Ajali ya Dr. Mwakyembe na yatokanayo

Ajali ya Dr. Mwakyembe na yatokanayo

ku entertain wazo ni haki ya mtu yeyote.
Hata ulevi, na hata uasherati kama hujaoa, ni haki ya mtu yeyoto yule. Je kila haki ni responsible kui exercise?

Hoja ya Halisi ni kuwa hakuna mahali popote ambapo Mwakyembe alisema (kudai factually) kuwa kuna mtu alipanga ajali hiyo.
Hiyo ni hoja ya Halisi. Ya kwangu ni kwamba Mwakyembe ametumia hiyo ``haki`` kuropoka vitu irresponsibly.

... nukuu yako umeacha the preceding conditional clause na kuweka maneno ambayo yanadai kana kwamba ni ukweli. Huku ni kujaribu kumfanya mtu aseme kitu ambacho hakukisema. Wakati mwingine nukuu kauli nzima kama ulivyoona...
Alichokisema ndicho nimenukuu neno kwa neno. Na unajua fika ndivyo alivyoongea akiwa hospitali.
Kusema "alientertain wazo" halijibu swali kwani wengi tuna entertain mawazo ya ajabu sana!! Ndiyo maana tunaitwa wanadamu.
Ku entertain mawazo mabaya pia ni kubaya. Larry Summers alifukuzwa Ukuu Harvard kwa kuitisha kongamano kujadili, kuwaza tu, kama wanawake hawawezi hesabu kimaumbile. Akaambiwa ame entertain mawazo potofu.

Mwakyembe hakutakiwa ku entertain na kuropoka nadharia za njama, ni irresponsible. Alichokisema kinatisha:

Mh. Mwakyembe:

``...Mimi ni Mkisto, nimemuachia Mungu hayo, nimesema Mungu kama hiyo, kilichotokea leo, ni binadamu alikipanga basi namshitakia yeye, na kama kilichotokea ni ajali, basi tumuachie Mungu. Lakini kama kilichotekia kilipangawa basi huyo aliyepangwa kufanya hivyo ni mtaalam wa hali ya juu sana maana jinsi alivyoigonga ile gari, kupoteza mwelekeo, mimi kwa kweli nimeiona hiyo, hayo matukio, kwenye sinema tu.``
 
Hata ulevi, na hata uasherati kama hujaoa, ni haki ya mtu yeyoto yule. Je kila haki ni responsible kui exercise?

Kama ni haki kwanini isiwe ni responsible kuiexercise?

Hiyo ni hoja ya Halisi. Ya kwangu ni kwamba Mwakyembe ametumia hiyo ``haki`` kuropoka vitu irresponsibly.

Hapana umenukuu swali la Halisi na kujaribu kulijibu kitu ambacho hakikuulizwa. Haikuwa hoja.

Alichokisema ndicho nimenukuu neno kwa neno. Na unajua fika ndivyo alivyoongea akiwa hospitali.

Ndiyo.. lakini msisitizo wako haukuwa kwenye condition ya maneno yake.

Ku entertain mawazo mabaya pia ni kubaya. Larry Summers alifukuzwa Ukuu Harvard kwa kuitisha kongamano kujadili, kuwaza tu, kama wanawake hawawezi hesabu kimaumbile. Akaambiwa ame entertain mawazo potofu.

Si kweli. Yeye alipoproose idea fulani siyo kuintertain. Kasome vizuri.

Mwakyembe hakutakiwa ku entertain na kuropoka nadharia za njama, ni irresponsible. Alichokisema kinatisha:

You missed the point.. ukisome alikuwa anaonesha jinsi gani wazo zima la kuwa ni conspiracy ni far fetched ndiyo maana kasema mambo kama hayo anayoana kwenye filamu. I'm suprised you missed that too.
 
Kama ni haki kwanini isiwe ni responsible kuiexercise?

