Ajali ya Dr. Mwakyembe na yatokanayo

Ajali ya Dr. Mwakyembe na yatokanayo

Nashukuru kwa ushauri wa bure,lakini soma tafadhali submission yangu ya awali.
NIMEONA basi zinazokwenda spidi hizo, hii ni baada kwa utundu tu kulifukuzia basi hilo nikiwa naundesha gari dogo jingine., na nilishangaa.
Pita barabara hiyo na utajionea vioja.
Polisi wanapewa mshiko na ni mwendo wa kasi kama kawa!!
Na ndio maana mabasi ya Mbeya yakipata ajali watu wanaokufa ni wengi sana.
Tatizo kubwa hapa ni technologia.
Haya mabasi, hata magari mengi ya kisasa ni very powerful ukilinganisha na mzigo unaobebwa.Hivyo basi huwa ni mepesi barabarani
Barabara zetu hazija catch up na technologia hii ya magari ya kisasa.Pengine barabara yenye technologia inayo karibia ubora wa magari yetu ya sasa ni barabara kati ya Chalinze na Morogoro.
Na ndio maana hapo awali ndugu engineer kama yuko katika vyombo vya miuondo mbinu nimemshauri kuwa ni vyema studies zika fanyika ili kusaidia kuondoa kutowiana kati ya uwezo wa magari na barabara zetu(traffic studies).
Lazima tuondokane na dhana kuwa uendeshaji wa magari barabarani iwe hisani ya madereva,lazima technology i control dhana hii.

Mkuu Lole,

Siku nyingi usije ukaja fanya utundu wa kulifuata gari linalokimbia, wewe ndio utakuwa wa kwanza kupata madhara.

Unataka technology gani ya barabara kukabiliana na hao madereva?

Je barabara ya Chalinze na Morogoro ina nini ambacho kinaweza kuzuia magari yasikimbie?

Dawa ni moja tu, ni kuandama mifuko ya madereva pamoja na wenye magari. Mkuu nakuhakikishia, ningelikuwa na kazi kama ya Masha, miaka miwili hizo ajali zingelipungua kwa asilimia kubwa sana. Sijipigii debe kwi kwi kwi!!! Lakini ndio ukweli wenyewe. Studies zote zimeonyesha binadamu wengi wako tayari kuchukua risks mbalimbali mpaka pale wanapoona mifuko yao itakuwa matatizoni. Kama ni technology basi itumike kukamata hao culprits ili wawajibike.

Iweje kila siku tunaongelea jambo moja kama vichaa bila kupata jawabu lake. Kwa Tanzania sioni barabara yoyote ya maderva kwenda speed zaidi ya 120kms/h.

Kama serikali inashindwa basi iwe tayari kutumia private companies kukamata hao culprits na mapato yao yatokane na asilimia ya pesa zinazopatikana. Pia serikali irahisishe sheria ili watu wanaodhurika na hizo ajali iwe rahisi kuwafungulia mashitaka wamiliki wa magari hayo. Uwajibikaji usiishie kwa dereva na uende mpaka kwenye mwenye gari.

Wakati mwingine mabadiliko yanakuja kwa manguvu.
 
Lole G,

Huko nyuma niliandika ila naona hukusoma. Ujenzi wa barabara ni kitu kimoja aghali sana na nchi chache sana wanafanya hivyo bila ya kusikia makali ya pesa zilizotumika na kwa Tz, barabara nyingi twajenga kwa msaada wa Wafadhili.

