Ajali ya Dr. Mwakyembe na yatokanayo

Ajali ya Dr. Mwakyembe na yatokanayo

Nashawishika kuamini kuwa hii ajali ilipangwa na kulikuwa pia kumepangwa maelezo tayari baada ya Mheshimiwa Mwakyembe kufariki. Huenda walikuwa wamepanga kutoa taarifa kuwa huyu jamaa alikuwa amelala. Mheshimiwa baada ya ajali alizimia, na hawakuwasiliana na dereva wake, lakini wakatoa maelezo yanayofanana. Hawa mapolisi wanadai alikuwa amelala, kama angekuwa amelala wangewezaje kutoa maelezo yanayofanana? Ajali inatokea Iringa, maelezo yanatolewa na mtu wa Dar es Salaam na in fact mapolisi kutoka Daa ndio wanaenda kupima.
Nawaambieni, ninatabiri vita Tanzania. Watanzania wameanza kuelimika na kwa hivyo hawatakubali kuendelea kudhulumiwa kiasi hiki.
 
Ninamheshimu sana Dr Mwakyembe lakini kwa kauli zake za kutatanisha naanza kuwa na mashaka na uwezo wake kiuongozi he looks like mtu wa mitaani.Please sir acha kubishana bishana.Utajiongezea heshima kwa sisi tunaokuheshimu.

SaidSabke,
Mabingwa wa mikakati huwa wanashauri kuwa mtu yeyote ambaye watu wamemuweka juu iwe kwa kumtukuza au kumsifu, unapotaka kueleza upande wa pili wake ambao ni mbovu wanasema huo si wakati mzuri. kitendo chako cha kuonesha wasiwasi juu yake ni cha kweli kabisa. Kwa nyakati nyingi ambazo nimewahi kuongea au kumsikiliza huyu mh akiongea katika mazungumzo ya kawaida utajua kabisa is not for real, hupati kuona ni jinsi gani labda huyu jamaa ameenda shule na hata huko alikokuwa anafundisha kumekuwa na sarakasi gani. Anyway lakini ni swala la wakati uwezo wake halisi na jinsi alivyohaviwezi kujificha siku zote.
 
Mmh! panapofuka moshi kuna moto, wanajaribu kuuzima lakini ndo kama wanachochea! mh! hawaamini dumu lao la maji limebadilika mafuta, wanaanza kuhisi hujuma lakini ni vipi mwanamtandao na afanye usaliti ah! hapana wanaenda ktk hifadhi kutafiti labda walikosea wakachanganya dumu! ah! wapi dumu la mafuta lipo pale limejaa telee! wanashikwa na butwaa! hiki kitumbua! ama kweli mafuta yaishapo nguvu maji hufaa! walizoea kugeuza geuza eti sie 2we ngano
 
Mimi binafsi nilistushwa sana na taarifa ya ajali ya Mh Mwakyembe lakini baada ya maelezo kupatikana kutoka kwake na dereva wake na baadae Polisi nimepata ninashawishika kabisa kusema kuwa ni ajali ya kawaida ina kwa sehemu kubwa imesababishwa na uzembe wa dereva wa Mh Mbunge. Nikirejea maelezo ya awali kuwa lorry ndiyo lilikuwa linataka kuipita gari ya mheshimiwa na wakati huohuo mbele kwa upande mwingine kulikuwa kuna kuja basi la abiria, badala ya dereva wa mheshimiwa kupunguza mwenndo ili lorry litangulie, yeye akafanya maamuzi ambayo hayakuwa sahihi kwa kuongeza mwendo wa gari lake. Hali hiyo ilikuwa ni hatari kwa wale waliokuwa katika lorry na basi la abiria pia. Laiti kama asingeliongeza mwendo ni wazi angeweza kulimiki gari lake vizuri na kuondoa hofu aliyokuwa nayo kwa wakati ule.
Sasa nikirejea katika hayo maelezo ya Mh Mwakyembe, nadhani amekosea kabisa kufanya hivyo kwani nchi hii inaendeshwa kwa utawala wa sheria ambazo wao ndiyo watungaji. Hakupashwa kulalamika wakati huu ambapo tayari mamlaka husika zimesha sema kuwa tatizo alikuwa ni dereva wake na atafikishwa katika mahakama kujibu mashtaka. Haya ambayo Mwakyembe anayoyaongea alitakiwa akayatoe mahakama kama shahidi wa dereva wake na si vinginevyo. tafsiri inayojitokeza ni kuwa Mh anataka kupindisha shauri zima kwa ajili ya 'kumsaidia' dereva wake. Hayo ya kuanza kusema hii ajali inaweza kuwa na mkono wa mtu ni mawazo finyu sana kuongelewa na mtu kama mbunge kwenye hadhara.