Kwa sababu haki zina majukumu yake. Haki ya kunywa pombe ina majukumu ya kunywa responsibly. Haki ya kuongea nayo ikitumiwa vibaya ndio hapo Mwakyembe anajiropokea ma nadharia ya njama irresponsibly.

Hapana umenukuu swali la Halisi na kujaribu kulijibu kitu ambacho hakikuulizwa. Haikuwa hoja.
Haikuwa hoja? Wewe ndio ulisema ``Hoja ya halisi ni...`` Nikakwambia, na mimi hoja yangu ni Mwakyembe ame entertain mawazo potofu.

Ndiyo.. lakini msisitizo wako haukuwa kwenye condition ya maneno yake.
Mwanzo ulisema sikunukuu kila kitu, sasa umebailika unasema tatizo ni msisitizo ulipowekwa. Which is which?

Si kweli. Yeye alipoproose idea fulani siyo kuintertain. Kasome vizuri.
Right, ali propose kwamba aidha ni ajali, au ilipangwa. Ame entertain kwamba ilipangwa.
You missed the point.. ukisome alikuwa anaonesha jinsi gani wazo zima la kuwa ni conspiracy ni far fetched ndiyo maana kasema mambo kama hayo anayoana kwenye filamu.
I am missing the point? I missing the point because you are making it up. Yeye hakusema kwamba ni idea ``far fetched.`` Ame entertain hadithi za njama ya ajali ilipangwa ``mtaalam wa hali ya juu sana.``

Mh. Mwakyembe:

``...Mimi ni Mkisto, nimemuachia Mungu hayo, nimesema Mungu kama hiyo, kilichotokea leo, ni binadamu alikipanga basi namshitakia yeye, na kama kilichotokea ni ajali, basi tumuachie Mungu. Lakini kama kilichotekia kilipangawa basi huyo aliyepangwa kufanya hivyo ni mtaalam wa hali ya juu sana maana jinsi alivyoigonga ile gari, kupoteza mwelekeo, mimi kwa kweli nimeiona hiyo, hayo matukio, kwenye sinema tu.``
 
Mkandara

Nafikiri umemiss point yangu. Haoj kuwa hakuna professional drivers sio ya kweli. Kila mtu kuwa na uwezo wa kuingia barabarani na kuendesha gari sio makosa ya madereva wa Tanzania bali ni kosa la Serikali hasa idara ya usalama barabarani ambapo leseni za udereva zimegeuzwa kuwa ni mradi wa kibiashara. Watu mabali mbali ikiwemo watoto wasio kuwa na umri unaoruhusiwa kuendesha magari huletewa leseni za udereva majumbani. Hali hii imechangia kwa kiwango kikubwa kushusha hadhi na heshima ya profession ya udereva. Hivyo leo hii katika barabara zetu kuna watu wanaendesha magari lakini hawajui sheria na alam za usalama barabarani na hali hiyo ndio chanzo kikubwa cha ajali za barabarani hapa nchini.

Lakini ukweli utabaki pale pale kuwa daktari akikosea ni maisha ya mgonjwa mmoja ntu huathiri kwa wakati mmoja, lakinui dereva wa basi akifanya makosa ni maisha ya abiria 65 huwa hatarini. Hivyo kama jamii tunataka kupunguza ajali za barabarni tunatakiwa kukemea na kudhibiti vitendo vyote vinvyosababisha fani ya udereva kukumbwa na mafurijko makubwa ya watu wasio na ajira hapa nchini hata kama hawako tayari kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za usaklama barabarani. Hali ilivyo sasa every Tom, Dick and Harry kama hana ajira lakini anaweze kujipatia leseni ya udereva kwa kununua na hivyo kuingia barabarni.
 
