Ajali ya Dr. Mwakyembe na yatokanayo

Mr Mwakyembe explained that a lorry was overtaking his car and suddenly a minibus appeared on the opposite direction.
Ni kweli ushabiki inabidi usiwepo kwenye mjadala huu. Mkuu Ibrah amenukuu chanzo chake kwamba gari ya Mwakyembe ndio lilikuwa linalipita lorry. Mkuu Pundamilia naye ameleta nukuu (ingawa hajasema chanzo cha habari yake) kwamba ni lorry ndio lilikuwa linalipita gari ya Mwakyembe. Sasa tuamini lipi, gari ya Mwakyembe lilikuwa linaovertake lorry au lorry lilikuwa linaovertake gari ya Mwakyembe?
 
Huyo Engineer naona anaandika very negatively kuhusu Dr. Mwakyembe.
Most of our leaders wanatembea na bastola, so hiyo sio news.

Pia presumptions kibao.

Please don't try a spin.
 
Huyo Engineer naona anaandika very negatively kuhusu Dr. Mwakyembe.
Most of our leaders wanatembea na bastola, so hiyo sio news.

Pia presumptions kibao.

Please don't try a spin.

Urithiwetu,

Sawa mimi nime spin, naomba mwenye ukweli wa Kyela tuambie. Vinginevyo subiri 2010 na ndio tutajua ni nani alikuwa ana spin.

Watu mmekaa Dar na kusoma Tanzania daima na Nipasha na mnajifanya mnajua yote yanayoendelea vijijini, ukweli ni kwamba hamjui kitu na ndio maana mara nyingi mnashangazwa.

Mimi si niliwaambia akina LazarosMtindi na Nsesi wakanushe habari zilizotokea wiki mbili zilizopita na mbona hawakuja hapa kukanusha? Baadaye magazeti yakaja aandika kile kile ambacho nilishaandika.

Anayetaka kusoma spins zangu asome na asiyetaka aendelee na mambo yake au aandike anayojua yeye kuhusu Kyela. Ebo! mtu halazimishwi hapa.
 

Sawa sawa kabisa Mhandisi, wape wape vidonge vyao, wakiamua wameze au wateme, shauri yao. Some people don't wanna know and even hear the other side of the story, halafu wanajiita wanakoma nyani...

WEKA vitu mwana, kila jiwe litageuzwa pande zote usawa huu.
 
wewe unayejiita Engineer nataka kukueleza kuwa kutembea na bastola siyo makosa ndugu yangu labda unogeshe habari zako kwa vitu vingine, pili suala la mwakyembe kuwa na alikuwa na pessure siyo sababu za msingi kuzielezea, katika yote uliyoyaongea sijaona kitu ndugu yangu. samahani ndugu yangu hivi wewe ni Engineer? na kama siyo engineer unajisikiaje kutumia hiyo username?. Kwa mtazamo wangu naona haiendani na wewe, kwa sababu engineers wengi hawako kama wewe.
 
Hmmm!!! that is political assasination the Kenyan style...remember Bishop Muge? and many more...

na je ya opposition leader Tsvangirai na mke wake...the wife died in a dubious accident?

If you read the kenyan newspapers you will always see those weird accidents.

now they have graduated to armed robbers...aka a roberry gone bad!

May God protect us.
 
...suala la mwakyembe kuwa na alikuwa na pessure siyo sababu za msingi kuzielezea, katika yote uliyoyaongea sijaona kitu ndugu yangu. ...


Wewe Mwakakeli, tuletee DATAZ basi, hata za hapo Mwakaleli tu, eeh, vipi bwana, hata bwana Yesu ana mabaya na udhaifu wake, ije kuwa Mwakyembe?

Je anyosema Engineer kwamba Mwakyembe kasoma alama za nyakati na kuona kwamba upepo hauvumi ipasavyo jimboni kwake, ni kweli au si kweli. Kama ni kweli weka hoja za kusupport, kama si kweli eleza sababu ili kurefute hoja, sio kumparamia Engineer.

Hoja hujibiwa kwa hoja.
 

Mwakaleli,

Unachekesha kweli kweli, umetoa wapi ya kusema kutembea na bastola ni kosa au si kosa?

Kutembea au hata kuwa na silaha nyumbani kunaweza kukupa confidence ya kukabiliana na hatari tofauti na kama usingelikuwa na silaha. Matokea yake inakuwa hatari kwako mwenyewe kuwa na silaha, hicho ndio nilikuwa naongelea. Mfano ni Ditto, asingelikuwa na silaha yasingelimkuta yale yaliyomkuta. Jambo ni baya tu hata kama kuna watu wengi wanafanya, hili la viongozi kuwa na silaha ni ushamba wao tu, wanachotakiwa wao ni kuwa na ulinzi kama wanaona maisha yao yako hatarini. Kama una wasiwasi na maisha yako basi ajiri mlinzi.

