Ajali ya Dr. Mwakyembe na yatokanayo


Mkuu Mtanzania,
Hoja zako nyingi zinakataa kukutana, zinapwayapwaya bila msingi mahsusi, lakini leo nimekuelewa. Una uchungu sana wa maendeleo ya Kyela na unadhani utamwondoa Dk. Mwakyembe, ambaye unamzungumzia kila mara kwa mizungukozunguko na kejeli za "kwi kwi kwi", kwa kutumia JF? Umepotea njia bro. If you are serious, nenda Kyela - wherever you are. Kwi kwi kwi kwenye JF na kwa kutumia wapambe njaa, utaishia kwi kwo kwu!
Regards.
 

Mkuu, huu ni usanii mtupu! Watamtafutaje wakati Mwandishi wa Tanzania Daima alishamhoji na yupo Iringa?
 
Hi wakuu,

Kuna issue nyingine Polisi wetu wanachekesha, mbona mashuhuda huwa wanahojiwa pindi ajali zikitokea hawajawahi kusema kuwa hawana utaalamu, ila kwa Mwakyembe tu. Kuna namna hapo, siyo bure.
 
Mkuu Mkandara,

Hayo ndio matatizo ya TZ kwenye ngazi zote za utwala. Wengi wao wanashindwa ku deliver kwa visingizio mbalimbali.

Matatizo sio Kyela pekee, ni wilaya zilizo nyingi kama ulivyosema.

Labda dawa ni watu wenye mawazo tofauti kujaribu kuingia na kuibadili system kila mtu kwa uwezo wake. mwakani kuna uchaguzi ni muda mzuri kwa wale ambao wako tayari kwenda kuwavisha kengere paka hawa wanaotumaliza. Najua sio rahisi na mtapigwa vijembe vyote lakini kama una amini katika mabadiliko ya kweli ni bora ujaribu.

Kinachosikitisha tu ni wengi wanaamini lakini wakifika kwenye system ndio wa kwanza kuwa wanafiki. Wanaanza kufanya yale yale ambayo huko nyuma walikuwa wanayapinga.

Mkuu ukiamua kwenda kule Mara tutakuunga mkono bila kujali uko chama gani. Tumepiga sana kelele hapa lakini inaelekea hazizai matunda kabisa, lets stand up and be ready to be counted.
 

Mhh. Mgeni huyu~~~~~!!!!! Kapela Msonda,

Join Date: Fri May 2009
Posts: 3
Thanks: 1
Thanked 0 Times in 0 Posts
Rep Power: 0

Credits: 4,590
 
Mhh. Mgeni huyu~~~~~!!!!! Kapela Msonda,

Join Date: Fri May 2009
Posts: 3
Thanks: 1
Thanked 0 Times in 0 Posts
Rep Power: 0

Credits: 4,590

Mkuu Sikonge,

Achana na wabadilisha majina kila siku. Kama mtu una hoja na unaongea ukweli kwanini kila siku kuja na majina mapya?

Yeye tayari yuko kichwani mwangu, eti anajua nataka kufanya? Tayari yuko vichwani mwa wana Kyela, eti anajua watachaguaje? Naona aishauri NEC isifanye uchaguzi Kyela.

Tumewazoea hawa ni kama vyura ambao hawamzuii ng'ombe kunywa maji pamoja na kelele zao zote.
 
Mtanzania,
Mkuu shukran sana, ningependa sana kuingia siasa lakini mkuu wangu mimi Mkerewe na mwoga sana wa tungule, wala sisemi uongo..kwa sababu najua zipo na zinafanya kazi muhimu nizikalie mbali wala nisikurubie..

Ubunge ni sawa na Utume ambao huwakilishi bwana mmoja ila unawakilisha watu wengi na wenye matakwa tofauti..naweza sema hata mitume wetu walikuwa na kazi kubwa lakini yenye unafuu kidogo kuwakilisha ujumbe wa Mungu mmoja kwa watu wengi kuliko kazi ya kuwakilisha watu wengi maskini kwa bwana mmoja (serikali)..Mara zote watu kama hawa huwabidi kujipachika Ubwana na heshima ni wajibu wa wananchi kuwapa, tofauti na Mitume ambao hupewa utume na ubwana wakaheshimika kwa matendo yao maokovu...