Kitu kikubwa kwangu, je kuna alama yoyote ya hiyo gari kugongwa kwenye hiyo taa ya nyuma? halafu kama ipo baada ya hapo gari iliangukiwa upande gani wa barabara kushoto au kulia. Kama ni kushuto basi gari la Mwakyembe lilikuwa lina rudi upande wake baada ya ku-overtake au katika jitihada ya ku-overtake, kama liliangukiwa upande wa kulia kuna uezekano ni kutokana na kupigwa push , na uthibitisho itakuwa hiyo impact kwenye taa nyuma ( kama ipo)
 
Gari liliangukia kushoto na lilienda mbele ya pale ambapo inasemekana ndipo liligongewa.

Kama nilivyoandika mwanzoni physics inakataa. Ukiligonga hilo gari taa ya kushoto na likaenda mbele basi peleka hiyo theory mbele unaweza kupata nobel prize ya physics. Hilo gari lingeenda mbele kama tu lingegongwa katikati.

Jaribu hata kuchezea toy nyumbani na igonge hapo wanaposema iligongwa, hiyo toi itageuka nyuma. Kwa maana hiyo ni kwamba ingelikuwa hatari zaidi maana ingegeuka na kugongwa vibaya kwa mara ya pili.

Tatizo la TZ waganga wa mvua wako kibao na untested theories zao, wanachosahau hizi ajali zote zinatokea miaka na miaka na kuna theories juu ya nini kitegemewe kwenye ajali fulani.

Hizo barabara hazina alama nzuri za barabarani lakini mwendo unaoruhusiwa vibao vipo ndio maana mimi niliandika toka mwanzoni kwamba hiyo barabara maximum speed ni 80km/h. Tatizo madereva wengi wa Tanzania hawaangalii kabisa hizo alama za barabarani.

Tunaongoza kwa risk taking, ingelikuwa tunafanya hivyo kwenye mambo ya kiuchumi nafikiri tungelikuwa na matajiri wengi sana, bahati mbaya sisi tunafanya kwenye magonjwa na barabarani.
 
Tu-assume gari ya mwakyembe ilikua zaidi ya 80km/h. Swali kama barabara inamichora ya kuruhusu ku overtake, ikiwa dereva wa lori alimruhusu kuovertake huku akiwa na spidi ya 80km/h, Je drereva wa Mwakyembe angetumia spidi gani chini ya 80km/h kuovertake???????
 
Mkuu Ikena,

Hivi wewe ni dereva?

Hata kama sehemu inaruhusu ku overtake; hataka dereva wa gari mbele yako akuruhusu kupita; hutakiwi kufanya hivyo kwa speed ambayo ni zaidi ya maximum speed kwa sehemu husika.

Kama Lori lilikuwa linaenda 80kms/h, jibu ni kwamba kisheria dereva wa Mwakyembe hakutakiwa kulipita hilo lori na ingebidi waongozane na lori mpaka pale ambapo lori lingepunguza mwendo.

Ku overtake unaongeza speed lakini lazima hiyo speed yako mpya isizidi maximum speed ya barabara husika. Kama wewe una overtake kwa speed kubwa kuliko allowed speed, unavunja sheria na inatakiwa uchukuliwe hatua.

Nenda hata usalama barabarani watakuambia hivyo hivyo.
 
Gari liliangukia kushoto na lilienda mbele ya pale ambapo inasemekana ndipo liligongewa.

Kama nilivyoandika mwanzoni physics inakataa. Ukiligonga hilo gari taa ya kushoto na likaenda mbele basi peleka hiyo theory mbele unaweza kupata nobel price ya physics. Hilo gari lingeenda mbele kama tu lingegongwa katikati.

Jaribu hata kuchezea toy nyumbani na igonge hapo wanaposema iligongwa, hiyo toi itageuka nyuma. Kwa maana hiyo ni kwamba ingelikuwa hatari zaidi maana ingegeuka na kugongwa vibaya kwa mara ya pili.

Tatizo la TZ waganga wa mvua wako kibao na untested theories zao, wanachosahau hizi ajali zote zinatokea miaka na miaka na kuna theories juu ya nini kitegemewe kwenye ajali fulani.