Mkuu hata wewe pia...? Hivi inagharimu sh ngapi kusoma alichoongea Mwakyembe?
 
Mweshimiwa MP umeandika ujumbe ambao ni mzuri na itakua busara kama maswali yako waeshimiwa wa jeshi la polisi wakiyajibu.Mambo ya kuonewa kwa waliopata ajari yapo apa nchini ila kwa kua watu uelewa wao ni mdogo basi wanakaa kimya tu na kukubali matokeo.
Wewe ni msomi na unaijua sheria pamoja na haki yako ndo maana hautaki kuburuzwa.

Endelea kupambana yawezekana na wanyonge tukaponea kupitia kwako.
Asante
 
Ofisi ya mbunge wa jimbo la Kyela iko Kunduchi (Dar es salaam)? Nampa pole mhe Mwakyembe na namshukuru kujitokeza kuongea licha ya zengwe alilokwisha wekewa na kombe ati asiingilie ya kitaalamu! Lakini bado nashangaa, itaishia magazetini tu au kuna hatua zaidi? Huyu kaka Mwakyembe anazo taaluma zote mbili za sheria na uandishi (alisomaga TSJ ya zamani), kwa kuwa ameshachukua hatua ya gazetini naona ingefaa akachukua na ya kisheria pia, maana hapa mwenye uwezekano wa kuumizwa ni dereva, ndiye mnyonge katika hao walioathirika na ajali hiyo.
 
ni vipi post yangu haionekani! ktk mada hii@MODS, I POSTED IT TWICE inaanza hivi! mmh! panapofuka....
 
Kwanza nimpe pole Mheshimiwa Mwakiembe kwa ajali iliyomkupata. Kati ya vitu ambavyo viliniudhi kwenye taarifa ya Kombe ni kusema kuwa Mh. alikuwa amelala kwa sababu walikuta kiti chake kimeegeshwa nyuma. Hapa ndipo ninapojiuliza utaalamu anaouringia Kombe ni upi, kwa sababu zifuatazo:-

1)Kutokana na kasi ya lile gari ambayo kitaalam tunaiita velocity kuwa kubwa (120km/hr) ni dhahiri tayari Mh. alikuwa na kitu kinachoitwa Momentum kubwa ( Mass kg X Velocity). Momentum hii kwa umbali mfupi sana ili ilirudi kuwa sifuri, pale gari liliposimama baada ya kuanguka. Mh Mwakiembe huwa namuona tu kwenye picha na TV, lakini naamini ana uzito sio chini ya 90kg. Kusimama kwa ghafla kwa lile gari kungeweza kusababisha msukumu ambao ungeweza kukata lock zinazotumika kurekebisha kiti ili kilale, kiegemee mbele au kama atakavyo abiria. Sasa sijui kama akina Kombe walikagua kile kiti na kuona kuwa lock zake au hata frame hazijakatika au walikurupuka tu.
2) hata kama lock na frame zilikuwa sahihi, yawezekana kuwa kiti kile kiliegeshwa nyuma na wasamaria wema waliowahi eneo la tukio kutoa msaada.
Hilo wamemuuliza nani?
3) Kama anavyoshangaa Mh Mwakiembe, hivi nani alifuatilia wakati ule lile lori na kuona kama halikuwa na alama yoyote ya rangi toka kwenye gari la Mh? Nasema kwa wakati ule kwa sababu kufanya hivyo kwa sasa ni kupoteza muda kwasababu rangi zinauzwa madukani na kwamba kazi hiyo ya kuondoa rangi ile na kupaka nyingine itakuwa imekamilika.

Nafikiri kazi ya kitaalam anayozungumzia Kombe ni ile ya kukamata na kupeleka watuhumiwa mahakamani ili sheria ichukuwe mkondo wake lakini maswala yanayohitaji wataalamu awaachie wataalamu!

Kwa maelezo haya ya Kombe, ninawasi wasi kama anajuwa mahusiano ya mwendo kasi wa gari, kona , uzito wa gari na centre of gravity ya gari (M*V*R*H). Kuna siku watakuja kutueleza magari yanapinduka sana sehemu fulani yenye kona kali kwa sababu kuna mbuyu una mashetani yanayohitaji damu za binadamu!
 
