Nashukuru kwa ushauri wa bure,lakini soma tafadhali submission yangu ya awali.
NIMEONA basi zinazokwenda spidi hizo, hii ni baada kwa utundu tu kulifukuzia basi hilo nikiwa naundesha gari dogo jingine., na nilishangaa.
Pita barabara hiyo na utajionea vioja.
Polisi wanapewa mshiko na ni mwendo wa kasi kama kawa!!
Na ndio maana mabasi ya Mbeya yakipata ajali watu wanaokufa ni wengi sana.
Tatizo kubwa hapa ni technologia.
Haya mabasi, hata magari mengi ya kisasa ni very powerful ukilinganisha na mzigo unaobebwa.Hivyo basi huwa ni mepesi barabarani
Barabara zetu hazija catch up na technologia hii ya magari ya kisasa.Pengine barabara yenye technologia inayo karibia ubora wa magari yetu ya sasa ni barabara kati ya Chalinze na Morogoro.
Na ndio maana hapo awali ndugu engineer kama yuko katika vyombo vya miuondo mbinu nimemshauri kuwa ni vyema studies zika fanyika ili kusaidia kuondoa kutowiana kati ya uwezo wa magari na barabara zetu(traffic studies).
Lazima tuondokane na dhana kuwa uendeshaji wa magari barabarani iwe hisani ya madereva,lazima technology i control dhana hii.
Mkuu Lole,
Siku nyingi usije ukaja fanya utundu wa kulifuata gari linalokimbia, wewe ndio utakuwa wa kwanza kupata madhara.
Unataka technology gani ya barabara kukabiliana na hao madereva?
Je barabara ya Chalinze na Morogoro ina nini ambacho kinaweza kuzuia magari yasikimbie?
Dawa ni moja tu, ni kuandama mifuko ya madereva pamoja na wenye magari. Mkuu nakuhakikishia, ningelikuwa na kazi kama ya Masha, miaka miwili hizo ajali zingelipungua kwa asilimia kubwa sana. Sijipigii debe kwi kwi kwi!!! Lakini ndio ukweli wenyewe. Studies zote zimeonyesha binadamu wengi wako tayari kuchukua risks mbalimbali mpaka pale wanapoona mifuko yao itakuwa matatizoni. Kama ni technology basi itumike kukamata hao culprits ili wawajibike.
Iweje kila siku tunaongelea jambo moja kama vichaa bila kupata jawabu lake. Kwa Tanzania sioni barabara yoyote ya maderva kwenda speed zaidi ya 120kms/h.
Kama serikali inashindwa basi iwe tayari kutumia private companies kukamata hao culprits na mapato yao yatokane na asilimia ya pesa zinazopatikana. Pia serikali irahisishe sheria ili watu wanaodhurika na hizo ajali iwe rahisi kuwafungulia mashitaka wamiliki wa magari hayo. Uwajibikaji usiishie kwa dereva na uende mpaka kwenye mwenye gari.
Wakati mwingine mabadiliko yanakuja kwa manguvu.