwa na mzungu, lakini alipoombwa kumbeba Dk. Mwakyembe, alikataa.
Hali hiyo, alisema ilimfanya dereva wa mbunge huyo aliyepata majaraha machache, kuchomoa bastola ili kumtisha na kumlazimisha mzungu huyo akubali kumbeba Dk. Mwakyembe, hadi katika Hospitali ya Mkoa wa Iringa.
Askari wa usalama walipoona hali hiyo, waliingilia kati na kumtaka dereva wa Dk. Mwakyembe kuacha kumlazimisha mzungu huyo kwa bastola na badala yake watafute usafiri mwingine ili kumwahisha mbunge huyo hospitalini.
Aliyemwokoa asimulia kilichotokea
Shuhuda aliyembeba mbunge huyo kutoka katika eneo la ajali na kumpeleka Hospitali ya Mkoa wa Iringa, kwa kutumia gari lake, Mboka Mwambusi, aliliambia Tanzania Daima kuwa, gari hilo lilihama barabarani kwa zaidi ya mita 70 na kwenda msituni.
Mwambusi ambaye alizungumza na Tanzania Daima akiwa eneo la tukio na baadaye jana akafika chumba cha habari cha gazeti hili alisema, alikuwa safarini kutoka Mbeya kwenda Dar es Salaam kwa kutumia gari lake aina ya Toyota Surf.
Shuhuda huyo ambaye ni Mkurugenzi wa Shule za St. Aggrey za mkoani Mbeya, alisema njiani walikutana na lori kubwa lenye tela la bluu na kichwa cheupe, likiwa kwenye mwendo kasi na baada ya dakika 15, walikutana na ajali hiyo ambapo gari la Dk. Mwakyembe lilikuwa nje ya barabara.
“Ilikuwa kama majira ya saa 12:45 asubuhi, hatukujua kama aliyekuwa majeruhi zaidi katika ajali hiyo alikuwa Mheshimiwa Mwakyembe. Tulishuka tu kwa lengo la kutaka kujua ni nani alikuwa amepata ajali hiyo na kama watahitaji msaada wetu, tukakuta ni Dk. Mwakyembe, lakini alikuwa na hali mbaya sana, amevimba uso, hatukujua kama alikuwa hai, kwani alikuwa hajitambui,” alisema.
Alisema waliwahi kumtoa kwenye gari hilo, lakini kukawa hakuna gari la kumchukua kumpeleka hospitali na muda huo gari nyingi zilikuwa katika mwendo kasi kutokana na giza la asubuhi na hakuna gari lililokuwa tayari kusimama.
“Alikuwa ameumia sana sehemu za kichwani na ilikuwa vigumu kujua kama yuko hai, wakati huo dereva wake naye akionekana kuumia, huku akionyesha wazi kuchanganyikiwa kutokana na ajali hiyo, hasa baada ya kumwona Dk. Mwakyembe akiwa na hali mbaya,” alisema.
Alisema dereva huyo huku akiwa katika hali ya kuchanganyikiwa, alianza kusimamisha magari akiomba msaada, kitendo kilichomlazimu kutumia bastola kutishia baadhi ya wenye magari ili watoe msaada wa kumbeba mbunge huyo.
“Nilimwambia yule dereva anaweza kusababisha maafa mengine. Gari langu lilikuwa limejaa mizigo mingi, tukalazimisha kulitumia. Nikapiga simu polisi, wakanisaidia kuwataarifu hospitalini.
“Tulipofika hospitali, tukakuta watu wa usalama, polisi, trafiki na madakatri wakiwa wameshajiandaa kabisa kwa ajili ya kutupokea na moja kwa moja wakamwingiza mgonjwa katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU),” alisema.
Alisema hadi wakati wakifika hospitalini, umbali wa kilomita 40 kutoka eneo la tukio, Mwakyembe alikuwa hajitambui.
Akizungumzia mazingira ya ajali hiyo, alisema ilikuwa vigumu kuelewa nini kilichosababisha dereva wa lori hilo kuingia upande wa pili wa barabara, kwani gari hilo lilikuwa likielekea Mbeya na liliigonga gari ya Dk. Mwakyembe ubavuni na kusababisha gari hilo kuanguka mara kadhaa upande alikokuwa amekaa Dk. Mwakyembe.
Polisi waokoa nyaraka za Richmond, Dowans