Mwanafyale usijali Tulipamwinga( tupo pamoja ).Na ukipona kaza kamba mpaka Mafisadi wajue kuwa Si wa wananchi wa tanzania tu wanaokutakia mema bali dunia nzima na Mungu pia yu upande wako.Mungu akiwa upande wako ni nani atakeye kudhuru?
Mwanafyale kaza kamba Wanyalu wote wapo pamoja nawe
 
Press release ya Dk Mwakyembe ni nzito, imeandikwa kwa umakini na umahiri mkubwa ambao mwandishi anamiliki, na inafichua vingi kwa mwenye akili timamu.
Machache ninayoyaona:
1. Polisi nchini ni vibaraka, vi-dolly au marrionetes ambao hawana lao. Aidha hawana sifa za kazi zao, ama hawana akili timamu kutosha kutofautisha uongo, upumbavu na uchafu kutoka kwenye ukweli. Wanaamrishwa kufanya kile kinachotakiwa na wale wanaowamiliki. Hawatendi kazi zao kwa umma kama ipasavyo.
2. Kamati maalum pia huundwa wakati hazina umaalum wowote! Ikiwa ajali haikuuwa mtu, kwa nini iundwe kamati maalum na kisha inatangaza matokeo ya "uchunguzi" ambayo yanadhihirisha kuwa waliokuwemo kwenye kamati maalum ni "MAJUHA" au VIHIYO!" Tayari kuna kamati ndogo ya usalama (pia maalum) ameundiwa Mengi, hivyo tukae "CHONJO"
3. Kwa mara nyingine tena tunadhihirishiwa ni jinsi gani vyombo vya dola "VIMEOZA" na viko tayari hata kushiriki ktk jitihada za kuua raia, mpiganiaji haki za wananchi na wanyonge, wakati mishahara wanayolipwa ni jasho la hao hao wanyonge inayowanyima haki! Wakishirikiana na waandishi wasiokuwa na maadili ya kutenda kazi zao, bali kujali matumbo yao tu!

Dalili zitakazofuata:
a) Gazeti halitoacha kutetea uongo inaousambaza kwa kuwa limewekwa hapo kwa nia hiyo. Ila waandishi wa gazeti hilo lazima wajue kuwa wanaendelea kujivunjia heshima zao.
b) Meneja wa Tanroad Iringa itabidi akae chonjo kwani anawezaje kudiriki kukanusha maoni ya "wataalamu" wa kamati maalum?!?
c) Dereva wa lori husika itabidi aidha 1. apandishwe cheo na kuwa waziri wa usafirishaji au 2. apigwe marufuku kunywa pombe asije akatoa siri ya kazi nzima aliyopewa bila kujiua!

Mwisho: Wahusika ktk sakata hili wameongeza pengo jingine ktk harakati zao, na wakumbuke kuwa siku itafika na watajikuta wanajibu mashitaka ya mpango wao hapa hapa duniani, na wakifanikiwa kukwepa, basi mbele ya Mungu.
Mungu ibariki Tanzania.
 
Inachekewsha kuona Mtu Kama Kombe mwenye cheo cha juu kiasi hicho katika jeshi la Polisi anaweza kuwa mkiukaji mkuu wa haki za mwananchi hii nchi tusipokuwa makini tutaharibu misingi yetu mizuri aliyotuachia mwalimu,Haki na Kazi
 
'dereva ndiye chanzo cha ajali ya dk. mwakyembe'
http://1.bp.blogspot.com/_HO8ijU76ZcQ/ShwMxJJyV_I/AAAAAAAApcY/pQDzt0Rf2-k/s1600-h/Mwakyembe1.jpg
Dereva wa Mbunge wa Kyela Dr Harrison Mwakyembe amedaiwa kuwa chanzo cha ajali iliyotaka kupoteza maisha ya mbunge huyo katika kijiji cha Ihemi, Iringa Vijijini baada ya gari lake lililokuwa likiendeshwa na Joseph Msuya (30) kuacha njia umbali wa mita sitini kutoka barabara kuu iendeayo Dar es Salaam, kugonga mti na kisha kupinduka.

Hayo yamo katika taarifa ya Kamati iliyoundwa na Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi (IGP), Said Mwema kuchunguza chanzo cha ajali hiyo .
Mkuu wa Kikosi cha Usalama wa Barabara nchini, James Kombe alisema baada ya uchunguzi wao kamati imebaini kwamba chanzo chake hakikuwa roli lililokuwa linapitwa kama alivyopata kunukuliwa mbunge huyo, bali dereva wa mbunge huyo aliyekuwa akiendesha gari hilo kwa mwendo mkali.


“Kamati imefika eneo la tukio na kuwahoji mashuhuda walioona gari la mbunge huyo kabla na baada ya kupata ajali, kukagua gari la mbunge pamoja na kumhoji mtaalam wa magari aliyesomea uingereza, Francis Mwakatundu ambaye ameonyesha kupingana na kauli ya mbunge huyo kuwa aligongwa baada ya kuchunguza gari hilo na kuona hakuna sehemu ambayo ilionyesha kugongwa” alisema.