Sijui una maana gani unaposema hizo technology. Kwenye ujenzi wa barabara, Traffic Engineers mara nyingi hulazimisha madereva wafuate nini wao wanakitaka. Hii hutokana na pesa kidogo iliyopo katika ujenzi wa hiyo barabara. Pia acha kujenga, inabidi iwepo pesa ya kuitunza hiyo barabara kwa kukata miti na nyasi za pembeni mwa barabara, kuziba mashimo, kutunza alama za barabarani au kuweka mpya pale inapobidi nk.
Traffic Engineer wana sheria na utaratibu wao wa kufanya hivyo na wakati mwingine mtu wa kawaida unaweza kuona ni kituko. Ila ndivyo lilivyo hilo somo. Sasa wakishamaliza kazi yao, na hawa ndiyo huwa watu wa mwisho kumalizia kazi kwa kuweka alama za barabarani, barabara hukabidhiwa na kuanza kutumiwa. Sasa nini kitafuata baada ya hapo, hiyo huwa ni kazi ya Traffic (POLISI). Dawa kubwa ya kupunguza rushwa ni kuweka magari yaliyo na camera ndani na hizo camera zimeungwa na mtandao wa internet kwenye vituo vya mkoa au POLICE head office ili mtu baadaye asipokee pesa kwani kila kitu kinakuwa kimerekodiwa. Pesa inayopatikana kwenye faini kwa hawa madereva wazembe, inatosha kabisa kununua magari mengine na camera zaidi, yaani kutokana na uzembe wa madereva wengi wa tz, haya magari kwa siku yangelikuwa yanaingiza hata dola 2,000 au zaidi per car. Faini haitakiwi ziwe za kuuwana sana ila ziwe zinatolewa kulingana na kufanya makosa ya kizembe na zaidi ni kwa wale wanaozidisha speed au ku-overtake sehemu zisizotakiwa kufanya hivyo.

Nafikiri baada ya muda upupu huu ungelipungua sana hasa baada ya madereva kuwa wanapigwa faini kushoto na kulia na kila kosa anajiwekea points na zikifika limit fulani basi anazuiliwa kuendesha gari kwa muda tuseme mwezi mmoja na inabidi aende kwenye shule special ambazo atalipia kwenye shule ya driving licence na lazima aje na kithibisho kuwa alikuwa kwenye shule hizo.

Haiwezekani madereva nchini watu-terolise Watz wote barabarani. Wao ni kundi dogo sana na kama tungelikuwa na serikali imara, sidhani kama hii kitu ingelikuwa inasumbua kiasi hicho. Yes, bado wangelikuwemo kichwa ngumu, ila hata wao wangelikuja kujua nini kinawasuburi, wangelianza kufikiri mara mbili.
Ila TATIZO la Tanzania, kama watu hawathibiti mali kubwa kubwa za Nchi, itakuwa makosa ya barabarani? William Malecela alisema juzi juu ya watu wa Igunga/Wanyamwezi kuwa "Acha wafu wawazike wafu wenzao.." Mie naona hata hili la barabarani, kama wakija watu wa Scandinavian, basi wakiona vituko vya barabarani na ajali zinazotokea, basi wanasema "Acha wafu......." Na kweli tutazikana sana. Sishangai hata Mzungu aligoma kumchukua Dr. na kuondoka zake (halafu eti dereva anatoa bastola....... hee, yeye ndiyo alikulazimisha u-overspeed?)
 
mwakyembe angeachiwa atoke halafu ukweli ndio utajulikana sidhani kama sasa hivi yuko kwenye good state of mind....

kitu ambacho watu humundani wanakanusha ni maneno ya mwakyembe, mwenyewe amesema walikuwa wanataka kuliover take gari wakawa wanalionyeshea indicator likakaa kimya baade likawa ruhusu, lilivyowaruhusu walivyokuwa wanataka kulimalizia likaongeza speed likawa linawafuata kwenye lane yao na kuwa push pembeni....
na dereva akarudia hivyo nakusema likawa linawasukuma pembeni mpaka akawa amelazimika kwenda pembeni kwenye majani
 
Mkuu, hii ni biashara ya kuandika kumbukumbu kwa mate badala ya wino! Waliohusika na kushuhudia ajali hiyo ikitokea wameongea. Sisi ambao hatukuwepo, tunaporomosha kila aina ya theory ku-contradict ushahidi wao. Kazi ya Polisi ni kuu-test ushahidi wa Dk. Mwakyembe na Dereva wake mahakamani na si vinginevyo! Huo ndo utawala wa sheria!

