Wanamtafuta tena dereva wakati uchunguzi ulishafanyika na dereva wa Mwakyembe kuonekana ndio "mzembe"? Au sio mkuu Mtanzania
Hapo Mtanzania anahusika vipi na polisi?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wanamtafuta tena dereva wakati uchunguzi ulishafanyika na dereva wa Mwakyembe kuonekana ndio "mzembe"? Au sio mkuu Mtanzania
Hapo Mtanzania anahusika vipi na polisi?
Mkuu Shalom,
"Mtu wa watu" kwi kwi kwi!! nimeipenda hii na nitaiweka kwenye manifesto yangu ya kugombea ubalozi wa mtaa hapa kijijini kwangu.
Mwenye wivu si ni yule anayekwamisha vijana wa Kyela wasiendelee? Mtu akiona vijana wanafanya kweli kiroho kinaanza kumpanda? Utamwonea wivu mtu anayeshindwa ku deliver ili iweje?
Mkuu nimekwambia tafuta sababu nyingine lakini huko kwenye majivuno au wivu hutanikuta. Kama Wanyika mmejaaa majivuno huku mnashindwa kufanya la maana kule kwenu mtakuwa wajinga kweli kweli.
Elimu ya kweli ni ile inayokusaidia kutatua matatizo yanayokuzunguka, sio ile ya kutamba mitaani na kutundika vyeti ofisini.
Elimu nzuri ni kama Dr. aliyoitumia kule kwenye Richmond, wala hakuhitaji kutamba, ile report ilikuwa inajiuza yenyewe.
Na Patricia Kimelemeta (Mwananchi) - Dereva wa Lori atafutwa
JESHI la Polisi linaendelea kumsaka dereva wa lori lililosababisha ajali iliyomjeruhi Mbunge wa Kyela, Dk Harrison Mwakyembe.
DK Mwakyembe alipata ajali hiyo mwishoni mwa mwezi uliopita, katika eneo la Ihemi mkoani Iringa akiwa njiani kutoka Makambako kuja Dar es Salaam.
Akizungumza na Mwananchi jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Robert Manumba, alisema dereva wa lori lililosababisha kupinduka kwa gari la Dk Mwakyembe, hajapatikana na kwamba jitihada za kumtafuta bado hazijazaa matunda.
Alisema dereva huyo alitoweka mara tu baada ya ajali hiyo, jambo lililosababisha asitambuliwe.
Alisema ikiwa watafanikiwa kumpata dereva huyo watakuwa wamefanikiwa kubaini chanzo cha ajali hiyo na hivyo kuhitimisha kazi ya uchunguzi.
Manumba alisema uchunguzi huo ndiyo utakaoamua kuhusu hatua za kisheria dhidi ya dereva huyo.
Mkuu Mkandara,Mtanzania,
Mkuu tuseme mathlan unazungumza unalolifahamu lakini bilka shaka mpango wa Kikwete hutokana na hoja za Wabunge kusisitiza na ukifuatilia zaidi utaona kuna baadhi ya wilaya zinmepata shule nyingi kuliko nyinginezo..
Katika swala la shule nadhani hatuna haja zaidi ya kutazama maendleo yake kwani hakika wilaya yenye shule za sekondary zaidi ya 20 ni mafanikio makubwa kwa viongozi wote wa wilaya hiyo..Kifupi hapa mimi nimebakia domo wazi na kuanza kuwafikiria wabunge wetu sisi wengine..
Kitu cha muhimu napenda kusikia zaidi malumbano yenu kwani yananipa picha zaidi ya utendaji kazi na nadhani hapa tulipo tumefikia sehemu nzuri ya kuelimishana kuliko kuendelea na upuuzi wa kukabana makoo..
Ningeomba tu kusikia zaidi mazuri ya Mwakyembe kwa wilaya ya Kyela kama alivyosema Shalom maanake swala la shule ni mojawapo, Kuhusiana na kuwasisitiza vijana kweli bila uwekezaji au kuwawezesha vijana hao ktk ubunifu ni swala ambalo bado serikali yetu inafikiria ni swala la watu binafsi..
