Ajali ya Dr. Mwakyembe na yatokanayo

Ajali ya Dr. Mwakyembe na yatokanayo

Nyongeza ni kwamba kwa kawaida kama dereva wa lori alikuwa na nia mbaya angaweza kupunguza mwendo na kumlazimu dereva wa gari dogo kuomba kupita na baadaye wa lori kuongeza mwendo ama vinginevyo na mara nyingi hali hiyo husababisha ajali. Nimeshawahi kuingia porini kukwepa ajali. Madereva wa malori mara nyingi hufanya uhuni barabarani hata bila kutumwa maana mara nyingi wapo vichaa katika barabara zetu.
 
Hapo juu nimezungumzia trafiki aliyekuwa katika basi dogo na ambaye anaelezwa kushuhudia ajali!!! Na kwa bahati mbaya hakutajwa jina na gazeti husika, na sijui alipatikanaje akapeleka taarifa katika gazeti (nadhani ni habari za uchunguzi) na alikuwa akitokea na kwenda wapi!? je, aliposhuhudia alishiriki kupima ajali na alimpa taarifa gani RPC wake aliyetoa taarifa zilizobadilishwa na tume iliyofanya kazi kwa saa chache tu na kuhoji watu waliokuwapo siku ya ajali ambao waliwasubiri siku zote hizo watoke Dar waje wawahoji, yaani hawajaenda majumbani mwao wala hawajapandikizwa. Hii ni sanaa ya hali ya juu!!! BONGOWOOD
 
Nyie Matumbi vipi? Nimefikisha POST 1,000 wala hamnipi HONGERA? Hee, mnanionea wivu nini? Dilunga uko wapi? Mtanzania, kimya kabisa?? Looo, ngoja ninywe BIA maana wala sikujua kama nimefikisha, hadi ghafla naangalia, duuuuu!!!!!!
 
Dereva ndiyo chanzo cha ajali ya Dr Mwakyembe: Kamati ya IGP

Dereva wa Mbunge wa Kyela Dr Harrison Mwakyembe amedaiwa kuwa chanzo cha ajali iliyotaka kupoteza maisha ya mbunge huyo katika kijiji cha Ihemi, Iringa Vijijini baada ya gari lake lililokuwa likiendeshwa na Joseph Msuya (30) kuacha njia umbali wa mita sitini kutoka barabara kuu iendeayo Dar es Salaam, kugonga mti na kisha kupinduka.



Hayo yamo katika taarifa ya Kamati iliyoundwa na Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi (IGP), Said Mwema kuchunguza chanzo cha ajali hiyo .
Mkuu wa Kikosi cha Usalama wa Barabara nchini, James Kombe alisema baada ya uchunguzi wao kamati imebaini kwamba chanzo chake hakikuwa roli lililokuwa linapitwa kama alivyopata kunukuliwa mbunge huyo, bali dereva wa mbunge huyo aliyekuwa akiendesha gari hilo kwa mwendo mkali.




“Kamati imefika eneo la tukio na kuwahoji mashuhuda walioona gari la mbunge huyo kabla na baada ya kupata ajali, kukagua gari la mbunge pamoja na kumhoji mtaalam wa magari aliyesomea uingereza, Francis Mwakatundu ambaye ameonyesha kupingana na kauli ya mbunge huyo kuwa aligongwa baada ya kuchunguza gari hilo na kuona hakuna sehemu ambayo ilionyesha kugongwa” alisema.



Alisema uchunguzi wao haukuona alama yoyote ambayo inayothibitisha kwamba gari la mbunge huyo liligongwa kwa nyuma au upande mwingine wowote. Alisema mikwaruzo iliyopo ni ile iliyotokana na gari hilo kuacha njia na kubiringika porini zaidi ya mita 60 kabla ya kugonga jiwe kubwa na kuling’oa na baadaye kuparamia mti mkubwa wenye mzunguko wa sentimeta 115 hadi kuung’oa na hivyo kupinduka.



Kamati hiyo iliundwa baada ya kuwepo na taarifa tofauti toka jeshi la Polisi, Mbunge huyo na dereva wake.



Pamoja na maelezo hayo kamati ilishauri:
-Ikumbukwe kwamba mwendo ulioruhusiwa kisheria ni spidi 80 kwa saa na kwamba ajali zinapotokea waviache vyombo vinavyohusika vichunguze
- Barabara hiyo ni mbaya kwa kuwa ina mashimo mengi hivyo inastahili kufanyiwa matengenezo.
- Magari ya viongozi yasifungwe kispoti na wasitumie matairi yasio na mipira kwa kuwa usalama wake ni mdogo ukilinganisha na matairi yenye mipira.
-madereva wawe waangalifu na kuzingatia sheria zingine zote za usalama barabarani .
Kamati ya uchunguzi wa ajali hiyo ilihusisha Jeshi la Polisi, TANROADS, Wataalamu wa Ufundi wa Magari, na Daktari mmoja ambaye ni mtaalamu wa uchunguzi wa ajali.