Au huko kwenu Mwakaleli mnatembea na mapanga? Angalia sehemu zote ambazo watu wanatembea na silaha zinavyoongoza kwa watu kuuana.

Mimi ni fundi mchundo, huku kwetu wananiita engineer kwasababu nyie wasomi si mmejazana mjini na kukimbia vijijini tu na ndio maana hamjui ya huku vijijini? Kazi zenu kuja kubisha tu hapa huku ukweli hamuujui. Kama mna ukweli si andikeni basi wote tuchambue hapa?
 
Last edited:
Engineer tunashukuru kwa observations zako na tafsiri zake.........

Labda kwa akina Lowassa na akina RA ndio wataokuwa wanasifiwa kila siku kwenye vikao vyao.....kwani "pesa" wanazo to almost every individual kwa majimbo yao........

Kukubalika au kutokubalika kwa Mh Mbunge kunategemea na mambo mengi.......nategemea the fundamental one ni ahadi zake kwa wananchi........hizi influence mnazoleta ili kumuona/kumuonyesha Mh Mbunge always in a negative way haziwasaidii wana-Kyela

Kwenye suala la maendeleo ya Jimbo hakuna barabara iliyonyooka.....kuna sehemu Mh ataonekana weak na sehemu nyingine ni strong............sasa nyinyi mnaokuja hapa na ku-insinuate mawazo yenu ya chuki......haina maana kabisa............

Njoo hapa sema tatizo ni nini........toa mapendekezo yako........na sio.....ooohh sijui Mh alikuw ana Pressure....oohh sijui wapambe wake pia wanasema Mh ana-pressure.....oooh sijui kikao hakikuenda vizuri.........damn soo what!....inaonekana mambo yasipoenda vizuri kwa Mh wewe unafurahia in a way.......

Ndio maana Nmheshimu sana Mtanzania.....ana-state tatizo na anatoa suggestions ya jinsi la kulitatua....mfano alisema hapa kuwa Kyela kuna makundi.....na aka-suggest Mh a-play na holistic approach ili kufanikisha ajenda zake i.e maendeleo kwa wana Kyela........

....ukija hapa na kutuambia e.g. "Mh kazomewa kikaoni"....sijui utakuwa unamsaidia nani!!!

By the way thanks kwa maelezo yako ya safari ya Mh. toka Kyela kuelekea Dar in relation na masaa aliyosafiri.........kutokana na maelezo yako naweza kusema UCHOVU wa safari nao umechangia ile ajali..........mimi mwenyewe nikiwa naenda kutembelea mashemeji zangu huwa nalala Iringa for a good number of hours
 

its good theory ..but for a proffessional serial killer..no body was suppose to live to see the story...surveillance team ingekuwa ya kwanza kufika eneo la tukio kama wasamaria wema na kumaliza kazi ....na wangesubiri kidogo ili wananchi waje wasaidiane nao kuwaingiza kwenye gari wawapeleke hosipitali ....

siku hizi if you have enemies au vyovyote ukiona gari inakufuata nyuma au gari haikupishi ..achana nayo tena ikibidi park pembeni uangalie wanafanya hadi magari yawe mawili matatu ..then mnaongozana...pia ni muhimu kuchukua namba za gari kama hilo na ukiweza unalipiga picha kwa simu na kumtumia mtu wako yeyote wa karibu [juzt for funny]..kwa MMS...that may end up to be a very stong starting poinT ya investigations....haya titayaona sana kwani mwaka wa uchaguzi ndio huo......wanasiasa ....be aware!!!!!!
 
Mkuu Magezi,

Kwi kwi kwi!!!! nimeipenda hii habari yako hapo juu maana imenifanya nicheke.
 
Kama Mwakyembe amenukuliwa vema hapa naamini atakuwa anazungumza bila kujua anachokizungumza. Inawezekana, lakini mazingira ya lori, tena lenye tela, kulipita Toyota land Cruiser ni ya kusadikika zaidi. Tena, lori hilo liwena uwezo wa kuongeza mwendo na kufanikiwa kulifikia Land Cruiser (lililokuwa limenmgeza mwendo nalo) na kuligonga kwa nyuma, ni ngumu sana kuamini
 
Ndugu yangu engineer si kwamba sisi tuko mjini hatujui kinachoendelea ndugu yangu mimi ni engineer wa Civil na naishi Mbeya nafanya kazi MIST kwa hiyo habari za kuwa mjini hapo umeteleza na hivyo vijiji vya mkoa wa mbeya mimi huko huwa nazunguka kote, hiyo kyela nimepita kila kijiji kufanya shughuli za consultancy services. nimekuuliza kwa sababu nimeona kama ni mwanasiasa sana, sikuwa na lengo baya fundi mchundo. Msalimie huyo Dada engineer wa maji hapo Kyela huyo. Na kwa sasa sipo Tz ila mwezi ujao nitakwepo karibu tubadilishane mawazo ili tunapokosea turekebishane, ili kuendeleza taifa letu.
 
