Ajali ya Dr. Mwakyembe na yatokanayo

Ajali ya Dr. Mwakyembe na yatokanayo

kuna ajali mbaya sana imetokea ihemi maeneo ya iringa karibu na kijiji cha ifunda ambayo inamhusisha dr. Mwakyembe

taarifa zaidi zinafuatia:

Picha ni hizi

i388_2.jpg

dr mwakyembe akifikishwa hospitali ya mkoa wa iringa leo baada ya ajali

i389_gari.jpg

gari la dr mwakyembe likiwa limeharibika vibaya baada ya ajali

i390_shimo.jpg

shimo lililosababisha ajari ya dr mwakyembe

nakumbuka kifo cha edward moringe sokoine april 1984 !!!

mungu akunusuru tupambane na mapinduzi kaka !!!!
 
Kuna mchangiaji alibashiri kuwa wakati wa overtaking kutakuwa na gari lilikuja mbele na dereva wa Mwakyembe akawa kwenye hati hati.

Na ndio exactly Mwakyembe alichokisema: Kuna Coaster ilikuwa inakuja mbele. Gari la Mwakyembe likaamua ku speed limalizie overtaking badala ya kujaribu kurudi nyuma ya truck. Huo ndio uzembe uliosababisha ajali.

Lakini badala ya kuacha ukweli kama ulivyo, Mwakyembe anadokeza kwamba inawezekana sio ajali, na aliyepangwa kufanya hivyo ni fundi mkubwa sana. Analeta nadharia za njama wakati gari lake ndio chanzo.
 
Jamani kuweni wakweli na hawa waandishi wa habari tanzania.. sisi sote tumeishi Bongo na tunajua barabara hizo ziko vipi.. Hakuna Lori la mizigo linalo kwenda mwendo wa 120 au 130Km/hr barabara ya Iringa hasa sehemu iliyotajwa kutokea ajali..
Nikiwa na maana kwamba haiwezekani Dreva wa Mwakyembe alilazimika kuendesha gari 140 Km/hr ili ku overtake lori ambalo lilikuwa likienda mwendo wa kawaida... Na kama kweli gari la Mwakyembe lilikuwa likienda kasi ya 140 km na lingekongwa na lori kidogo tu ubavuni basi lingeangukia over 100 metres from the scene of accident..haikutokea hivyo!..
Hapa maneno yameongezwa - WHY hilo ndio swali la kujiuliza!

Mkuu Bob,

hiyo speed niliwahi kuishuhudia mwenyewe kwa malori ambayo hayana mizigo, kwa kweli lilivyonipita lile lori na ile speed na sehemu tuliyokuwa nilishangaa sana.......kwa hiyo sioni ajabu kusikia lori lisilo na mzigo likiwa kwenye speed ya aina hiyo.........
 
Engineer punguza speculations usizokuwa na uhakika nazo.Zinapunguza reliability yako kwa mtu anayeita Engineer(proffession ya mambo hakika)
Kwa tarifa yako Makambako hadi Iringa kuna kilometa karibu 180, hata mabasi hayachukui masaa 3 kusafiri mwendo huo, sembuse gari dogo linaloenda 120km per hr!

Lole,

Usiwe unaleta ubishi usio na maana. Nimekuambia mwendo kisheria na wala sio mwendo ambao wewe unaendesha. Ukitaka nenda hata 1000km/h.

Hiyo njia sehemu nyingi maximum speed ni 80kms/h na baadhi ya sehemu iko chini ya hapo. Sasa kama umbali ni km 180, kwa huo mwendo ambao ndio unakubalika kisheria utatumia masaa mangapi?

Ulivyo mjinga unafikiri hata gari likienda 80km/h basi safari nzima itakuwa hivyo. Katikati kuna vijiji na miji ambapo speed iko mpaka 40km/h. Ukitafuta wastani ni hayo masaa matatu.

Wavunja sheria ndio mnakimbia na mkipata ajali mnasingizia mkono wa mtu.
 
Mkuu, mbona arguments zako hazilingani na hadhi ya usomi na uhandisi uliojipa? Mwenzako anajenga hoja, wewe unabwatuka kwa hoja zisizo na mpangilio na kukimbilia matusi ya rejareja kama "usiwe unaleta ubishi usio na maana" na "ulivyo mjinga unafikiri ..." n.k. Hebu tumegee kidogo, wewe engineer wa nini, wa matusi?
 