Polisi wakiendelea kukaidi kulitafuta lori hilo kwa sababu za kibinafsi au za kisiasa, watakuwa wanapoteza fedha za Jamhuri na muda kuendelea na kesi hii. Itakuwa sawa na kuendesha kesi ya KAGODA bila kumhoji ROSTAM AZIZ; kesi ya RADA bila kumhoji CHENGE, IDRISSA na SOMAIA; kesi ya RICHMOND/DOWANS bila kumhoji LOWASSA, ROSTAM na MSABAHA; kesi ya Kiwira Coal Mine bila kumhoji MKAPA na YONA; kesi ya helikopta za jeshi bila kumhoji SOMAIA; kesi ya majengo ya NSSF bila kumhoji MANJI; kesi ya mabilioni ya IMPORT SUPPORT bila kumhoji ROSTAM; kesi ya Liganga na Mchuchuma bila kumhoji SHUBASH PATEL na KARAMAGI n.k.!
 
Mkuu LazaroSmtindi,

Karibu tena mkuu mbona ulipotea hivyo?

Kama ulikuwa unaumwa pole sana na karibu tena tuendelee na Libeneke letu.

Vipi siasa za Kyela na Mbeya? Vipi viboko hawajamaliza kula mazao ya wakulima?

Nakubaliana na wewe inatakiwa polisi TZ wawe wanafanya uchunguzi makini. Kuacha mambo bila kuchunguza ndio maana hata wapika majungu wanatokea. Lakini hata sisi wananchi tukiona watu wanatenda makosa tupeleke taarifa polisi. Kwa mfano ukiona mtu anahonga wananchi au wananchi wanasema wamehongwa na fulani, inabidi ukatoa report polisi.
 
Ripoti ya Tume iliyoundwa kuchunguza ajali hii, imesema kuwa Mhe. Mwakyembe alikuwa amelala usingizini wakati ajali inatokea na kumuonya kutotoa maelezo/maoni ya ajali hiyo kwani alikuwa usingizini na hana taaluma katika fani hiyo.

Uchunguzi wa kudhibitisha kuwa Mhe. alikuwa amelala ulifanywa na mtaalamu aliyesomea Uingereza, kwa kusema kuwa kiti alichokalia Mh. kinaonyesha kuwa alikuwa usingizini wakati wa ajali hiyo. Na iwapo angalikuwa yupo macho basi leo hii ingekuwa ni hadithi nyingine.

Aidha chanzo cha ajali sio shimo wala kugongwa na lori, bali ni mwendo kasi uliosababisha Shofeli kushindwa kulimudu gari lake kabla ya kulifikia shimo hilo. Zaidi baada ya kulivaa shimo hilo tairi moja lilichomoka na gari kukusosa mwelekeo kabla ya kulivaa jiwe kubwa pembeni ya barabara hiyo lilisababisha tairi la pili kuchomoka na gari kuanguka na kugonga mti wenye kipenyo cha sm 117. Kasheshe hilo lote hadi gari kusimama ni urefu mita 67 tokea kwenye shimo.
 