Kama nilivyosema tumeingilia Ubepari bila kufahamu unafanya kazi vipi.. Nchi za magharibi hata zile shule au Hopspital za watu binafsi zinapata subsidies kutoka serikalini, na biashara zote hizi za huduma zinakwenda sambamba na serikali..Utakuta mgonjwa akilazwa Hospital ya Private lakini analipiwa na serikali au mtu anakwenda shule ya private na serikali inatoka kiwango fulani kufidia gharama..
Unaweza kuta mwanafunzi anaingia Chuo Kikuu akilipa dollar 10,000 lakini mwanafuinzi toka nchi ya nje ktk shule hiyo hiyo hulipa mara mbili ya kiwango hicho..
Tanzania kila kitu Private ni private hata ktk huduma muhimu utakutwa mwanya shule au Hospital ndiye anaamua kitakachofanyika na kwa ghartama gani...
Mimi nadhani inabidi tuwaelemishe Wabunge wetu, waende Bungeni na picha ya Ubepari kuliko imani waliyojengwa kwamba vUbepari ni kila mtu na mzigo wake hivyo hakuna kitu kuwezeshwa..Fanya kazi kwa nguvu ni lazima utafanikiwa!.. Hii ni imani ya kikoloni, imani potovu na haiko ktk Ubepari isipokuwa malengo huwekwa na wewe mwananchi unatakiwa ku play your part!..
Kama alivyosema Mtanzania, familia yake walikuwa wakizalisha magunia mengi wakati wa zamanai na hii nafahamu ilikuwa zamani kweli wala sii wakati wa Mkapa. Kilimo kimeanguka kutokana na mipango mibaya ya serukali nzima na hata mimi nimetoa mfano wa Ukerewe ambako tulikuwa wakulima wazuri wa Mpunga tukiuita - Faya, huu ulinukia kama wa Kyela lakini umepotea kwani wakulima walianza kula mbegu. Imetokea kila wilaya nchini na haya ni makosa ya Wabunge wote kutotetea kilimo ktk budget ya seriikali..Kama wabunge wetu wameshindwa kuikataa Budget inayokiweka kilimo, elimu na Afya nyuma ni jukumu letu kuwalaumu Wabunge wote waliopitisha budget hiyo..
Tanzania itaweza tu kujitegemea kwa kufikiria kile tunachoweza kuzalisha na kikauzika..huwezi kupandisha uchumi wa nchi kwa services ambazo zinatokana na mashirika ya nje ambayo yanatoa services moja kwa moja kwa mteja hayana chain ya trickle down..Ukitazama simu nyaya zake hatutengenezi nchini, sincard, simu zenyewe, milingoti, dish na hata uniform za wafanyakazi vyote vinaagizwa nje iweje vitu hivi vilete maendeleo nchini na viwekewe msisitizo zaidi...
Bila shaka utaona sehemu nyingi nipo na Mwakyembe kwa sababu najua kazi ngumu waliyokuwa nayo Wabunge lakini in general hawa watu hawatutendei haki wananchi na wala hakuna exceptional Kitaifa. Na ndio maana nimetaka unieleze alofanya Mwakyembe mara nyingi kama sii zote wabunge wengi huwezxi hata kuhesabu vidole vya mkono mmoja. Hardly kumkuta Mbunge kafanya mabo MATANO makuu kwa wilaya yake ktk miaka mitano aliyokaa Bungeni..
Mkuu Mtanzania,
Hoja zako nyingi zinakataa kukutana, zinapwayapwaya bila msingi mahsusi, lakini leo nimekuelewa. Una uchungu sana wa maendeleo ya Kyela na unadhani utamwondoa Dk. Mwakyembe, ambaye unamzungumzia kila mara kwa mizungukozunguko na kejeli za "kwi kwi kwi", kwa kutumia JF? Umepotea njia bro. If you are serious, nenda Kyela - wherever you are. Kwi kwi kwi kwenye JF na kwa kutumia wapambe njaa, utaishia kwi kwo kwu!
Regards.