Kuna mchangiaji alibashiri kuwa wakati wa overtaking kutakuwa na gari lilikuja mbele na dereva wa Mwakyembe akawa kwenye hati hati.

Na ndio exactly Mwakyembe alichokisema: Kuna Coaster ilikuwa inakuja mbele. Gari la Mwakyembe likaamua ku speed limalizie overtaking badala ya kujaribu kurudi nyuma ya truck. Huo ndio uzembe uliosababisha ajali.

Lakini badala ya kuacha ukweli kama ulivyo, Mwakyembe anadokeza kwamba inawezekana sio ajali, na aliyepangwa kufanya hivyo ni fundi mkubwa sana. Analeta nadharia za njama wakati gari lake ndio chanzo.
wewe kwa investigation yako unaonaje?
 
Mkuu,
hoja zako mbili zimenilazimu nikusaidie uone upande wa pili wa sarafu! Kwanza unasema "Gari la Mwakyembe likaamua ku speed limalizie overtaking badala ya kujaribu kurudi nyuma ya truck. Huo ndio uzembe uliosababisha ajali". Mkuu, wewe unaongelea truck, wakati Mwakyembe anaongelea semi-trailer, low loader! Kwa kuwa gari alilokuwa analipita lilikuwa semi-trailer, kurudi nyuma isingekuwa rahisi hivyo! Una risk kugongwa na trailer ya nyuma! Madereva wengi tungeamua kama alivyofanya dereva wa Mwakyembe: kwenda mbele kwa kasi zaidi. Mwakyembe anasema, na mimi nimemsikiliza, mini-bus hiyo ilikuwa bado mbali! Vilevile, comments zako Mkuu kwamba kulikuwa na "uzembe" n.k. si za busara wakati suala liko mikononi mwa vyombo vya sheria. Tusi behave kama gazeti la Tanzania Daima ambalo bado linaendeleza kampeni zake dhidi ya chochote kinachomhusu Mwakyembe. (Hongera ndoa ya Rostam na Kibanda!)

Pili, unasema "Mwakyembe anadokeza kwamba inawezekana sio ajali, na aliyepangwa kufanya hivyo ni fundi mkubwa sana. Analeta nadharia za njama wakati gari lake ndio chanzo". Mkuu, kwa nini ufunge akili ya watu? Kwa nini isiwezekane kuwa njama? Unaposema gari lake "ndio chanzo", una ushahidi gani? Ushahidi wa Tanzania Daima? Mkuu, waache watu wafikiri "outside the box". Afterall, mashahidi pekee wa kusikilizwa hapa ni: Dk. Mwakyembe, dereva wake na dereva wa lori ambaye anadai aliona ajali mbaya ikitokea mbele yake, lakini hakusimama, akaendelea na safari! Sisi wengine ni udaku bin udaku tu!

Mkuu nimalizie kwa kusema, statement ya Polisi saa chache baada ya ajali, kabla hata ya kumhoji dereva wa lori, dereva wa Mwakyembe na Mbunge mwenyewe (ambaye wakati huo alikuwa hajitambui) kwamba hakukuwepo hujuma, inatia mashaka sana juu ya usafi, uadilifu na umakini wa jeshi letu la Polisi!
Doulton
 
Mwakye.jpg

Mbunge wa Kyela, Dk. Harrison Mwakyembe, akiwa kwenye kitanda cha wagonjwa wakati akipelekwa wodi ya Taasisi ya Mifupa ya Muhimbili (MOI).