Katika eneo la tukio, mmoja wa askari wa usalama barabarani, ambaye alifika mapema, alimweleza mwandishi wa habari hizi kwa sharti la kutotaja jina lake kuwa, baadhi ya nyaraka alizokuwa nazo Dk. Mwakyembe, ni zile za Richmond, Dowans na baadhi ya taarifa za jimbo lake la uchaguzi.
Pia alisema katika gari hilo, kulikuwa na mchele, kuku pamoja na kompyuta ndogo (LapTop), ambavyo vyote vimeokolewa na polisi.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama Barabarani Mkoa wa Iringa, Salim Asas, alisema taarifa za ajali hiyo amezipokea kwa mshituko mkubwa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Advocate Nyombi, ambaye alifika eneo la tukio muda mfupi baada ya ajali hiyo, akiwa na maofisa wengine wa polisi, alisema amelazimika kufika eneo hilo ili kupata undani wa tukio hilo.
Hata hivyo, alisema uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa shimo lililopo eneo hilo ni moja ya sababu zilizochangia ajali hiyo kutokea.
Kamanda Nyombi alisema, Dk. Mwakyembe alitoka jimboni kwake Kyela, mkoani Mbeya juzi, majira ya saa 2:00 usiku kuja Iringa, na baada ya kufika Makambako, Wilaya ya Njombe, alilala na asubuhi alianza safari ya kwenda Dar es Salaam.
Alisema katika gari hilo, Dk. Mwakyembe alikuwa na dereva wake, ambaye amepata michubuko mwilini mwake, na kwamba nyaraka zake nyeti, ikiwamo kompyuta aina ya LapTop, zilizokuwamo kwenye gari hilo zimeokolewa.
Hata hivyo alisema hakuna mtu anayeshikiliwa na polisi kutokana na tukio hilo na kuwa Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi zaidi ili kujua sababu hasa za ajali hiyo.
Mganga Mfawidhi Iringa asimulia
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Iringa, Dk. Oscar Gabone, alisema hali ya mbunge huyo hadi jana, majira ya saa 6:00 mchana, ilikuwa ikiendelea vizuri tofauti na alipofikishwa hospitali hapo majira ya saa 2 asubuhi.
Alisema sehemu zenye maumivu zaidi ni kichwani na katika taya lake na upande wa kulia na hana jeraha kichwani, ila uchunguzi unaonyesha kuwa alijigonga kwenye kitu kidumu wakati ajali hiyo inatokea.
Dk. Gabone alisema kabla ya kulazwa kwa muda hospitalini hapo, alifanyiwa uchunguzi wa kina pamoja na kupigwa picha za X-ray ambazo hazijaonyesha kama kuna mfupa uliovunjika.
Kwa upande wa dereva wake, alisema alitibiwa na kuruhusiwa kuondoka baada ya hali yake kuwa nzuri.
Pamoja na kupatiwa matibabu katika hospitali hiyo ya Mkoa wa Iringa, bado alisema serikali imetuma usafiri wa ndege kwa ajili ya kumsafirisha mbunge huyo hadi Dar es Salaam ili akapate matibabu zaidi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHC), Kitengo cha Mifupa cha MOI.
Mwandishi wa habari hizi alipowasiliana na Meneja wa Tanroads Mkoa wa Iringa, Paul Lyakurwa kwa njia ya simu ili kutolea ufafanuzi juu ya mashimo hayo ambayo yamekuwa yakilalamikiwa na madereva mkoani hapa, alisema amefika eneo la tukio na kuliona shimo hilo.
Alisema, shimo hilo lenye ukubwa wa nchi mbili, hata kama gari lingekuwa katika mwendo mkali, lisingeweza kuleta madhara makubwa kama hayo.
"...Aaah si kweli kama shimo ni chanzo cha ajali ya Dk. Mwakyembe, mimi nafikiri chanzo hapa ni mwendo kasi, ila ninachotaka kusema suala hili la kuziba mashimo, tunaendelea kulifanya japo hata barabara yenyewe kwa sasa imechoka sana," alisema.