Kikubwa ni kusubiri uchunguzi ukamilike. We can speculate whatever we want, lakini ni muhimu kwenda deep na kufanya uchunguzi wa kina. Na kwa sifa anazopewa Dr. Mwakyembe za kupambana na ufisadi bila woga, naamini atatoka hadharani na kudai uchunguzi wa kina kuhusu ajali hiyo.

At the moment hii ni ajali kama ajali nyingine and nothing more. I guess we should discuss kipaumbele alichopewa Dr baada ya ajali compared to his drivers and watanzania wengine wanaokumbwa na ajali kama hizo.
 

Kinachotia mashaka ni kuwa hatujaambiwa kama dereva wa lori amekamatwa zaidi ya polisi kudai wanamshikilia dereva wa Dk. Mwakyembe! Hofu yangu ni kuwa polisi wetu ama hawafanyikazi professionally au wanajua wanachokifanya. Hata baada ya saa moja hadi mawili kupita uwezekano wa kulikamata lori hilo njiani ulikuwepo.

RPC Nyombi atupe taarifa kamili kama dereva wa lori naye yupo chini ya ulinzi kama wa Dk Mwakeyembe au la.
 
Mkuu Ogah,
Hiyo barabara ya Iringa Mbeya kidogo mimi iniweke chini. Kuna dereva ambaye siku zote namtumia, alikuwa na tender nzuri zaidi, akaona kuiachia kwa safari za wiki mbili haitakuwa vizuri. Nikamwelewa na akanitafutia dereva mwingine; njiani nikawa namwambia hii barabara mbaya punguza mwendo. Akawa anapunguza kisha anarudi pale pale, ilifika mahali nikachoka na kumwacha. Ghafla mwendesha baiskeli akaingia barabarani kutokea vichochoroni. Bwana wee! ilikuwa patashika, gari huku na kule mpaka tulipoenda kusimama kila mtu akamwangalia mwenzake kama dakika tano bila kusema kitu. Ilikuwa bahati tu vinginevyo ile gari ilitakiwa ipinduke, igongane na gari upande wa pili au imwue mwendesha baiskeli.

Sikumwambia kitu na baada ya kuona gari liko salama tukaendelea mbele; toka hapo hakukimbia tena. Mimi sitalaumu sana uembamba wa barabara maana kwa umaskini wetu kweli kuna haja ya kutumia mabilioni kwenye barabara moja wakati robo tatu ya barabara hazina lami? Nafikiri tatizo kubwa ni madereva wabovu, over speeding, ukosefu wa alama barabarani, sisi tunaoendeshwa ambao tunataka madereva waongeze mwendo na TANROAD ambaye wameshindwa ku maintain hizo barabara.

Watu wengi sana wamekufa na hizi barabara, jamani tujitahidi maana hao watu wana familia zao, si ajabu wanategemewa. Ifike mahali tuanze kuchukua hatua. Unakuta shimo kubwa barabarani, TANROAD wanakuwa wapi mpaka wiki zinapita bila kufanya matengenezo?

Alikufa jamaa yangu mmoja Dr. yaani ndio alikuwa ametoka Japan na kurudi na Ph.D yake. Akabanwa na lori kati ya Dar na Morogoro. Yaani kupoteza vijana kama hao ambao ndio kwanza walikuwa peak ya careers zao inasikitisha sana.

Sijui nini kifanyike lakini mimi nina wasiwasi kweli na hizo barabara zetu.
 
Mkuu Mwakaleli,

Nimependa hii ya consultancy services vijijini. Kama unaweza naomba niandikie zaidi kidogo hata kupitia PM yangu juu ya zina include vitu gani? Huenda kuna mambo ambayo unafanya ambayo na wengine tunaweza kujifunza/kufaidika au kusaidiana. Kuna mambo mengi sana huko vijijini yakifanywa inavyotakiwa, kuna weza kuwa na impact kubwa kwa wananchi wa kawaida.

Kazi njema.
 
Mtanzania, ndiyo matatizo ya nchi kuendeshwa bila SHERIA. Matatizo huanzia IKULU na matokeo yake huwa ni hadi huko barabarani. Hao madereva wangelikuwa wanapata adhabu kubwa, wasingelifanya hivyo. Mbona kosa la KUUWA linakuwa kwa nadra, kisa tu ni kwamba watu wanafahamu nini kinawasubiri.
 

Mtanzania huyu ni mkuu Mwakaleli,Mkuu Mwanjelwa kapotea kiaina.
 
Last edited:
Hilo gari kweli linaonyesha kama limegongwa kwa nyuma? Tena kama lori lilikuwa lina overtake basi taa ambayo ingegongwa ni ile ya upande wa kulia. Mbona gari linaonekana salama kabisa upande wa kulia?

Ni kweli inatakiwa polisi walitafute lori na magari yote ambayo yalishuhudia hiyo ajali kama sehemu ya uchunguzi.

Nakubaliana na MN; kweli lori lenye trela linaweza ku overtake shangingi ambalo liko kwenye speed?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…