Sakata la ajali iliyompata mbunge wa jimbo la Kyela, Dokta Harrison Mwakyembe, umeingia katika hatua mpya baada ya baadhi ya watu kudai kuwa ajali hiyo ilipangwa na lengo lake lilikuwa kummaliza.
Baadhi ya watu waliozungumza na Alasiri wamesema uwepo wa taarifa tofauti zinazohusiana na chanzo cha ajali hiyo, unaonyesha wazi kwamba `si bure’.
Mmoja wa watu waliodai kuwa ajali hiyo ina mkono wa mtu ni Mwenyekiti wa DP, Mchungaji Christopher Mtikila ambaye amesema maelezo ya Dk. Mwakyembe na dereva wake ndiyo yanapaswa kuwa ya kweli kwa vile wao ndio walikuwa kwenye eneo la ajali.
"Polisi walifika baada ya ajali, lakini Dk. Mwakyembe na dereva wake wameishuhudia ajali, hivyo maelezo yao ndiyo yako sahihi," akasema Mchungaji Mtikila.
Akasema kitendo cha Polisi kutoa maelezo tofauti na wao ndicho kinachozidi kuleta mashaka.
``Hapa kuna jambo. Walioshuhudia ajali wanatoa maeleo yao na wasioshuhudia nao wanaleta yao…hili ndilo linaleta utata,’’ akasisitiza Mchungaji Mtikila.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa chama cha TLP,Bw. Augustine Mrema amesema licha ya kuwa Polisi wana maelezo tofauti, kinachopaswa kufanywa hivi sasa ni kuwaachia wachunguze ukweli wa chanzo cha ajali hiyo na kutoa ripoti yao.
Amemshauri Dk. Mwakyembe kutoendelea kulizungumzia suala hilo na badala yake aachie dola ifanye kazi yake.
Kabla ya kutoa rai hiyo, Bw. Mrema alimpa pole Dk. Mwakyembe kwa kupata ajali hiyo, huku akimtaka aendelee kujiweka mikononi mwa Mungu.
Maelezo ya Polisi kuhusiana na ajali hiyo yanadai kuwa gari la Mheshimiwa Mwakyembe wakati likijaribu kulipita lori, lilivaa shimo lililokuwa katikati ya barabara, tairi likachomoka na hivyo gari likapoteza mwelekeo na kuingia porini ambako lilipinduka mara nne.
Hata hivyo dereva wa gari la Dk. Mwakyembe alisema lori lilimpa saiti ya kupita na alipofanya hivyo, likamzibia tena njia, kitendo kilichosabisha ajali.
Dk. Mwakyembe alipata ajali mbaya juzi katika eneo la Ihemi, mkoani Iringa wakati akitokea jimboni mwake kuja Jijini Dar es Salaam.
Baada ya ajali hiyo, Dk. Mwakyembe alikimbizwa katika Hospitali ya Mkoa wa Iringa kabla ya kusafirishwa kwa ndege ya kukodi kuletwa Dar es Salaam na kulazwa katika Taasisi ya Mifupa Muhimbili, MOI.
Hata hivyo jana jioni Dk. Mwakyembe aliruhusiwa kutoka hospitalini baada ya madaktari kuwa afya yake imeimarika.
 
Jamani kuweni wakweli na hawa waandishi wa habari tanzania.. sisi sote tumeishi Bongo na tunajua barabara hizo ziko vipi.. Hakuna Lori la mizigo linalo kwenda mwendo wa 120 au 130Km/hr barabara ya Iringa hasa sehemu iliyotajwa kutokea ajali..
Nikiwa na maana kwamba haiwezekani Dreva wa Mwakyembe alilazimika kuendesha gari 140 Km/hr ili ku overtake lori ambalo lilikuwa likienda mwendo wa kawaida... Na kama kweli gari la Mwakyembe lilikuwa likienda kasi ya 140 km na lingekongwa na lori kidogo tu ubavuni basi lingeangukia over 100 metres from the scene of accident..haikutokea hivyo!..
Hapa maneno yameongezwa - WHY hilo ndio swali la kujiuliza!

nakubaliana na wewe
120 -130 km/hr ni sawa na 90miles/hr
hiyo speed hata kwa lori huku ulaya ni kubwa sana na malori ya tz ni mazee sana
pili kama dereva wa lori alikuwa 130 siwezi kuamini kama alikuwa anamchelewesha dr mwakyembe...
kwa hiyo inamaanisha hilo lori lilikuwa mwendo wa konokono..

kwa barabara za tz gari likikupita hata likiwa 90km/h kwa ajili ya udogo wa barabara unaweza ukazani liko 200km/h
 
...

Nani kakudanganya malori yote yanakwenda mwendo wa konokono? Nadhani umeondoka bongo siku nyingi na kama uko bongo basi hujasafiri ukakuta na malori yanayokwenda speed kuzidi hata mabasi.
 