Taarifa hii imeandaliwa na Francis Godwin Iringa, Christopher Nyenyembe, Mbeya na Deogratias Temba, Dar.

sasa unaona tofauti ilivyokubwa, inadaiwa kuwa wakati wa ajali kulikuwa na basi ambalo lililazimika kusimama vinginevyo lingegongana uso kwa uso na gari la Dr. Mwakyembe. Na kwamba ndani ya hilo basi kulikuwa na askari wawili wa usalama bara barani.

Kwamba hakuna mali au nyaraka zilizoibiwa, dereva alibaki na pistol yake, nyaraka za Richmond na Dowans pamoja na laptop zilichukuliwa na trafic police.

Lori lililohusika na ajali halikusimama, licha ya kushuhudiwa na watu wengi (waliokuwa kwenye basi) pamoja na traffic police wawili. mwee hapa lazima ufanyike uchunguzi.
 
Mwakyembe apone haraka labda atafanya interview na KLH news au ataita press conference kueleza kilichojiri, mazingira ya ajali yalikuwaje, na kuprove au kudisapprove conspiracy theories wafuasi wake wateule.

Ashukuriwe baba wa mbinguni kwa kumnusuru kwenye hii ajali.

inategemea ni nani wametoa conspiracy theories.. hadi sasa sijatoa commentary yangu kama ilivyokuwa kwenye suala la Wangwe. Siharakishi kusema kwenye mambo haya.
 
Mh. ameongea na driver wake ameeleza vizuri tu.
Wamesema bada yakupita Ifunda, kulikua na semi trailer inatembea polepole wakaomba kupita, driver akawaruhusu lakini waliposogea mbele driver akasogea kwao, driver wa Mh alibidi aongeze mwendo kukwepa wakagongwa kidogo taa ya nyuma. Wakati ameongeza mwendo ndio akaingia lile shimo aka lose mwelekeo wakapinduka.Mbele kwambali kuna coaster ilikua inakuja.

Hizi habari kweli zinachanganya! Kwasababu hatujui kama gari lilipinduka baada ya kulivaa shimo na kupoteza nati,ama lilipinduka baada ya kugongwa kwenye taa ya nyuma. Na je lilipinduka mara baada ya yeye kujaribu kulikwepa shimo ama gari analo li overtake? Before this story,dereva alisema kulikuwa na gari linawafuata nyuma kwa kasi,na kwamba gari hilo liliwagonga kwa nyuma.
Aaah! Pole Mwakyembe na ni furaha kuwa umepona na kwamba utaendelea na shughuli za ujenzi wa Taifa letu....Ni sawa tu ukimwachia Mungu,na pia mjue kuwa ufisadi unaosababisha tuwe na miundo mbinu mibovu ndo karibia upelekee kupoteza kwako maisha....Adui wa maisha,uzima na afya ni FISADI.....Warudishe mali za watanzania ili tusibakie kwenye jalala la soga,umasikini,maradhi,njaa na maafa yanavyoweza kuzuilika,madhara kama ajali uliyoipata(Ajali endapo kweli ni ajali)
 

Mh. ameongea na driver wake ameeleza vizuri tu. Wamesema....

No no no, dereva tulishamsikia. "Mheshimiwa" amesema nini?

TBC wamesema dakika 30 zilizopita Mkuu ndo katoka hospitali. Sasa ulimsikia on bed side interview hospitali?
 
Nimepata fununu kuwa ajali ya Mh Mwakyembe ilikuwa imepagwa kwa makusudi ya kumuondoa. Tz ni nchi yenye fununu nyingi na mwanzoni nilipomsikia RPC wa Iringa akizungumzia ajali hiyo kwenye vyombo vya habari niliamini ni ajali ya kawaida.

Jana, dereva wa Mwakyembe alikaririwa akidai kuwa aligongwa kwa nyuma na lori na kusababisha ajali tofauti na RPC wa Iringa. Kauli ya dereva wa Mwakyembe niliipuuza na kuona labda kachanganyikiwa au alikuwa anaona 'mauza-uza' ambayo baadhi ya madereva hydai kukutana nayo kabla ya ajali na badala yake nikamwamini RPC wa Irainga.