Dunia ya leo ni vugumu kupata viongozi wazuri, tazama Biblia na Msahafu utakuta mitume wote wameaminiwa na kusifika kwa kazi walizozifanya, mazuri waliyoyafanya, wokovu na zaidi ya yote unyenyekevu wao kuogopa sheria zinazowafunga ktk imani hiyo. Lakini siii wabunge, mawaziri wala marais wetu..Wao ndio Miungu, Watawala na husifika tu wakiwa jeuri, wakali, wenye kufikiria wao kile kinachowafaa wananchi..kwa sababu ndogo sana - Wao ni Watawala sii tena wawakilishi wa wananchi..

Mkuu huyo Kapela wala asikusumbue mpe mke tu, mtu muhimu wa kulumbana naye ni Shalom ambaye anatupa hoja zinazojibu hoja...na hakika ningependa sana kuona malumbano ambayo yanachukua hatua nyingine ya kuhoji hawa wabunge wetu.. Wilaya kwa wilaya tupate wale wanao support na wale wanaopinga uongozi ktk kuwafahamu hawa wawakilishi wa hizi wilaya zetu maanake kesho utasikia mbunge fulani kawa waziri unashindwa kujua katokea wapi..
 

Mimi ni mmoja wa watu ambao kwa kipindi kirefu sana nimekuwa fan wa kusoma comments kwenye forum hii, hivyo nawaelewa wengi na naelewa hata mwelekeo wa mawazo ya baadhi. Wewe in particular umenigusa kwa vile una mwelekeo unaomgusa mtu, sitaki kuficha, ninaye mu-admire. Kuna kosa hapo? Kuna tatizo kuanza kuchangia kwa kukushauri kuhusu ndoto yako mpaka niitwe chura? Unapata tabu gani unaposhauriwa? Badala ya kuniambia niishauri NEC isifanye uchaguzi Kyela, wewe anza kujizoeza kubugia vidonge vya BP! Sisi macho na tupo!
 
Mkuu Mkandara,

Sasa hayo sio ndio mabadiliko ambayo tunayapigania? Kama utaweza kuonyesha kwa vitendo kwamba huna jeuri juu ya wananchi wako; kama utaonyesha kwa vitendo kwamba wewe si mtawala bali ni kiongozi ambaye uko tayari kujifunza; uko tayari kukosolewa na kutukanwa. Kama utaonyesha kwa vitendo kwamba unaweza kuunganisha watu badala ya kuwagawa, hapo utakuwa umefanya jambo la maana. Huwezi kutatua matatizo yote, hata wenzetu huku walio endelea hawajamaliza matatizo yao yote. Ila tu tatizo la leo likiendelea kuwepo kesho na kesho kutwa ni dalili ya uongozi ulioshindwa kufanya kazi.

Tatizo kubwa la Tanzania ni jamii iliyojenga masifa tu; ukimwambia mfalme uko uchi wakati kweli yuko uchi inaonekana wewe humtakii mema; wenyewe wapambe wanakuja na lugha tofauti hata pale ambapo mioyoni mwao wanajua si kweli. Unatakiwa usimguse wanayemwamini vinginevyo wewe ni adui. Akili za namna hiyo ndio zimetufikisha hapa tulipo. Matokeo yake viongozi wamepata kiburi na kuamini wanaweza kufanya lolote kwasababu wana madaraka; wana mapesa; hawawezi kubabaishwa na watu wasio na uwezo kama wao.

Hayo ndio mambo tunayaona hata hapa JF ambapo watu hawaamini principles zozote na badala yake wanaamini watu. Matokeo yake ni kuwa dissapointed inapoonekana hao miungu watu wao ni binadamu tu kama wengine pamoja na weaknesses zao kibao.