Na Michuzi blog
 
-Ikumbukwe kwamba mwendo ulioruhusiwa kisheria ni spidi 80 kwa saa na kwamba ajali zinapotokea waviache vyombo vinavyohusika vichunguze

Na wale ndugu zangu wanaona kwenda 150km/h ni OK, mumeambiwa ukweli, mkisababisha ajali msije mkaanza kusaka wachawi.
 
Magari ya viongozi yasifungwe kispoti na wasitumie matairi yasio na mipira kwa kuwa usalama wake ni mdogo ukilinganisha na matairi yenye mipira.
Hii kail jamani sijawahi kusikia.. naomba huyu mtaalam atueleze ukweli wa maneno haya..Nakumbuka sana mwaka 1988 nilisoma mahala wataalam wakielezea Usalam wa matairi yasiyokuwa na tube against yenye tube na ndio maana technologia ya leo inapitisha matairi yasiyokuwa na tube kwa sababu tube ikipata Pancha hupoteza upepo within few seconds na hivyo kusababisha gari kuacha njia kirahisi kuliko tairi lisilo kuwa na tube ambalo upepo huchukua muda zaidi kwisha.
 
Mtanzania,
Mkuu wangu kwa jinsi nilivyoliona lile gari baada ya ajali na vitu wanavyosemna limevifagia kabla ya kusimama lisingekuwa hali hiyo kama kweli lilikuwa speed over 120Km/hr.. hii yote inatengenezwa tu..
Kumbuka ajali ya Wangwe, jamaa dereva katoka hana hana vimbi akapachikwa makosa kama tunayoyaona hapa.. kachukua mvua zake sijui miaka mwili mambo kama Kenya!..
Wangwe hatunae tena, Ukweli haujulikani na utabakia haujulikani kaa Sokoine, Mwaikambo na wengineo.
 
3-Lakini maswali yangu yanakwenda kwa Tanzania Daima.
Ilianzia kwa Jumapili iliyopita na baadaye gazeti la Jumanne hii kuandika taarifa kuhusu "utata" wa ajali hiyo. Awali walinukuu taarifa za dereva wa lori na trafiki mmoja alkiyekuwa katika basi dogo linalotajwa tajwa. Katika maelezo hayo ilionekana kama dereva amejitokeza na kuhojiwa. Taarifa zinasema polisi hawajafanikiwa kumpata dereva huyo wa lori (wamenukuu Tanzania Daima).

Halisi,

Ukiangalia kurasa za nyuma kuna sehemu niliandika kwamba inasemekana dereva wa lori amepatikana na kuhojiwa na polisi. Hizo taarifa mimi nilipewa na kijana mmoja ambaye ni polisi ngazi ya ofisa na ambaye alishiriki kwenye kuchunguza hiyo ajali. Mengi aliyosema ni copy right na taarifa iliyotoka leo.

Kwa kuangalia lile gari lilivyo pale mimi nili rule out mara moja kuhusu kugongwa nyuma. Kwa mtu yeyote anayejua physics ataliona hilo kirahisi mno. Kama lile gari lingegongwa kwenye taa ya kushoto, gari lingegeuka nyuma na ingekuwa ajali mbaya zaidi.

Lakini kwasasabu sisi Waafrika huwa hatuthamini sayansi na teknolojia zaidi ya uchawi basi tuna haki ya kuendelea kutafuta mchawi wa ajali hii.
 
Mtanzania,
Mkuu wangu kwa jinsi nilivyoliona lile gari baada ya ajali na vitu wanavyosemna limevifagia kabla ya kusimama lisingekuwa hali hiyo kama kweli lilikuwa speed over 120Km/hr.. hii yote inatengenezwa tu..
Kumbuka ajali ya Wangwe, jamaa dereva katoka hana hana vimbi akapachikwa makosa kama tunayoyaona hapa.. kachukua mvua zake sijui miaka mwili mambo kama Kenya!..
Wangwe hatunae tena, Ukweli haujulikani na utabakia haujulikani kaa Sokoine, Mwaikambo na wengineo.

Mimi kinachonishangaza hii kamati imechukua siku kama tatu tu kukamilisha uchunguzi wake. Wakati nyingine huchukua zaidi ya miezi sita, kuna nini hasa kinachotaka kufunikwa kabla hakijabackfire?, je kamati imemuhoji Mwakyembe?, imemuhoji Dereva, imemuhoji na dereva wa roli? au wametumia michoro ya barabarani kuja na conclusion ambazo nyingi ni politically motivated?
 
ajaliyamwakembe2.jpg


a. Ukisoma mapendekezo ya hiyo ripoti inalazimisha kuuliza swali; ni nini kilisababisha ajali? Maana kama nikifuatilia kile wanachosema kuwa ndicho kilichosababisha ajali pendekezo walilotakiwa kutoa ni moja tu.

b. Unajuaje mtu amesinzia kwenye gari? na ambaye ni abiria?

c. Pale palipotokea ajali ni karibu kwa kiasi gani na maeneo ya watu (mashuhuda); Je abiria waliokuwa kwenye gari nyingine walikuwa umbali gani kuweza kuona kilichotokea?

d. Huyo mtaalamu wa magari utaalamu wake kwenye magari ni nini hasa (maana hata mimi nina utaalamu wa magari!)

e. Tairi lilichomoka kwa sababu ipi hasa?

let me stop..
 