Lole G,

Sijui una maana gani unaposema hizo technology. Kwenye ujenzi wa barabara, Traffic Engineers mara nyingi hulazimisha madereva wafuate nini wao wanakitaka. Hii hutokana na pesa kidogo iliyopo katika ujenzi wa hiyo barabara. Pia acha kujenga, inabidi iwepo pesa ya kuitunza hiyo barabara kwa kukata miti na nyasi za pembeni mwa barabara, kuziba mashimo, kutunza alama za barabarani au kuweka mpya pale inapobidi nk.
Traffic Engineer wana sheria na utaratibu wao wa kufanya hivyo na wakati mwingine mtu wa kawaida unaweza kuona ni kituko. Ila ndivyo lilivyo hilo somo. Sasa wakishamaliza kazi yao, na hawa ndiyo huwa watu wa mwisho kumalizia kazi kwa kuweka alama za barabarani, barabara hukabidhiwa na kuanza kutumiwa. Sasa nini kitafuata baada ya hapo, hiyo huwa ni kazi ya Traffic (POLISI). Dawa kubwa ya kupunguza rushwa ni kuweka magari yaliyo na camera ndani na hizo camera zimeungwa na mtandao wa internet kwenye vituo vya mkoa au POLICE head office ili mtu baadaye asipokee pesa kwani kila kitu kinakuwa kimerekodiwa. Pesa inayopatikana kwenye faini kwa hawa madereva wazembe, inatosha kabisa kununua magari mengine na camera zaidi, yaani kutokana na uzembe wa madereva wengi wa tz, haya magari kwa siku yangelikuwa yanaingiza hata dola 2,000 au zaidi per car. Faini haitakiwi ziwe za kuuwana sana ila ziwe zinatolewa kulingana na kufanya makosa ya kizembe na zaidi ni kwa wale wanaozidisha speed au ku-overtake sehemu zisizotakiwa kufanya hivyo.

Kwa teknologia ya jinsi ya kuzitumia barabara zetu nakubaliana na wewe mkuu kwa 100%.
Bila kutumia technologia ambayo sasa mainjinia wengi tu watanzania wanaweza kuitumia na kuiendesha kupitia TANROADS ,POLISI n.k. itakuwa vigumu sana kuongoza uendeshaji wa magari barabarani, hasa kwenye hizi highways kubwa.Hata hivyo kuna matizo.
Tatizo la kwanza ambalo halina budi kutatuliwa ni KUITUMIA technologia kama uliyoilezea na kuweza kufanya maintainance ya mara kwa mara.Sasa hivi zile speed radar za polisi mikoani karibu zote zimejaa to capacity na wao wala hawajui kuzi reset.Mitambo ya camera uliyo i propose ni muafaka ila wasi wasi wangu ni maintainance.
Vile vile mainjinia wajenzi wa barabara wanaweza kutengeneza barabara zile zenye inbuilt speed barrriers .Speed bumbs ni moja wapo ingawaje hazipendwi sana.
Tatizo la pili ni hilo la fines au ticketing.Ingewezekana hii ticketing ingefanywa bila kuwa na mwingiliano wa binadamu moja kwa moja tatizo lingepungua.The weak link hapo ni "ubinadamu" wa polisi wetu kwa kuachia makosa au kuchukua rushwa baada ya kumkamata dereva mhalifu anayekwenda kwa mwendo kasi.Ni kweli nchi za wenzetu traffic offences zina fine kali sana kiasi cha mtu kuacha kabisa kazi ya udereva au kuuza gari lake kwa kufungiwa kisheria.
Tukiweza kutatua hayo, ambayo yamo katika uwezo wetu tutakuwa tumepunguza ingalau kifo kimoja cha zaidi.
 
Wakubwa kiti kuonyesha kua mtu alikua amesinzia ni technologia gani iyo?
Hata kama mchunguzi kasomea Uingereza, ni kwa nini tusiseme Mwakyembe alikua kalala make kuna tofauti kati ya kulala na kusinzia.
Mtu anaweza kulaza kiti ili alale ila akawa ajasinzia.
Mchunguzi wetu aliyesomea Uingereza ametofautishaje kulala na kulala usingizi alipoangalia kiti?
 
Chenge kasoma Havard if am not mistaken, but alikuwa anaendesha gari bila BIMA for almost two years,achilia mbali mikataba feki kibao aliyoshiriki akiwa AG!! kusoma Uingereza is not a big deal, after all mtaalam mwenyewe anaweza kuwa kati ya watoto wa vigogo ambao ni vilaza tu, wanapelekwa nje kupata vyeti na kupanda vyeo...
 
