Dereva wa Mbunge wa Kyela Dr Harrison Mwakyembe amedaiwa kuwa chanzo cha ajali iliyotaka kupoteza maisha ya mbunge huyo katika kijiji cha Ihemi, Iringa Vijijini baada ya gari lake lililokuwa likiendeshwa na Joseph Msuya (30) kuacha njia umbali wa mita sitini kutoka barabara kuu iendeayo Dar es Salaam, kugonga mti na kisha kupinduka.
Hayo yamo katika taarifa ya Kamati iliyoundwa na Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi (IGP), Said Mwema kuchunguza chanzo cha ajali hiyo .
Mkuu wa Kikosi cha Usalama wa Barabara nchini, James Kombe alisema baada ya uchunguzi wao kamati imebaini kwamba chanzo chake hakikuwa roli lililokuwa linapitwa kama alivyopata kunukuliwa mbunge huyo, bali dereva wa mbunge huyo aliyekuwa akiendesha gari hilo kwa mwendo mkali.
Kamati imefika eneo la tukio na kuwahoji mashuhuda walioona gari la mbunge huyo kabla na baada ya kupata ajali, kukagua gari la mbunge pamoja na kumhoji mtaalam wa magari aliyesomea uingereza, Francis Mwakatundu ambaye ameonyesha kupingana na kauli ya mbunge huyo kuwa aligongwa baada ya kuchunguza gari hilo na kuona hakuna sehemu ambayo ilionyesha kugongwa alisema.
Alisema uchunguzi wao haukuona alama yoyote ambayo inayothibitisha kwamba gari la mbunge huyo liligongwa kwa nyuma au upande mwingine wowote. Alisema mikwaruzo iliyopo ni ile iliyotokana na gari hilo kuacha njia na kubiringika porini zaidi ya mita 60 kabla ya kugonga jiwe kubwa na kulingoa na baadaye kuparamia mti mkubwa wenye mzunguko wa sentimeta 115 hadi kuungoa na hivyo kupinduka.
Kamati hiyo iliundwa baada ya kuwepo na taarifa tofauti toka jeshi la Polisi, Mbunge huyo na dereva wake.
Pamoja na maelezo hayo kamati ilishauri:
-Ikumbukwe kwamba mwendo ulioruhusiwa kisheria ni spidi 80 kwa saa na kwamba ajali zinapotokea waviache vyombo vinavyohusika vichunguze
- Barabara hiyo ni mbaya kwa kuwa ina mashimo mengi hivyo inastahili kufanyiwa matengenezo.
- Magari ya viongozi yasifungwe kispoti na wasitumie matairi yasio na mipira kwa kuwa usalama wake ni mdogo ukilinganisha na matairi yenye mipira.
-madereva wawe waangalifu na kuzingatia sheria zingine zote za usalama barabarani .
Kamati ya uchunguzi wa ajali hiyo ilihusisha Jeshi la Polisi, TANROADS, Wataalamu wa Ufundi wa Magari, na Daktari mmoja ambaye ni mtaalamu wa uchunguzi wa ajali.
Na Michuzi blog
-Ikumbukwe kwamba mwendo ulioruhusiwa kisheria ni spidi 80 kwa saa na kwamba ajali zinapotokea waviache vyombo vinavyohusika vichunguze
Hii kail jamani sijawahi kusikia.. naomba huyu mtaalam atueleze ukweli wa maneno haya..Nakumbuka sana mwaka 1988 nilisoma mahala wataalam wakielezea Usalam wa matairi yasiyokuwa na tube against yenye tube na ndio maana technologia ya leo inapitisha matairi yasiyokuwa na tube kwa sababu tube ikipata Pancha hupoteza upepo within few seconds na hivyo kusababisha gari kuacha njia kirahisi kuliko tairi lisilo kuwa na tube ambalo upepo huchukua muda zaidi kwisha.Magari ya viongozi yasifungwe kispoti na wasitumie matairi yasio na mipira kwa kuwa usalama wake ni mdogo ukilinganisha na matairi yenye mipira.
3-Lakini maswali yangu yanakwenda kwa Tanzania Daima.
Ilianzia kwa Jumapili iliyopita na baadaye gazeti la Jumanne hii kuandika taarifa kuhusu "utata" wa ajali hiyo. Awali walinukuu taarifa za dereva wa lori na trafiki mmoja alkiyekuwa katika basi dogo linalotajwa tajwa. Katika maelezo hayo ilionekana kama dereva amejitokeza na kuhojiwa. Taarifa zinasema polisi hawajafanikiwa kumpata dereva huyo wa lori (wamenukuu Tanzania Daima).
Mtanzania,
Mkuu wangu kwa jinsi nilivyoliona lile gari baada ya ajali na vitu wanavyosemna limevifagia kabla ya kusimama lisingekuwa hali hiyo kama kweli lilikuwa speed over 120Km/hr.. hii yote inatengenezwa tu..
Kumbuka ajali ya Wangwe, jamaa dereva katoka hana hana vimbi akapachikwa makosa kama tunayoyaona hapa.. kachukua mvua zake sijui miaka mwili mambo kama Kenya!..
Wangwe hatunae tena, Ukweli haujulikani na utabakia haujulikani kaa Sokoine, Mwaikambo na wengineo.
Kwanza sidhani kama kuna mahali Mwakyembe amesema kwamba kuna mtu aliyepanga ajali....
``...Mimi ni Mkisto, nimemuachia Mungu hayo, nimesema Mungu kama hiyo, kilichotokea leo, ni binadamu alikipanga basi namshitakia yeye, na kama kilichotokea ni ajali, basi tumuachie Mungu. Lakini kama kilichotekia kilipangawa basi huyo aliyepangwa kufanya hivyo ni mtaalam wa hali ya juu sana maana jinsi alivyoigonga ile gari, kupoteza mwelekeo, mimi kwa kweli nimeiona hiyo, hayo matukio, kwenye sinema tu.``
Mwakyembe ali entertain wazo kwamba kuna mtu, tena mtaalam wa hali ya juu, alitumwa kumuua.
Kama gari lililokuwa lina overtake lilikuwa linaenda zaidi ya 120 kwenye 80.. je gari lililokuwa lina overtekiwa lilikuwa linaenda mwendo gani?
Kuna speed limit bongo..?