Leo Dk Mwakyembe kazungumza. Nimemsikia akisema kuwa walikuwa wakijaribu kumpita dereva wa lile lori lakini wakati dereva wa lori lile hakuwa anataka apitwe na gari ya Mwakyembe! Na walipokuwa wakimpita aliongeza mwendo na kusababisha kugongwa na lori kwa nyuma na hivyo kusukumwa na kupinduka. MAelezo ya Dk Mwakyembe yanashabihiana na maelezo ya Dereva wake ambyo niliyachukia kama ni kujitetea tu kwa uzembe wake.

Maelezo haya ya Mwakyembe ndiyo yananipelekea nianze kuchukulia kwa uzito tetesi za uwezekan wa kupangwa kwa ajaili hiyo. HAdi sasa sijasikia kukamatwa kwa dereva wa lori lile wa lori lenyewe azidi ya kusikia kuwa Dereva wa Mwakyembe aliwekwa chini ya ulinzi wa polisi! Je, dereva wa lori na lori lenyewe yuko wapi?

Mwaka jana ajali ya namna hiyo ilimpoteza Mbnge Salome Mbatia Iringa na tuliambiwa kuwa dereva wa lori alikamatwa (sijui kesi ilienda na kuisha vipi). LAkini baada a ajali hiyo tukasikia kuwa mlengwa alikuwa Mh. Zitto abaye ndiye aliyewasaidia majeruhi wa ajali hiyo Zito mwenyewe akathibitisha hayo.

Ni vema tusiichulie ajali hiyo kirahisi rahisi ikizingatia kuwa mwaka jana ilisemekana Mwakyembe alilishwa sumu (ingawa haikuthibitishwa na yeyote) na wazee wa Kyela wakasema watapambana na yeyote anayetishia uhai wa Mbunge wao kupitia njia za giza. Pia tukumbuke kauli ya Mengi kuwa Mafisadi wanamtishia kifo (tukumbuke pia kuwa Mengi na Mwakyembe na Selelii walikuwa mikoa ya Ziwa kwenye ziara ambazo walizungumzia sana mapambano dhidi ya ufisadi).

Wana JF ni vema tuchukulie tetesi hizi kwa uzito unaostahili,
 
inategemea ni nani wametoa conspiracy theories.. hadi sasa sijatoa commentary yangu kama ilivyokuwa kwenye suala la Wangwe. Siharakishi kusema kwenye mambo haya.


Nakuaminia mkuu, wengine twasubiri tamko lako kwa hamu kubwa
 
- Wakuu Nsaji, Engineer na Lazaro vipi jamani tupeni uptodates au? Mana naona maneno mengi sana hapa, damn hebu tupeni dataz huko wakuu!

- Nsaji Mpoki vipi mkuu hakuna habari za uhakika huko? Binafsi nitaanza kuzitafuta rasmi dataz kuanzia kesho, otherwise tupeni dataz wakuu!.

FMEs!
 
Nimepata fununu kuwa ajali ya Mh Mwakyembe ilikuwa imepagwa kwa makusudi ya kumuondoa. Tz ni nchi yenye fununu nyingi na mwanzoni nilipomsikia RPC wa Iringa akizungumzia ajali hiyo kwenye vyombo vya habari niliamini ni ajali ya kawaida.

Jana, dereva wa Mwakyembe alikaririwa akidai kuwa aligongwa kwa nyuma na lori na kusababisha ajali tofauti na RPC wa Iringa. Kauli ya dereva wa Mwakyembe niliipuuza na kuona labda kachanganyikiwa au alikuwa anaona 'mauza-uza' ambayo baadhi ya madereva hydai kukutana nayo kabla ya ajali na badala yake nikamwamini RPC wa Irainga.

Leo Dk Mwakyembe kazungumza. Nimemsikia akisema kuwa walikuwa wakijaribu kumpita dereva wa lile lori lakini wakati dereva wa lori lile hakuwa anataka apitwe na gari ya Mwakyembe! Na walipokuwa wakimpita aliongeza mwendo na kusababisha kugongwa na lori kwa nyuma na hivyo kusukumwa na kupinduka. MAelezo ya Dk Mwakyembe yanashabihiana na maelezo ya Dereva wake ambyo niliyachukia kama ni kujitetea tu kwa uzembe wake.