Mkuu,
hoja zako mbili zimenilazimu nikusaidie uone upande wa pili wa sarafu! Kwanza unasema "Gari la Mwakyembe likaamua ku speed limalizie overtaking badala ya kujaribu kurudi nyuma ya truck. Huo ndio uzembe uliosababisha ajali". Mkuu, wewe unaongelea truck, wakati Mwakyembe anaongelea semi-trailer, low loader! Kwa kuwa gari alilokuwa analipita lilikuwa semi-trailer, kurudi nyuma isingekuwa rahisi hivyo! Una risk kugongwa na trailer ya nyuma! Madereva wengi tungeamua kama alivyofanya dereva wa Mwakyembe: kwenda mbele kwa kasi zaidi. Mwakyembe anasema, na mimi nimemsikiliza, mini-bus hiyo ilikuwa bado mbali! Vilevile, comments zako Mkuu kwamba kulikuwa na "uzembe" n.k. si za busara wakati suala liko mikononi mwa vyombo vya sheria. Tusi behave kama gazeti la Tanzania Daima ambalo bado linaendeleza kampeni zake dhidi ya chochote kinachomhusu Mwakyembe. (Hongera ndoa ya Rostam na Kibanda!)

Pili, unasema "Mwakyembe anadokeza kwamba inawezekana sio ajali, na aliyepangwa kufanya hivyo ni fundi mkubwa sana. Analeta nadharia za njama wakati gari lake ndio chanzo". Mkuu, kwa nini ufunge akili ya watu? Kwa nini isiwezekane kuwa njama? Unaposema gari lake "ndio chanzo", una ushahidi gani? Ushahidi wa Tanzania Daima? Mkuu, waache watu wafikiri "outside the box". Afterall, mashahidi pekee wa kusikilizwa hapa ni: Dk. Mwakyembe, dereva wake na dereva wa lori ambaye anadai aliona ajali mbaya ikitokea mbele yake, lakini hakusimama, akaendelea na safari! Sisi wengine ni udaku bin udaku tu!

Mkuu nimalizie kwa kusema, statement ya Polisi saa chache baada ya ajali, kabla hata ya kumhoji dereva wa lori, dereva wa Mwakyembe na Mbunge mwenyewe (ambaye wakati huo alikuwa hajitambui) kwamba hakukuwepo hujuma, inatia mashaka sana juu ya usafi, uadilifu na umakini wa jeshi letu la Polisi!
Doulton

- Saafi sana, Mwakyembe ana haki zote kuamini anachotaka kama sisi wengine, cha muhimu hapa JF ni hoja, kama Mwakyembe anaweza kujenga hoja na hofu zake hapa tutazichambua tu, lakini hatuwezi kunyamazisha haki ya Mwakyembe kuwa na maoni yoyote anayotaka kuwa nayo.

- Ninampa pole sana DK, na Mungu amsaidie apone haraka maana bado tunamuhitaji sana na tumem-miss sana Busanda.

Ahsante.

William.
 
nakubaliana na wewe
120 -130 km/hr ni sawa na 90miles/hr
hiyo speed hata kwa lori huku ulaya ni kubwa sana na malori ya tz ni mazee sana
pili kama dereva wa lori alikuwa 130 siwezi kuamini kama alikuwa anamchelewesha dr mwakyembe...
kwa hiyo inamaanisha hilo lori lilikuwa mwendo wa konokono..

kwa barabara za tz gari likikupita hata likiwa 90km/h kwa ajili ya udogo wa barabara unaweza ukazani liko 200km/h

Nani kakudanganya malori yote yanakwenda mwendo wa konokono? Nadhani umeondoka bongo siku nyingi na kama uko bongo basi hujasafiri ukakuta na malori yanayokwenda speed kuzidi hata mabasi.
sijasema malori yote yanakwenda mwendo wa konokono nimesema sababu ya mwakyembe kumu overtake ni lazima hilo lori litakuwa lilikuwa polepole(konokono)
haitaji rocket science kujua hili
kama lori likupita inamaanisha liko speed, ukilipita inamaanisha liko polepole inamaanisha polepole ya tz ni 130km/h kwa barabara zipi?
nilipokuja kufatwa airport dereva alikuwa mbio kuangalia speed 70km/h kumbe sio mbio bali ufinyu wa barabara