Ila mimi siamini huo uchawi na kule kwetu wanasema wanaenda Malawi kuutafuta lakini ukiwachunguza hakuna lolote zaidi ya kutishia watu tu. Kuna vijana mimi kule kwetu walikuwa wanabishana kwamba mtu fulani ni mchawi eti anafuga funza. Mimi nikawaambia kama kuna mtu ataenda kwa huyo mchawi ili atume hao funza kwangu na kama watanikamata basi huyo kijana atapata elfu kumi na pia huyo mchawi elfu kumi. Hao vijana wakasema kumbe kaka umejikinga sana. Ukweli ni kwamba huo uchawi hakuna na ni porojo tu kama za Yahaya Hussein. Sasa unataka nisikutembelee kule kanda ya ziwa kwasababu nitalimishwa usiku? Ukiamini hivyo kweli kila siku utaamka umechoka na kuendelea kuamini zaidi na zaidi kwamba unalimishwa.

Kikubwa naamini kila mtu atakufa na siku yangu ikifika basi nitaondoka kama walivyoondoka mababu na mababu. Cha kuogopa ni kuondoka ukiacha nyuma lundo la watu uliowadhulumu, uliowanyanyasa na ulio watesa. Vinginevyo kifo ni njia itakayomkuta kila mtu. Muhimu tu ni kuhakikisha hukitafuti kifo kwa reckless acts kama ngono, madawa ya kulevya, uendeshaji mbaya na mambo mengine. Ni bora kifo kikifuate kwa magonjwa ya mungu au mambo ambayo huna control nayo.
 
Mtanzania,
Mkuu shukran, nazidi kusema mimi utume siuwezi na hatukuumbwa wote kuwa viongozi wa kuwakilisha watu..Mimi ni ktk kundi la kuongozwa - Kondoo..
Nachoweza kuongoza au kuwakilisha ni uchumi, iwe shirika au kikampuni uchwara kwa sababu naamini kabisa kuwa inao uwezo na kipaji cha ubunifu ktk maswala la kuzalisha FEDHA kihalali ktk kuondokana na umaskini wa mali...
Kama una nafasi ya kazi mkuu ktk sehemu hizo nishtue, unajua tena huku kichuguu kimeota majani!..Usoshalist unachukua hatamu.
 
Mkuu, naona kuna sehemu member mmoja humu anasema yeye na Kombe (James) wamefundishwa certificate ya sheria na Dr Mwakyembe pale mlimani...inawezekana msingi wa hilo suala hapo juu ni huo?

Respect mkuu.

- Mkuu wangu mimi ninasema hivi inapokuja sheria hasa ya bongo, kama tuna wasomi watano tu wa juu basi Mwakyembe ni mmojawapo, hakupewa ubunge na CCM kwenda EAC bila sababu ni kwa sababu walimuhitaji sana kule kwenye maamuzi muhimu ya kisheria kuhusu kuanzishwa kwa EAC,

- Sasa wananchi tusichanganye ishus, kama Mwakyembe ana makosa kiuongozi huko Kyela, yasemwe hapa kwa facts na dataz tuyachambue na mazuri yake pia yasemwe, otherwise tupunguze blah! blah! na ndugu wa siasa za Kyela endeleeni kutupa elimu ya bure hapa kuna tunaofuatilia sana tena kila siku.

Respect.


FMEs!
 
Mkuu Mkandara

MOD amefuta post na hilo limenisikitisha sana kwani inakuwa vigumu kujua nianziye wapi kwa sasa au kwa lugha nyingine amekubaliana na Mtanzania kuwa Mwakyembe ni kati ya wabunge wasiotenda kazi na wanaostahili kutopewa muda mwingine.

Mimi sikubaliana na hilo na ninasema kuwa mwakyembe ni kati ya wabunge walofanya vizuri (in fact kwa kyela hakuna mbunge yoyote ambaye ameweza kufanya aliyoyafanya DK kwa muda mfupi tangia uhuru).

Ndiyo ana mapungufu yake hata mimi huwa sikubaliani naye kwenye mambo mengine kwa mfano la kuona upinzani (uchadema) kama ni upuuzi hilo huwa napingana naye kabisa.

Sasa unapoona kuwa kuna mtu anamchukia tu bila sababu yoyote ya msingi, zipo za kusingizia nasisitiza za msingi inabidi tunaoipenda kyela tutoke na kutetea. Na kama mtu atakuja na kusibitisha kuwa kyela ya sasa sio bora kama ilivyokuwa miaka 4 iliyopita basi tutamuunga mkono.