Maelezo haya ya Mwakyembe ndiyo yananipelekea nianze kuchukulia kwa uzito tetesi za uwezekan wa kupangwa kwa ajaili hiyo. HAdi sasa sijasikia kukamatwa kwa dereva wa lori lile wa lori lenyewe azidi ya kusikia kuwa Dereva wa Mwakyembe aliwekwa chini ya ulinzi wa polisi! Je, dereva wa lori na lori lenyewe yuko wapi?

Mwaka jana ajali ya namna hiyo ilimpoteza Mbnge Salome Mbatia Iringa na tuliambiwa kuwa dereva wa lori alikamatwa (sijui kesi ilienda na kuisha vipi). LAkini baada a ajali hiyo tukasikia kuwa mlengwa alikuwa Mh. Zitto abaye ndiye aliyewasaidia majeruhi wa ajali hiyo Zito mwenyewe akathibitisha hayo.

Ni vema tusiichulie ajali hiyo kirahisi rahisi ikizingatia kuwa mwaka jana ilisemekana Mwakyembe alilishwa sumu (ingawa haikuthibitishwa na yeyote) na wazee wa Kyela wakasema watapambana na yeyote anayetishia uhai wa Mbunge wao kupitia njia za giza. Pia tukumbuke kauli ya Mengi kuwa Mafisadi wanamtishia kifo (tukumbuke pia kuwa Mengi na Mwakyembe na Selelii walikuwa mikoa ya Ziwa kwenye ziara ambazo walizungumzia sana mapambano dhidi ya ufisadi).

Wana JF ni vema tuchukulie tetesi hizi kwa uzito unaostahili,


Mkuu hilo liko wazi, kale ka sjimo hakaingiii akilini kuweza kuchomoa gurudumu la VX neva, neva..jamani! unless hilo gudumu lilisha legezwa kabla ya safari!

Pia nilishangazwa na salamu za pole za harka haraka kutoka TBC? haija niingia hata kidogo!

Lakini swali linalo baki pia lile lori liko wapi? na dereva wake? Kweli siasa mchezo mchafu!
 
Kinacho nishangaza mimi ni kuwa wakati ajali inatokea, kulikuwa na basi (Dr. Mwakyembe ameita coaster, nadhani hakuona vizuri) ndani ya hilo basi kulikuwa na askari wa usalama bara barani wawili (Two Traffic Police). Hao askari ndo waliookoa mali na nyaraka za Dkt. Mshangao wangu ni kwanini hawakufanya jitihada za kuzuia lori linalohusika na ajali hata kwa kuwapigia simu askari wenzao? Kama dereva wa lori hatapatikana, nitaunga mkono shaka hii.
 
lets rule out foul play....ni barabara mbovu...,na uendeshaji mbaya wa madereva wetu ....hasa wa magari makubwa wana mioyo kutu,alichofanyiwa mwakyembe na truck drivers wetu wanakifanya kila siku na magari mengi yanayoanguka along the highways main reason ni irresponsible careless driving ya malori au wrong parking......

mara zote mimi nikiendesha along the highway zetu na avoid sana kuyafuata mabasi ya mikoani au malori nyuma,au yaje nyuma yangu ..njia nzuri ni kuondoka mapema sana .Moja ya tabia zao maarufu ni kukuruhusu uwapite kwenye kona au hata sehemu ikiwa nzuri anakuruhusu pale anapoona mbele kuna gari lingine linakuja kwa kasi.......wenyewe wanaita kupambanisha ,wanawaacha mnagongana uso kwa uso ...wanabakia wanacheka ndani!!!

misingi mibovu ya uendeshaji wa biashara za usafiri Tazania na imani za kishirikina zinapelekea kuamini kuwa hawa madereva na matajiri zao ni devil worshippers na unaweza kufikiri wakisababisha ajali damu ikimwagika ....wanatoa zaka ya kuteketeza ....na kuhisi wanapata bahati zaidi....
 
Ni mapenzi ya Mungu, tumuachie Mungu.


Huyu Mungu huyu? kuna siku ndimi za moto zitashuka na kutushuhudia kwamba ka! hili simo!

Make walo kufa kwa mabomu, mapenzi ya Mungu.., wanao kolimbwa wote mapenzi ya Mungu.. jamani Mungu gani huyo mwenye kupenda mabaya yatokee juu ya viumbe wake alio tuumba kwa mapenzi yake na kwa mfano wake?
 
Back
Top Bottom