wewe unatuambia lori ambalo nyuma lina mtoto lilikuwa speed ya 130km/h na barabara yenyewe ni single dual carriage way kama inavyoonyesha kwenye picha, lazima uwelewe hiyo barabara ni ndogo gari likupita likiwa 90km/h na upepo unakuwa mkali kama ujui mambo ya speed unaweza ukadhani hilo gari liko 200km/h, gari likikupita kwenye barabara tatu hata likiwa 200km/h uhuisi vishindo vya upepo ambavyo utavipata gari likiwa speed 100km/h kwenye barabara moja
 
- Mkuu Semilong, saafi sana maelezo mazito sana haya na ubarikiwe!

Respect.

FMES!
 
Date::5/23/2009

Utata ajali ya Mwakyembe unahitaji taarifa sahihi

Mwananchi

MBALI na hekaheka za kampeni za uchaguzi mdogo wa Busanda, wilayani Geita, Mwanza na mabomu ya Mbagala, jijini Dar es Salaam; tukio lililoshitua wengi wiki hii, ni ajali mbaya ya barabarani aliyopata Mbunge wa Kyela, Dk Harrison Mwakyembe baada ya gari lake kuchomoka gurudumu la mbele kisha kupinduka eneo la Ihemi, Ifunda mkoani Iringa.

Mbunge huyo ambaye alipata ajali Alhamisi asubuhi akitoka Mbeya kurudi Dar es Salaam na kuhamishiwa jijini kwa matibabu zaidi katika Taasisi ya Mifupa Muhimbili, ameruhusiwa kutoka baada ya madaktari kuridhika na maendeleo mazuri ya afya yake.

Hata hivyo, kutokana na umaarufu wa Dk Mwakyembe, uliongezeka baada ya kamati yake ya Bunge ya kuchunguza mazingira ya utoaji zabuni ya kufua umeme wa dharura kwa kampuni ya Richmond kufanya kazi nzuri, kuliwafanya watu wengi kupata mashaka kwamba huenda kuna mkono wa mtu.

Utata unazidi kujitokeza kutokana na kutofautiana kati ya taarifa iliyotolewa na polisi na ya upande wa Dk Mwakyembe. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Advocate Nyombi alisema ajali hiyo ilitokea wakati dereva wa Dk Mwakyembe akitaka kulipita lori lililokuwa mbele yao, lakini akaingia kwenye shimo, ndipo gurudumu la mbele likachomoka na kisha kugonga mti. Lakini Dk Mwakyembe na dereva wake wamedai kuwa kabla ya ajali hiyo waligongwa kwa nyuma na lori hilo ambalo mpaka sasa taarifa zake zinatatanisha.

Kwa ujumla, utata huo unaendelea kutia mashaka juu ya ajali hiyo, hivyo taarifa zaidi inatakiwa kutolewa na vyombo husika vya umma. Mbali na taarifa yake ya awali, baada ya madai ya upande wa Dk Mwakyembe, Kamanda Nyombi alisema hawezi kutoa taarifa nyingine kwa sababu uchunguzi wa tukio hilo unaendelea kufanyika.

Tunadhani kuna haja ya kuweka wazi haraka matokeo ya uchunguzi wa ajali hiyo kwa vile kwa vyovyote vile watu wanaanza kuhusisha ajali hiyo na mambo mengine na hasa mapambano dhidi ya ufisadi. Ni dhahiri kwamba wapo wanaodhani kuwa kuna mkono wa mtu ingawa, Mwakyembe hakuzungumzia hilo, bali alisema kama ni mtu anamwachia Mungu.

Ni kawaida mtu maarufu na hasa aliyeweka rekodi katika mambo fulani yaliyoungwa mkono kutokana na mchango wake katika kupigania haki; anapopatwa na janga au jambo lisilo la kawaida, hasa linalotishia uhai wake ni rahisi kuhusisha na njama za kutaka kummaliza ili maadui zake wapate nafuu.

Hata kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Moringe Sokoine kilichotokea katikati ya mapambano yake dhidi ya wahujumu uchumi, kilizua hisia nyingi katika jamii ikiwemo ya kuwa aliuawa na mpaka sasa baadhi ya watu wanaamini hivyo.