Wengine hatuko hapa kusema vitu ambavyo vitawafurahisha watu bali tutasema vile tunavyoamini sasa kama kuna watu watachukia au kufurahi hiyo ni juu yao.

Nimemwomba MOd anitumie zile post alizofuta ili niweze kuendela na mjadala kwani imenibidi nitafute more data na hapa hapatakalika jamani. Hizi siasa zetu ni za ajabu sana hebu fikiria kuna jamaa mmoja ambaye alikuwa rafiki sana wa DK na alimsaidia kwenye kampeni lakini sasa anaongoza kumpiga majungu ukimwuliza sababu anasema eti jamaa baada ya kupata ubunge yupo karibu na shemeji zake kuliko rafiki zake sasa huo ni upuuzi kabisa. Yaani sisi tusipate mendeleo kwa upuuzi huu jamani!
 

Mkuu, well-said! Ndo maana I can see sense in what Kapela Msonda has said, awe mgeni asiwe mgeni. JF siyo campaign forum ya kuchafua watu bila msingi, ni forum ya kurutubisha mawazo. Mtanzania asitumalizie space tu humu kuhusu ndoto zake za Kyela ambazo hazitafanikiwa mbele ya kile "kisiki cha mpingo". Simple advice: aende kuungana na yule RC wao ambaye toka aapishwe hajui kazi nyingine bali kumbugiza mangumi Mwakyembe to JK's total satisfaction.
 

Mkuu Sikonge,
Huyu Kapela Msondo,Ndiye yuleyule chizi wa siku zote.Mara anajiita Lazaro, mara Ntindi,mara Kapela.

Yote ni ukosefu wa akili na na kuwa na mwelekeo wa ujinga.
Halafu huyohuyo kwao wanamwita ni msomi. So stupid.
 
Mkuu Shalom,

Kwa mara nyingine data zako si sahihi; huyo unayemsema analalamika kama wanavyolalamika wengine hapa. Sababu ya kukosana sio hiyo unayoisema. Kwa mara nyingine unathibitisha huelewi kabisa yanayotokea Kyela.

Tatizo kubwa ni kwamba Mwanjala alikuwa tayari kumaliza ugomvi na Mwakipesile kitu ambacho mbunge hakupenda. Mwanjala ni mfanyabiashara na anajali maslahi yake. Mwakipesile alipochaguliwa kuwa RC alienda kumwona na kumpongeza na huo ndio mwanzo wa ugomvi wao.

Kwanza akaanza kwa kumfukuza pale alipokuwa ana park malori yake, akaanza kumwambia jamaa mwendesha malori tu na hana elimu na dharau zingine kibao. Kibaya zaidi akaenda mpaka kwa wazazi wa huyo jamaa kuwaambia mwanao anataka kumwua.

Badala ya rafiki akatengeneza adui. Hata wengine tulikuwa marafiki hivyo hivyo hiyo 2005 lakini baada ya hapo tumeshuhudia vituko tu na njama za kukwamishana bila sababu zozote. Uzuri wengine hatutegemei fadhila za mtu, tunategemea kuhangaika na kuchapa kazi. Mtu anaweza kukucheleweshea mambo yako lakini hawezi kuyakwamisha.

Jiulize waliomwunga mkono Mwakyembe 2005 wako wapi? kwanini anakosana na kila mtu anayekaribiana naye?

Hayo ya kwamba jamaa analalamika kwasababu ya mashemeji ni kwenda chini kwa mtu kama wewe kuamini hivyo. Tafuta simu ya Mwanjala na ongea naye na upate upande wa pili wa shilingi, hata mimi naweza kukupatia ukiitaka.

Mwakyembe wa Richmond na mwakyembe tunayemjua wengine kule Kyela ni watu tofauti kabisa. Yeye anahama tu ugomvi kutoka mtu mmoja kwenda mwingine. Mwanzoni alifikiri Mwakipesile anataka kugombea tena; akamwandama kwa maneno, kupanga vijana wa kuzomea na kuandika magazetini. Alipogundua Mwakipesile hagombei nguvu ikahamia kwa Mwanjala, sms za matusi, kejeli za mitaani na kumhusisha na Lowassa. Sasa wamehamia kwa mtu mwingine.

At last hata wana Kyela walio wengi wameshagundua tatizo liko wapi na watatoa hukumu yao 2010.