Wakubwa kiti kuonyesha kua mtu alikua amesinzia ni technologia gani iyo?
Hata kama mchunguzi kasomea Uingereza, ni kwa nini tusiseme Mwakyembe alikua kalala make kuna tofauti kati ya kulala na kusinzia.
Mtu anaweza kulaza kiti ili alale ila akawa ajasinzia.
Mchunguzi wetu aliyesomea Uingereza ametofautishaje kulala na kulala usingizi alipoangalia kiti?
Kiti alichokalia Mh. kilikuwa kimelazwa, hii inaonyesha kuwa alikuwa ameuchapa usingizi wakati wa ajali. Iwapo kiti hicho kingekuwa katika hali ya kawaida, basi Mh. angepata madhara makubwa zaidi. Huu ndio uchunguzi uliofanywa na mtaalumu aliyesomea Uingereza.
 
labda dereva wa lori ajitokeze na kueleza upande wake
wa hali ilivyokuwa.
Hatujasikia driver wa lorry akijieleza though inasemekana alipatikana.
-Gari lake halikua na mzigo ndio maana aliendesha kwa speed.
-Gari lake lilikua na tinted glass, inaruhusiwa hiyo??????
-Kwa nini baada yakusababisha ajali hakusimama????????????
-Watu waliyokua kwenye ajali walieleza kilicotokea kwanini polisi wanataka maelezo tofauti na yao??
 
Mkuu, hii ni biashara ya kuandika kumbukumbu kwa mate badala ya wino! Waliohusika na kushuhudia ajali hiyo ikitokea wameongea. Sisi ambao hatukuwepo, tunaporomosha kila aina ya theory ku-contradict ushahidi wao. Kazi ya Polisi ni kuu-test ushahidi wa Dk. Mwakyembe na Dereva wake mahakamani na si vinginevyo! Huo ndo utawala wa sheria!

Polisi wakiendelea kukaidi kulitafuta lori hilo kwa sababu za kibinafsi au za kisiasa, watakuwa wanapoteza fedha za Jamhuri na muda kuendelea na kesi hii. Itakuwa sawa na kuendesha kesi ya KAGODA bila kumhoji ROSTAM AZIZ; kesi ya RADA bila kumhoji CHENGE, IDRISSA na SOMAIA; kesi ya RICHMOND/DOWANS bila kumhoji LOWASSA, ROSTAM na MSABAHA; kesi ya Kiwira Coal Mine bila kumhoji MKAPA na YONA; kesi ya helikopta za jeshi bila kumhoji SOMAIA; kesi ya majengo ya NSSF bila kumhoji MANJI; kesi ya mabilioni ya IMPORT SUPPORT bila kumhoji ROSTAM; kesi ya Liganga na Mchuchuma bila kumhoji SHUBASH PATEL na KARAMAGI n.k.!
Hapo umesema niko nyuma yako
 
Kiti alichokalia Mh. kilikuwa kimelazwa, hii inaonyesha kuwa alikuwa ameuchapa usingizi wakati wa ajali. Iwapo kiti hicho kingekuwa katika hali ya kawaida, basi Mh. angepata madhara makubwa zaidi. Huu ndio uchunguzi uliofanywa na mtaalumu aliyesomea Uingereza.

Jee Dr. amesemaje kuhusu taarifa hiyo? Kwanza kuuchapa usingizi ambalo ni jambo la kawaida ukiwa katika safari ndefu na dereva wako unamwamini. Pili hakuna alama yeyote inayoonyesha kuwa gari lake liligongwa na lori hilo. Tatu mashuhuda walioona gari lake likiswing left and right kabla ya shimo, hasa ile coster iliyowapisha. Nne utata wa overspeeding, driver akisema 120kph wakati Dr. akisema 140kph.? Tano kuona kama driver wa lorry alitengeneza ajali hiyo wakati yeye kiti chake kilikuwa flat down.

