Press release ya Dk Mwakyembe ni nzito, imeandikwa kwa umakini na umahiri mkubwa ambao mwandishi anamiliki, na inafichua vingi kwa mwenye akili timamu.
Machache ninayoyaona:
1. Polisi nchini ni vibaraka, vi-dolly au marrionetes ambao hawana lao. Aidha hawana sifa za kazi zao, ama hawana akili timamu kutosha kutofautisha uongo, upumbavu na uchafu kutoka kwenye ukweli. Wanaamrishwa kufanya kile kinachotakiwa na wale wanaowamiliki. Hawatendi kazi zao kwa umma kama ipasavyo.
2. Kamati maalum pia huundwa wakati hazina umaalum wowote! Ikiwa ajali haikuuwa mtu, kwa nini iundwe kamati maalum na kisha inatangaza matokeo ya "uchunguzi" ambayo yanadhihirisha kuwa waliokuwemo kwenye kamati maalum ni "MAJUHA" au VIHIYO!" Tayari kuna kamati ndogo ya usalama (pia maalum) ameundiwa Mengi, hivyo tukae "CHONJO"
3. Kwa mara nyingine tena tunadhihirishiwa ni jinsi gani vyombo vya dola "VIMEOZA" na viko tayari hata kushiriki ktk jitihada za kuua raia, mpiganiaji haki za wananchi na wanyonge, wakati mishahara wanayolipwa ni jasho la hao hao wanyonge inayowanyima haki! Wakishirikiana na waandishi wasiokuwa na maadili ya kutenda kazi zao, bali kujali matumbo yao tu!
Dalili zitakazofuata:
a) Gazeti halitoacha kutetea uongo inaousambaza kwa kuwa limewekwa hapo kwa nia hiyo. Ila waandishi wa gazeti hilo lazima wajue kuwa wanaendelea kujivunjia heshima zao.
b) Meneja wa Tanroad Iringa itabidi akae chonjo kwani anawezaje kudiriki kukanusha maoni ya "wataalamu" wa kamati maalum?!?
c) Dereva wa lori husika itabidi aidha 1. apandishwe cheo na kuwa waziri wa usafirishaji au 2. apigwe marufuku kunywa pombe asije akatoa siri ya kazi nzima aliyopewa bila kujiua!
Mwisho: Wahusika ktk sakata hili wameongeza pengo jingine ktk harakati zao, na wakumbuke kuwa siku itafika na watajikuta wanajibu mashitaka ya mpango wao hapa hapa duniani, na wakifanikiwa kukwepa, basi mbele ya Mungu.
Mungu ibariki Tanzania.