Alisema uchunguzi wao haukuona alama yoyote ambayo inayothibitisha kwamba gari la mbunge huyo liligongwa kwa nyuma au upande mwingine wowote. Alisema mikwaruzo iliyopo ni ile iliyotokana na gari hilo kuacha njia na kubiringika porini zaidi ya mita 60 kabla ya kugonga jiwe kubwa na kuling’oa na baadaye kuparamia mti mkubwa wenye mzunguko wa sentimeta 115 hadi kuung’oa na hivyo kupinduka.


Kamati hiyo iliundwa baada ya kuwepo na taarifa tofauti toka jeshi la Polisi, Mbunge huyo na dereva wake.


Pamoja na maelezo hayo kamati ilishauri:
-Ikumbukwe kwamba mwendo ulioruhusiwa kisheria ni spidi 80 kwa saa na kwamba ajali zinapotokea waviache vyombo vinavyohusika vichunguze
- Barabara hiyo ni mbaya kwa kuwa ina mashimo mengi hivyo inastahili kufanyiwa matengenezo.
- Magari ya viongozi yasifungwe kispoti na wasitumie matairi yasio na mipira kwa kuwa usalama wake ni mdogo ukilinganisha na matairi yenye mipira.
-madereva wawe waangalifu na kuzingatia sheria zingine zote za usalama barabarani .
Kamati ya uchunguzi wa ajali hiyo ilihusisha Jeshi la Polisi, TANROADS, Wataalamu wa Ufundi wa Magari, na Daktari mmoja ambaye ni mtaalamu wa uchunguzi wa ajali.

 
Mwanzoni niliweka post moja nikieleza juu ya kikosi maalum cha wauaji kwa njia ya ajali na nikasema zamani kikosi kilikuwa kina operate kutokea nje (nchi jirani jina linahifadhiwa) lakini sasa kinaimarishwa hapa hapa tz, kuna mwmbers wakanicheka lakini naomba mtambue kuwa kikosi hicho kipo na wamiliki wanakiimarisha hapa hapa ili kiwe effective, kaeni chonjo mengi yanafuata siku si nyingi.
 
Kuna VILAZA ambao they get away with terrible things they do......and yet wanapanda vyeo.......katika hilo kundi huwezi kumkosa huyu Polisi Kombe.........
 
Kuna VILAZA ambao they get away with terrible things they do......and yet wanapanda vyeo.......katika hilo kundi huwezi kumkosa huyu Polisi Kombe.........

Ogah,

Ndio maana nchi inaenda hovyo; kazi za maana zimeshikwa na wababaishaji wengi. Ukiwa mchapa kazi au kama unauliza maswali magumu magumu, huwezi kupanda vyeo.

Wana JF nendeni mkaokoe jahazi, wabaishaji wengi mno kwenye system. Tatizo ni chini mpaka juu.
 
Pole sana Mh Mwakyembe kwa ajali na kutopewa nafasi ya kusikilizwa. Huo ndio utaratibu wa kamati zinazoundwa na pia hata wewe kwenye kamati ulioongoza hukuwapa nafasi ya kuwasikiliza watuhumiwa. Nafikiri wakati mwingine hutarudia kosa hilo maana umeongea kwa uchungu sana. Siku zote mkuki kwa nguruwe kwa Mwanadamu .......
 
Mwakyembe ameonyesha ukomavu. Alisema tumwachie Mungu. Polisi wakamchokoza, kamwaga yote. Vile vile ipo siku hata ya Richmond atamwaga mboga
 
SaidSabke,
Mabingwa wa mikakati huwa wanashauri kuwa mtu yeyote ambaye watu wamemuweka juu iwe kwa kumtukuza au kumsifu, unapotaka kueleza upande wa pili wake ambao ni mbovu wanasema huo si wakati mzuri. kitendo chako cha kuonesha wasiwasi juu yake ni cha kweli kabisa. Kwa nyakati nyingi ambazo nimewahi kuongea au kumsikiliza huyu mh akiongea katika mazungumzo ya kawaida utajua kabisa is not for real, hupati kuona ni jinsi gani labda huyu jamaa ameenda shule na hata huko alikokuwa anafundisha kumekuwa na sarakasi gani. Anyway lakini ni swala la wakati uwezo wake halisi na jinsi alivyohaviwezi kujificha siku zote.

Hayo ni mawazo yenu na ujinga wenu na misimamo yenu lakini kaeni mkijua hamuwezi kujilinganisha na Dk. Mwankyembe hata kwa chembe! Tatizo mmenyweshwa maji ya mafisadi basi tena.
 
Back
Top Bottom