Ni vizuri tukayajua hayo kabla hatujawabana Polisi..
 
nakubaliana na wewe
120 -130 km/hr ni sawa na 90miles/hr
hiyo speed hata kwa lori huku ulaya ni kubwa sana na malori ya tz ni mazee sana
pili kama dereva wa lori alikuwa 130 siwezi kuamini kama alikuwa anamchelewesha dr mwakyembe...
kwa hiyo inamaanisha hilo lori lilikuwa mwendo wa konokono..

kwa barabara za tz gari likikupita hata likiwa 90km/h kwa ajili ya udogo wa barabara unaweza ukazani liko 200km/h

Jamani tuongee ukweli na sio nadharia. hiyo speed ya 120Km/hr malori yetu yanafika na mimi nimeshuhudia. Niliendesha gari dogo kwenda Mbeya una-overtake lori kwa speed 140km/hr na watu wakumbuke kuwa kuna malori mpya ya makampuni ya nje yanapita njia hiyo kwa hiyo suala lakusema kuwa malori hapa bongo hayafiki 120km/hr sio kweli. Hapo juu mtu amezungumzia kuwa upepo unakuwa mkali na udogo wa barabara kwa kkweli sio sawa kwani ni barabara hizi hizi tuna kwenda hadi 150km/hr tuna-overtake mabasi malori na magari madogo na mashimo pia.
 
Jee Dr. amesemaje kuhusu taarifa hiyo? Kwanza kuuchapa usingizi ambalo ni jambo la kawaida ukiwa katika safari ndefu na dereva wako unamwamini. Pili hakuna alama yeyote inayoonyesha kuwa gari lake liligongwa na lori hilo. Tatu mashuhuda walioona gari lake likiswing left and right kabla ya shimo, hasa ile coster iliyowapisha. Nne utata wa overspeeding, driver akisema 120kph wakati Dr. akisema 140kph.? Tano kuona kama driver wa lorry alitengeneza ajali hiyo wakati yeye kiti chake kilikuwa flat down.

Ni vizuri tukayajua hayo kabla hatujawabana Polisi..
Hiyo Taarifa haikumuoji Mh. wala Dereva wake.
 
Kulingana na report ni kwamba Mwakyembe na dereva wake wamedanganya. Hivi kulikuwa na haja gani ya kudanganya?

Imeamuliwa dereva wake akamatwe mara moja na kushitakiwa. Soma taarifa zaidi gazeti la Tanzania Daima la leo.

Unajua ukizoea kuishi kiusanii unakuja naswa kwenye tundu bovu. Kyela watu wanacheka tu na hawashangai maana wanamjua mbunge wao.

Alitaka kutumia ajali hii ili aonewe huruma kisiasa wakati makosa yote yalikuwa ya dereva wake.

Wapambe kazi mnayo, sijui mtasema mafisadi wamewahonga polisi?
 
Taarifa sahihi ni hii:

1. Mwakyembe na dereva wake ndio chanzo cha ajali, ajali haichagui, uwe mbunge, muuza karanga au waziri.
2. Taarifa ya polisi inawezekana kabisa kuwa haikuwa ya kweli wka sababu zifuatazo.
(a) ndio siku zote wako hivyo na haiwezekani wawe makini kwa sababu eti mwakyembe kapata ajali
(b) kuna uwezekano mkubwa kuwa, walichanganyikiwa na ajali ya Mwakyembe na wakasahau hatua muhimu za kuchukua, wakabaki kutaka kuokoa maisha ya Mwakyembe

3. Kama kuna mtu alipanga jali hii, basi ana akili sana, YAANI ALIINGIA KICHWANI MWA MWAKYEMBE NA KUMWAMBIA DEREVA WAKE AOVATEKI LORI kwa speed 140! halafu wagongwe, mpangaji ajali hii lazima sio mwanadamu wa kaiwada!