Kwanza sidhani kama kuna mahali Mwakyembe amesema kwamba kuna mtu aliyepanga ajali
....
Mwakyembe ali entertain wazo kwamba kuna mtu, tena mtaalam wa hali ya juu, alitumwa kumuua.

``...Mimi ni Mkisto, nimemuachia Mungu hayo, nimesema Mungu kama hiyo, kilichotokea leo, ni binadamu alikipanga basi namshitakia yeye, na kama kilichotokea ni ajali, basi tumuachie Mungu. Lakini kama kilichotekia kilipangawa basi huyo aliyepangwa kufanya hivyo ni mtaalam wa hali ya juu sana maana jinsi alivyoigonga ile gari, kupoteza mwelekeo, mimi kwa kweli nimeiona hiyo, hayo matukio, kwenye sinema tu.``
 
Mwakyembe ali entertain wazo kwamba kuna mtu, tena mtaalam wa hali ya juu, alitumwa kumuua.


ku entertain wazo ni haki ya mtu yeyote. Kudai kuwa kitu fulani ni factual pia ni haki. Hoja ya Halisi ni kuwa hakuna mahali popote ambapo Mwakyembe alisema (kudai factually) kuwa kuna mtu alipanga ajali hiyo.

Ndiyo maana katika nukuu yako umeacha the preceding conditional clause na kuweka maneno ambayo yanadai kana kwamba ni ukweli. Huku ni kujaribu kumfanya mtu aseme kitu ambacho hakukisema.

Mtu akisema "kuna mtu alipanga ajali ili kumuua Mwakyembe" na mwingine akasema "kama kuna mtu alipanga ajali ili kumuua Mwakyembe" katika mawazo yako unaweza kuona kuwa wamesema kitu kile kile. Vitu hivyo hata havikaribiani.

Wakati mwingine nukuu kauli nzima kama ulivyoona badala ya kuweka msisitizo kwenye kile ambacho unataka kusingizia kuwa amesema.

Je kuna mahali popote ambapo Mwakyembe amesema kuwa kuna mtu/watu waliopanga ajali hiyo na kuitekeleza?

Kusema "alientertain wazo" halijibu swali kwani wengi tuna entertain mawazo ya ajabu sana!! Ndiyo maana tunaitwa wanadamu.
 
Pamoja na kwamba sisi sote hatupo wala hajtujafika ktk eneno la ajali hiyo.. naomba kuuliza kitu kimoja.. katika picha moja hapo juu inayoonyesha lile shimo, kwa mbali kama mita 60 upande wa kushoto ni gari la Mh. Mwakyembe?..(rejea kwenye picha)
Kama ndivyo ningependa kuelewa mbona liko upande wa kuendeshe sio wa ku overtake!chuhuliaa kwamba walilipita hilo shimo kabla ya kufika kule waliko (direction ya kule walikuwa wakienda)..
 
Limit ya 80 KMS/H ni maalum kwa magari ya abiria tu. Walioshuhudia tukio walipaswa kutuambia michoro iliyoko barabarani at that particular point inasemaje? Ili tuweze kufanya a fair judgement. Kama ilikuwa inazuia kuovertake at that particular point ni wazi kosa la dereva. Then mambo ya hujuma hayapo kabisa. Ni vyema tukatambua kuwa driving is an art and profession. A driver is required to perform 5 actions in split second in order prevent accidents. They are SCAN,IDENTIFY,PREDICT.DECIDE and EXECUTE in order to minimise risk. Remember in a matter of a second or two when a drive is compelled to undergo the above 5 tasks he/she doesnt have an advisor nor assistant. Thus failure to perform any of the above tasks precisely amounts to loss of precious life and property which exceeds losses generated by other professions. For instance if a doctor or a lawyer errors a single life is in danger. But if a passenger bus error r 65 lives are endangered.Hence drivers should be accorded more respect and remunerations than they presently receive
 
Kama gari lililokuwa lina overtake lilikuwa linaenda zaidi ya 120 kwenye 80.. je gari lililokuwa lina overtekiwa lilikuwa linaenda mwendo gani?
 
wasiwasi wangu ni kwamba kama mwakyembe anamwamini dereva wake wasije wakahakikisha wanamfunga tu kwa makusudi ili wapate mwanya wa kufanya kweli kama hawajafanya
 
Jatropha,
Mkuu unaona barabara yanyewe haina line ya katikati hivyo huwezi kutumia sheria yoyote kwani vielelezo vya barabarani ndio sheria, hakuna mtu anayesimama na kuwambia wenye magari wasi overtake..
Hakuna alama hakuna sheria!
Derava dereva tu hakuna Professional ni kama mwendesha baiskeli unaweza kutojua kuandika bado ukaendesha gari bila ajali!..huwezi kumlinganisha na daktari hata kidogo..
 
Back
Top Bottom