Pia tunapoongelea performance ya mtu ni muhimu kutumia SMART (specific, measurable, achievable, relevant and time-based) tool. Ukisema amefanikiwa kuliko mbunge yeyote toka uhuru ni too vague na huwatendei haki wasomaji au wanaojadili. Njoo na data kama ulivyosema kakuta shule 2 na sasa ziko 14. Hapo ndipo panakuwa na mjadala na ndipo nyani anaweza kukomwa giladi. Hizi vague statements mtu yeyote anaweza kuzitoa bila hata kuwa na data za kuhalalisha statements kama hizo.

Ukiona mtu anaanza kuja na vague statements kama hizo ni dalili hana data.
 
Simple advice: aende kuungana na yule RC wao ambaye toka aapishwe hajui kazi nyingine bali kumbugiza mangumi Mwakyembe to JK's total satisfaction.

Sawa mkuu, nimesikia ushauri wako na nitaenda kuungana na RC.

Ila tu soma report ya Kinana ni nani alikutwa na makosa na kuomba msamaha kwa migogoro ya Kyela? Kama wewe ndio unabugizwa mangumi kwanini uombe msamaha?

Ni nani hapo juzi kakutwa ndiye anayumbisha CCM Kyela? Iweje watu waliomchagua kwa kura nyingi leo wamshutukie na kumhukumu kwa kuwa kinara wa migogoro?

Ukiwa msanii kuna siku ukweli utaanza kujulikana na ndicho kitu kinachotokea sasa kwa huyo mheshimiwa.
 

Mkuu Mkandara,

Nyie mabepari si mlisema ujamaa umekwisha kwi kwi kwi!! Sasa we are back with a vengeance, nationalizing GM, banks and other important financial institutions.

Nafikiri hata watu wa JK au Pinda walioko hapa tayari wamechukua jina lako. Nchi inahitaji watu wenye mawazo tofauti kama yako ili kusaidia kwenda mbele. Inatakiwa wawe wanavizia watu ambao wana uwezo na wanataka kurudi nyumbani ili kuwaingiza kwenye system. Ndivyo walivyofanya Asia hasa miaka ya 90.

Mimi nikiona kuna nafasi nitakuwa wa kwanza kukushutua. Nina list ya watu kama 10 JF ambao mimi ningekuwa na kazi za maana ningewapa bila hata kusita. Sitaitaja hiyo list maana unaweza kutengeneza maadui wengi badala ya marafiki.
 

hatuwezi wote kuwa polotician ila ni wajibu wetu wote kuleta maendeleo. Siku moja niliwaza kwanini James Carville au Paul Begala Wasigombee urais wenyewe badala yake wanampa akili zao zote president Clinton au Karl Christian Rove asingekuwa yeye president badala ya Bush kwa mtizamo wangu huyu jamaa ni ten time clever than bush pia David Axelrod badala ya obama mzee wa teleprompter guess who is writing.

Jibu nililolipata ni kwamba si lazima wote tungombee uraisi au ubunge bali nijukumu letu wote kuhakikisha kile tunachoamini kinafanikiwa (kwa watu wa kyela ni shule, maji afya na watu kuacha uvivu).

Badala ya kumchukia mbunge wako na kutaka ukagombee wewe (ni haki yako) akikisha amepewa muda wa kutosha kutekeleza majukumu, Ili miaka mitano( bila kumchomolea tairi za gari hakuna uchaguzi mwingine) ingalau kitu kifanyike ukimkwamisha kabisa kwanza miaka mitano inakwenda bure na pili huna uhakika wa kufanikiwa na tatu unkuwa umetesa maelfu kwa ubisfsi wako.

Mbunge wetu angefanya mambo mengi na makubwa sana kama watu wangetofautisha muda wa kampeni na muda wa kufanya kazi. sasa hata asipo deliver ana sababu kubwa ya kutuambia. Na uchaguzi wa kyela hautakuwa wa issues hata siku moja bali utakuwa wa events tu. Tutasikia hata siku moja kura zikiombwa kwa "nimeleta maji kwa vijiji 4 kata ya saba nipeni muda nimalizie vilivyobaki " bali itakuwa "mimi ninaungwa mkono na raisi"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…