4. Ni wakati mzuri wa Mwakyembe na viongozi wengine kujua kuwa hakuna sensor kwenye vyombo vya moto inayotofutisha kati ya waziri, mpiganaji wa mafisadi na rais, wote sawa tu.

5.Hivi nani amuue Mwakyembe?? CHADEMA?? maana Chadema kupita kwenye jimbo la mwakyembe wasahau! labda afe LAKINI KUSEMA ETI MAFISADI NANI?? WANAGOMBANA KWENYE VYOMBO VYA HABARI JIONI WANAGONGA GLASS, CHAMA KIMOJA, NGUVU MOJA, KUNA FISADI KAENDA JELA KWA SABABU YA MWAKYEMBE ?-HAPANA, NANI WA KUMUUA MWAKYEMBE?? AU TUMEZOEA TU KILA AJALI IMEPANGWA??

KWA CCM, uhai wa Mwakyembe ni mali na muhimu sana kwao, unafikiri huko Busanda au magogoni angesisamishwa Mwakyembe kupiga kampeni kwa mgombea wa CCM kuna mtu angeenda kinyume?? kasimama Rostam watu wameshinda, je Mwakyembe?? au atagoma wakati ni mwana-CCM??

Mwakyembe atakuwa threat tu na kuwa katika hali ya kuuawa kama akihama CCM wakiwa ndani ya CCM (ni watu wa kuuzwa ili chama kishinde) haijalishi kuna mafisadi au wasafi-Kalagabhao!!

Kwanza nikiri kwamba nimebanwa na majukumu mengi kiasi cha kuzidiwa na kasi ya JF, hivyo kama nitakuwa nimerudia ama nimehoji maswali ambayo yamekwisha kujibiwa, natanguliza kunradhi kwa nitakaowakwaza.

Kwa ufupi nina masahihisho na maswali kadhaa.

1-Kwanza sidhani kama kuna mahali Mwakyembe amesema kwamba kuna mtu aliyepanga ajali, bali kwa kuwa anamuamini dereva wake na alishuhudia ajali angalao ilipoanza na hata ilipoishia akiwa taabani, aliona angalao kwamba lile lori ndilo lilisababisha dereva aache njia kwa sababu mbalimbali.

2-Kuhusu kiti kukutwa kimelala, hata kama alilala kitendo cha gari kuyumba angeshituka na kuangalia kinachotokea, lakini jamani kiti kulala ndio yeye kulala? Leo nikiwa safari ndefu nilikuwa naongea na simu na mtu akijadili hiyo hiyo ajali ya Mwakyembe na nilicheka sana, maana nilikuwa nimelaza kiti wakati naongea na hiyo simu tena nikiangalia eneo tulipofika. Sikuwa nimelala.

3-Lakini maswali yangu yanakwenda kwa Tanzania Daima.
Ilianzia kwa Jumapili iliyopita na baadaye gazeti la Jumanne hii kuandika taarifa kuhusu "utata" wa ajali hiyo. Awali walinukuu taarifa za dereva wa lori na trafiki mmoja alkiyekuwa katika basi dogo linalotajwa tajwa. Katika maelezo hayo ilionekana kama dereva amejitokeza na kuhojiwa. Taarifa zinasema polisi hawajafanikiwa kumpata dereva huyo wa lori (wamenukuu Tanzania Daima).

Hata hivyo dereva huyo anasemekana ndiye aliyepiga simu kwa namba isiyoonekana kupeleka taarifa hiyo gazetini!! Walimuamini vipi? dereva huyo hajapatikana kwa mwajiri wake!! Amesafiri na simu yake haipatikani!! Lakini kabla ya kumpata, kwa kasi ya ajabu, timu ya polisi ikiwa Iringa, imekamilisha kazi ya siku moja na kutoa taarifa kwamba Mwakyembe amesema uongo na dereva wake akamatwe kwa kusababisha ajali!! dereva wa lori hajahojiwa, dereva wa Mwakyembe aliandika maeelzo Iringa, Mwakyembe aliandika maelezo Dar es salaam, na maelezo yao hayajaaminiwa ila wameaminiwa "Mashuhuda wa ajali" ambao walisubiri hadi kina James Kombe wafike!!!

