- Katika dunia ya kibepari kama tuliyonayo Tanzania sasa hivi, haya maneno ni ya kawaida sana na ni vyema sisi wananchi tukaji-tune na kuyakubali ili tuondokane na zile attitude za kijamaa jamaa, za kutambea na kandambili huku ni millionea kwa sababu ya kuogopa kuonekana unaringa na jamii,
- Yale mambo ya darasa la saba Mwenyekiti wa tawi la CCM kiwandani, kushindana na PhD yaani Director wa kiwanda na kuishia kuwa taifa la kwanza duniani kuwa na viwanda vya Sigara na Bia visivyoleta faida kwa taifa, sasa yameisha kama wewe ni bingwa wa fani yoyote ile, ubepari inataka useme tena sana au wazi bila kuficha kwa sababu under siasa ya ubepari tuliyonayo sasa hivi, huwezi jua opportunity ita-strike wapi na wakati gani,
- Bila majivuno ubepari hauwezi kushamiri, hakutakuwepo na competition katika biashara, hakutakua na competition katika siasa, tutaishia kurudi kule kule tulikotoka, kama ni majivuno basi hata mashindano ya uzuri wa kinadada zetu ni dhambi na majivuno kwani wanaoshindwa maana yake ni nini kama sio ugly? Je wewe uliowatoa kwenye mashindano unaweza kuwaumba ndio hizo mentality za kudai ukweli ni majivuno, hazina nafasi tena katika taifa letu,
Mwakyembe either ni bingwa sheria au sio, lakini ndio anayo haki zote kujitangaza kwa public na dunia, ndio ubepari tunaoutaka unavyotaka ndio maana unaona watu kama Michuzi sasa wanapeta maana anachikifanya kule Michuzi blog ndio hasa maana ya ubepari, indivualism kwanza!
Ahsante Wakuu.
William.
Naona na hapa Tanzania tuanzishe Club ya kujisifu. Nchi nyingine kuna Club za aina hiyo. Utaratibu unakuwa kwanza unasimama mwenyewe unajisifu wee na baadaye wana member wengine wanasimama kumsifu aliye jisifu na humo humo wanajisifu mwenyewe. "Majisifu si upinde". Siungi mkono kuiga mambo ambayo hayana faida na taifa kwa kisingizio cha ubepari.