Mhh. Mgeni huyu~~~~~!!!!! Kapela Msonda,
Join Date: Fri May 2009
Posts: 3
Thanks: 1
Thanked 0 Times in 0 Posts
Rep Power: 0![]()
![]()
![]()
![]()
![]()
![]()
![]()
![]()
Credits: 4,590
Mkuu Sikonge,
Achana na wabadilisha majina kila siku. Kama mtu una hoja na unaongea ukweli kwanini kila siku kuja na majina mapya?
Yeye tayari yuko kichwani mwangu, eti anajua nataka kufanya? Tayari yuko vichwani mwa wana Kyela, eti anajua watachaguaje? Naona aishauri NEC isifanye uchaguzi Kyela.
Tumewazoea hawa ni kama vyura ambao hawamzuii ng'ombe kunywa maji pamoja na kelele zao zote.
Mkuu Mkandara,Mtanzania,
Mkuu shukran sana, ningependa sana kuingia siasa lakini mkuu wangu mimi Mkerewe na mwoga sana wa tungule, wala sisemi uongo..kwa sababu najua zipo na zinafanya kazi muhimu nizikalie mbali wala nisikurubie..
Ubunge ni sawa na Utume ambao huwakilishi bwana mmoja ila unawakilisha watu wengi na wenye matakwa tofauti..naweza sema hata mitume wetu walikuwa na kazi kubwa lakini yenye unafuu kidogo kuwakilisha ujumbe wa Mungu mmoja kwa watu wengi kuliko kazi ya kuwakilisha watu wengi maskini kwa bwana mmoja (serikali)..Mara zote watu kama hawa huwabidi kujipachika Ubwana na heshima ni wajibu wa wananchi kuwapa, tofauti na Mitume ambao hupewa utume na ubwana wakaheshimika kwa matendo yao maokovu...
Dunia ya leo ni vugumu kupata viongozi wazuri, tazama Biblia na Msahafu utakuta mitume wote wameaminiwa na kusifika kwa kazi walizozifanya, mazuri waliyoyafanya, wokovu na zaidi ya yote unyenyekevu wao kuogopa sheria zinazowafunga ktk imani hiyo. Lakini siii wabunge, mawaziri wala marais wetu..Wao ndio Miungu, Watawala na husifika tu wakiwa jeuri, wakali, wenye kufikiria wao kile kinachowafaa wananchi..kwa sababu ndogo sana - Wao ni Watawala sii tena wawakilishi wa wananchi..
Mkuu, naona kuna sehemu member mmoja humu anasema yeye na Kombe (James) wamefundishwa certificate ya sheria na Dr Mwakyembe pale mlimani...inawezekana msingi wa hilo suala hapo juu ni huo?
Respect mkuu.
Mkuu Mkandara
MOD amefuta post na hilo limenisikitisha sana kwani inakuwa vigumu kujua nianziye wapi kwa sasa au kwa lugha nyingine amekubaliana na Mtanzania kuwa Mwakyembe ni kati ya wabunge wasiotenda kazi na wanaostahili kutopewa muda mwingine.
Mimi sikubaliana na hilo na ninasema kuwa mwakyembe ni kati ya wabunge walofanya vizuri (in fact kwa kyela hakuna mbunge yoyote ambaye ameweza kufanya aliyoyafanya DK kwa muda mfupi tangia uhuru).
Ndiyo ana mapungufu yake hata mimi huwa sikubaliani naye kwenye mambo mengine kwa mfano la kuona upinzani (uchadema) kama ni upuuzi hilo huwa napingana naye kabisa.
Sasa unapoona kuwa kuna mtu anamchukia tu bila sababu yoyote ya msingi, zipo za kusingizia nasisitiza za msingi inabidi tunaoipenda kyela tutoke na kutetea. Na kama mtu atakuja na kusibitisha kuwa kyela ya sasa sio bora kama ilivyokuwa miaka 4 iliyopita basi tutamuunga mkono.
Wengine hatuko hapa kusema vitu ambavyo vitawafurahisha watu bali tutasema vile tunavyoamini sasa kama kuna watu watachukia au kufurahi hiyo ni juu yao.