Maoni yangu ni kwamba, kulikuwa na haraka gani polisi kutoa taarifa kabla ya kupata maelezo ya pande zote husika na kuyachuja? Hivi polisi hawakuwahoji mashuhuda pale pale siku ile ile mpaka timu ya IGP ifike?

Hivi kama kulikuwa na mpango wa ajali hiyo, unaweza kweli kuthibitishwa kwa siku moja? Je, kama dereva wa Mwakyembe alihusika? Je, kama kuna fundi aliyelitengeneza akalichezea? Je, kama walipaki mahali mtu akategua lock mkono wa gurudumu? Hivi kweli uchunguzi wa ajali ya kiongozi hufanywa haraka haraka tu?

Ajali ya Salome Mbatia kulikuwa na tume na ilichukua muda gani? Ajali ya Wangwe kulikuwa na timu na ilichukua muda gani? Ajali ya SOkoine tume ilkuwapo na ilichukua muda gani? Ajali nyingi za mabasi zilizoua mamia ya Watanzania wenzetu ziliundiwa tume? KULIKONI? Tusitengeneza hadithi halafu tukatengeneza majibu, halafu tukayapotosha halafu tukayaundia tume tutakayakanusha tuliyoyapotosha wenyewe!!!
 
Halisi,
Unajua watu wengine jamani hata hawana hoja waache kama walivyo.. sasa Mwakyembe akiwa hakulala, ndio kusema ajali isingetokea?.. swala ni nani mkosefu ktk ajali ile.. sababu ya ajali na sio hali ya victims wa ajali ile..hawa watu vipi mkuu wangu.
Mwakyembe hakuwa anaendesha gari..Na sisi sote humu hulala usingizi tukiwa safarini iwe bus ndege au gari ndogo maadam hatuendeshi ni ruksa mtu kujipumzisha..lakini haiwezi kuchukuliwa kulala kwetu kuwe sababu ya makosa ya ajali au maumivu yatokanayo!
Kitendo cha kupona au kufa hakina kulala wala kuwa macho, hapa hatuzungumzii hali yake, mbona huyo dereva aliyekuwa akiendesha na macho ndiye kaumia zaidi!.. naye alitakiwa afanye nini zaidi ili asiumie hivyo alivyoumia!..
jamani watu kaa hawana la kuandika basi acheni wengine wenye dataz watumwagie hizi habari za kulala zinahusu kitu gani!.. Je ndio kusema mwakyembe alosema aliyaona hakuyaona na Uongo kwa sababu alikuwa amelala usingizi?..thenm what is the truth kama mnao.. Huyo mchunguzi lazima aje na sinerio yake ya ajali kuwa mnene wa mwili wa Mwakyembe na kulala kwake kulilifanya gari liyumbe na kutoka barabarani au?..
 
Hiyo Taarifa haikumuoji Mh. wala Dereva wake.

Interesting, kama kweli tume husika ilitoa findings zake bila kuwahoji Dr. Mwakyembe na dereva wake, then itakuwa imefanya makosa yale yale aliyoyafanya Dr. ya kumhukumu Lowassa bila kumuhoji.

Hata hivyo hilo halimkatazi Dr. kuijubu taarifa hiyo kimaandishi na kuweka wazi kasoro zilizomo katika repoti hiyo na ikiwezekana Polisi iwe taken to task for coverup.
 
Nimejizuia kuhoji hii ajali, na ninaendelea kujizuia maana nitaitwa namtetea mwakyembe tena. We have been here before and we gonna be here again until tutake majibu kwa maswali sahihi. Otherwise, kubalini tu mapenzi ya Mungu na dereva atiwe ndani. Msichunguze sana hamtamla.
 
Back
Top Bottom