Kwa sababu hiyo basi, utata uliojitokeza katika taarifa zilizotolewa na polisi na upande wa Dk Mwakyembe zinazotofautiana sana, upatiwe majibu sahihi na taarifa itolewe mapema, vinginevyo utaifanya jamii iamini kile inachokiamini.
 
Taarifa sahihi ni hii:

1. Mwakyembe na dereva wake ndio chanzo cha ajali, ajali haichagui, uwe mbunge, muuza karanga au waziri.
2. Taarifa ya polisi inawezekana kabisa kuwa haikuwa ya kweli wka sababu zifuatazo.
(a) ndio siku zote wako hivyo na haiwezekani wawe makini kwa sababu eti mwakyembe kapata ajali
(b) kuna uwezekano mkubwa kuwa, walichanganyikiwa na ajali ya Mwakyembe na wakasahau hatua muhimu za kuchukua, wakabaki kutaka kuokoa maisha ya Mwakyembe

3. Kama kuna mtu alipanga jali hii, basi ana akili sana, YAANI ALIINGIA KICHWANI MWA MWAKYEMBE NA KUMWAMBIA DEREVA WAKE AOVATEKI LORI kwa speed 140! halafu wagongwe, mpangaji ajali hii lazima sio mwanadamu wa kaiwada!

4. Ni wakati mzuri wa Mwakyembe na viongozi wengine kujua kuwa hakuna sensor kwenye vyombo vya moto inayotofutisha kati ya waziri, mpiganaji wa mafisadi na rais, wote sawa tu.

5.Hivi nani amuue Mwakyembe?? CHADEMA?? maana Chadema kupita kwenye jimbo la mwakyembe wasahau! labda afe LAKINI KUSEMA ETI MAFISADI NANI?? WANAGOMBANA KWENYE VYOMBO VYA HABARI JIONI WANAGONGA GLASS, CHAMA KIMOJA, NGUVU MOJA, KUNA FISADI KAENDA JELA KWA SABABU YA MWAKYEMBE ?-HAPANA, NANI WA KUMUUA MWAKYEMBE?? AU TUMEZOEA TU KILA AJALI IMEPANGWA??

KWA CCM, uhai wa Mwakyembe ni mali na muhimu sana kwao, unafikiri huko Busanda au magogoni angesisamishwa Mwakyembe kupiga kampeni kwa mgombea wa CCM kuna mtu angeenda kinyume?? kasimama Rostam watu wameshinda, je Mwakyembe?? au atagoma wakati ni mwana-CCM??

Mwakyembe atakuwa threat tu na kuwa katika hali ya kuuawa kama akihama CCM wakiwa ndani ya CCM (ni watu wa kuuzwa ili chama kishinde) haijalishi kuna mafisadi au wasafi-Kalagabhao!!
 
Lole,

Usiwe unaleta ubishi usio na maana. Nimekuambia mwendo kisheria na wala sio mwendo ambao wewe unaendesha. Ukitaka nenda hata 1000km/h.

Hiyo njia sehemu nyingi maximum speed ni 80kms/h na baadhi ya sehemu iko chini ya hapo. Sasa kama umbali ni km 180, kwa huo mwendo ambao ndio unakubalika kisheria utatumia masaa mangapi?

Ulivyo mjinga unafikiri hata gari likienda 80km/h basi safari nzima itakuwa hivyo. Katikati kuna vijiji na miji ambapo speed iko mpaka 40km/h. Ukitafuta wastani ni hayo masaa matatu.

Wavunja sheria ndio mnakimbia na mkipata ajali mnasingizia mkono wa mtu.

Dont panic mzee , ukweli unabaki palepale.Basi la abiria katika sehemu hizo kwenda kwa mwendo wa kisheria wa 80km/hr ni mtazamo wa kusadikika.
Bahati mbaya watu kama wewe kama kweli ni engineer then you are making a poor case for your self.Reality ni kitu kingine kabisa .
Acheni kupasha moto viti maofisini ma muone mambo yanayotokea barabarani.
Nimeshuhudia basi likienda over 160 km/hr(Scania engine)-Mbeya -Igawa stretch
Nimeshuhudia lori tanker tupu-(Scania engine) going over 130km/hr(tena jana) between Kitonga -Mbuyuni stretch
Magari ya sasa hivi when you are talking of an official 80km per/hr basi inabidi urudi shule ili kufanya traffic studies upya kabisa.Na hili ndio kosa walifanyalo watendaji wengi- kubase argument zao na mambo ya kusadikika na sio reality on the ground.
 