Nimemwomba MOd anitumie zile post alizofuta ili niweze kuendela na mjadala kwani imenibidi nitafute more data na hapa hapatakalika jamani. Hizi siasa zetu ni za ajabu sana hebu fikiria kuna jamaa mmoja ambaye alikuwa rafiki sana wa DK na alimsaidia kwenye kampeni lakini sasa anaongoza kumpiga majungu ukimwuliza sababu anasema eti jamaa baada ya kupata ubunge yupo karibu na shemeji zake kuliko rafiki zake sasa huo ni upuuzi kabisa. Yaani sisi tusipate mendeleo kwa upuuzi huu jamani!
Mimi ni mmoja wa watu ambao kwa kipindi kirefu sana nimekuwa fan wa kusoma comments kwenye forum hii, hivyo nawaelewa wengi na naelewa hata mwelekeo wa mawazo ya baadhi. Wewe in particular umenigusa kwa vile una mwelekeo unaomgusa mtu, sitaki kuficha, ninaye mu-admire. Kuna kosa hapo? Kuna tatizo kuanza kuchangia kwa kukushauri kuhusu ndoto yako mpaka niitwe chura? Unapata tabu gani unaposhauriwa? Badala ya kuniambia niishauri NEC isifanye uchaguzi Kyela, wewe anza kujizoeza kubugia vidonge vya BP! Sisi macho na tupo!
Mkuu Shalom,Nimemwomba MOd anitumie zile post alizofuta ili niweze kuendela na mjadala kwani imenibidi nitafute more data na hapa hapatakalika jamani. Hizi siasa zetu ni za ajabu sana hebu fikiria kuna jamaa mmoja ambaye alikuwa rafiki sana wa DK na alimsaidia kwenye kampeni lakini sasa anaongoza kumpiga majungu ukimwuliza sababu anasema eti jamaa baada ya kupata ubunge yupo karibu na shemeji zake kuliko rafiki zake sasa huo ni upuuzi kabisa. Yaani sisi tusipate mendeleo kwa upuuzi huu jamani!
Simple advice: aende kuungana na yule RC wao ambaye toka aapishwe hajui kazi nyingine bali kumbugiza mangumi Mwakyembe to JK's total satisfaction.
Mtanzania,
Mkuu shukran, nazidi kusema mimi utume siuwezi na hatukuumbwa wote kuwa viongozi wa kuwakilisha watu..Mimi ni ktk kundi la kuongozwa - Kondoo..
Nachoweza kuongoza au kuwakilisha ni uchumi, iwe shirika au kikampuni uchwara kwa sababu naamini kabisa kuwa inao uwezo na kipaji cha ubunifu ktk maswala la kuzalisha FEDHA kihalali ktk kuondokana na umaskini wa mali...
Kama una nafasi ya kazi mkuu ktk sehemu hizo nishtue, unajua tena huku kichuguu kimeota majani!..Usoshalist unachukua hatamu.
Mkuu Mkandara,
Hayo ndio matatizo ya TZ kwenye ngazi zote za utwala. Wengi wao wanashindwa ku deliver kwa visingizio mbalimbali.
Matatizo sio Kyela pekee, ni wilaya zilizo nyingi kama ulivyosema.
Labda dawa ni watu wenye mawazo tofauti kujaribu kuingia na kuibadili system kila mtu kwa uwezo wake. mwakani kuna uchaguzi ni muda mzuri kwa wale ambao wako tayari kwenda kuwavisha kengere paka hawa wanaotumaliza. Najua sio rahisi na mtapigwa vijembe vyote lakini kama una amini katika mabadiliko ya kweli ni bora ujaribu.
Kinachosikitisha tu ni wengi wanaamini lakini wakifika kwenye system ndio wa kwanza kuwa wanafiki. Wanaanza kufanya yale yale ambayo huko nyuma walikuwa wanayapinga.
Mkuu ukiamua kwenda kule Mara tutakuunga mkono bila kujali uko chama gani. Tumepiga sana kelele hapa lakini inaelekea hazizai matunda kabisa, lets stand up and be ready to be counted.