Mkuu Lole,

Sitaki kuingilia mabishano yako na Engineer ila ninapata wasiwasi na baadhi ya mambo uliyoyaandika hapo juu.

Hiyo barabara mimi nimeipita mara nyingi na kwa kweli ndugu yangu kama unapanda basi linaloenda kwa hiyo speed au unaendesha gari kwa speed karibu na uliyoandika hapo juu basi unachezea maisha yako. Utakuwa sawa na mtu anayeenda kufanya ngono bila condoms kwenye mji ambao maambukizi ya ukimwi ni asilimia zaidi ya 20.

Speed ya 160km/h ni sawasawa na 100m/h, mwendo ambao hata kwa barabara kubwa, imara na magari mapya ambayo watu wanayo kama hapa UK, watu wengi hawawezi kuukaribia. Maximum speed hapa ni 70m/h ambayo ni 112k/h. Labda hawa wazungu huku na barabara zao hawajui traffic studies.

Bahati nzuri kazi zangu zinahitaji kuzunguka nchi nzima (UK) na kwa mwaka ninafikisha hata miles 35,000. Barabara ambayo inafanana na hiyo ya kwetu huko Mbeya mpaka Iringa ni barabara inayounganisha England na Scotland. Kuna umbali wa kama miles 50 ambazo ni nyembamba kama barabara ya kwetu ingawaje ni imara zaidi maana haina mashimo wala haijabonyea, maximum speed ni 50miles/h ambayo ni sawa na 80kms/h.

Kidogo napata shida nikisoma maelezo yako hapo juu. Ni kama unaona it's OK kwa magari kwenda speeds kubwa kiasi hicho. Ni sawa kuna mara nyingi tu abiria watafika salama, kama ambavyo hata kwenye ngono, watu wengi tu wasiotumia condoms bado ni wazima. Lakini kweli kuna haja ya kuchukua risks za namna hiyo?

Ushauri wa bure; tusingetaka kukupoteza; jihadhari na huo mwendo kasi; usipande mabasi yanayokimbia kiasi hicho. Maisha yako ni bora zaidi ya masaa machache ya kuwahi uendako. Ndio maana wengine tunakwepa baadhi ya yale mabasi ya Kyela kwasababu ya speeds zao. Siwezi kuhatarisha maisha yangu kiasi hicho. Sawa kila mtu atakufa lakini kweli kuna haja ya kutokuwa makini kiasi hicho? Halafu ikitokea ajali tunaanza kutafuta mchawi.
 
Nashukuru kwa ushauri wa bure,lakini soma tafadhali submission yangu ya awali.
NIMEONA basi zinazokwenda spidi hizo, hii ni baada kwa utundu tu kulifukuzia basi hilo nikiwa naundesha gari dogo jingine., na nilishangaa.
Pita barabara hiyo na utajionea vioja.
Polisi wanapewa mshiko na ni mwendo wa kasi kama kawa!!
Na ndio maana mabasi ya Mbeya yakipata ajali watu wanaokufa ni wengi sana.
Tatizo kubwa hapa ni technologia.
Haya mabasi, hata magari mengi ya kisasa ni very powerful ukilinganisha na mzigo unaobebwa.Hivyo basi huwa ni mepesi barabarani
Barabara zetu hazija catch up na technologia hii ya magari ya kisasa.Pengine barabara yenye technologia inayo karibia ubora wa magari yetu ya sasa ni barabara kati ya Chalinze na Morogoro.
Na ndio maana hapo awali ndugu engineer kama yuko katika vyombo vya miuondo mbinu nimemshauri kuwa ni vyema studies zika fanyika ili kusaidia kuondoa kutowiana kati ya uwezo wa magari na barabara zetu(traffic studies).
Lazima tuondokane na dhana kuwa uendeshaji wa magari barabarani iwe hisani ya madereva,lazima technology i control dhana hii.
 
Back
Top Bottom