Hizo barabara hazina alama nzuri za barabarani lakini mwendo unaoruhusiwa vibao vipo ndio maana mimi niliandika toka mwanzoni kwamba hiyo barabara maximum speed ni 80km/h. Tatizo madereva wengi wa Tanzania hawaangalii kabisa hizo alama za barabarani.

Tunaongoza kwa risk taking, ingelikuwa tunafanya hivyo kwenye mambo ya kiuchumi nafikiri tungelikuwa na matajiri wengi sana, bahati mbaya sisi tunafanya kwenye magonjwa na barabarani.
kama liliangukia kushoto , kuna uwezekano mkubwa wa dereva wa mwakyembe kuwa na makosa, lakini ina kuja suala laustaarabu wa barabarani , sasa sijui kama ni sheria au vipi kwamba unapoona gari linalo kuja nyuma yako lina mwendo mkali na lina nia ya kukupita, na hakuna kizuizi cha wewe kulizui lisikupite mfano hakuna gari linakuja mbele yako au ni sehemu ya mlima au kona , basi ni vizuri ukaliruhusu lipite.
 
August,

Nakubaliana na wewe, huyo dereva wa lori alitakiwa alipishe gari la mheshimiwa hasa alipoona wanataka kupita kwa nguvu zote. Dereva yeyote mstaarabu ataamua kuwapisha hata kama wanaenda mwendo ambao si salama. Kwa kujaribu kuwazuia unaweza kusababisha ajali hata mbaya zaidi.

Ila kwa TZ ya umwamba umwamba, sishangai nikiona watu wanakosa ustaarabu kabisa wanapokuwa barabarani.
 
....unapoona gari linalo kuja nyuma yako lina mwendo mkali na lina nia ya kukupita, na hakuna kizuizi cha wewe kulizui lisikupite mfano hakuna gari linakuja mbele yako au ni sehemu ya mlima au kona , basi ni vizuri ukaliruhusu lipite.

August,

Nakubaliana na wewe, huyo dereva wa lori alitakiwa alipishe gari la mheshimiwa...

...Dereva yeyote mstaarabu ataamua kuwapisha hata kama wanaenda mwendo ambao si salama ......Ila ...watu wanakosa ustaarabu kabisa wanapokuwa barabarani.

Wakuu August na Mtanzania, hebu tusaidiane kuelewa huo "ustaarabu" wa hicho kitu mnachosema "kupisha."

Nikiwa mbele yako, naendesha 18 wheeler upande wangu wa barabara, mwendo 80km/saa. Eneo hilo, kikomo cha mwendokasi ni 80km/saa. Wewe uko nyuma, unawasha mataa na kupiga mahoni, unataka "nikupishe."

Maana yake nini "nikupishe"? Natakiwa ni pull over nikasimame au niongeze mwendo, au natakiwa nifanye nini?

Nikupishe niende wapi?
 
Mkuu Dilunga,

Wengine tulivyofundishwa kuendesha gari ni kwamba ukiona mtu nyuma yako anafanya vituko, ikiwezekana kama ni salama basi hata simama akupite. Hakuna haja ya kushindana kwenye barabara.

Maana ya ustaarabu niliokuwa naongelea ni kwamba, huyo dereva wa lori angepunguza mwendo ili huyo aliyekuwa anataka kumpita kwa nguvu zote apite. Hakuna sheria inayolazimisha hivyo ila kwenye ustaarabu wa kuendesha inabidi kufanya hivyo.

Mfano mwingine, unamwona mtu yuko lane ya kwenda upande mwingine ghafla anaonyesha indicator kwenda upande wa kwako. Kama ni dereva mstaarabu na ni salama kufanya hivyo inabidi umpishe, huwezi kujua, si ajabu ni mgeni na amepotea. Of course huko mijini ni unyama unyama, badala ya kukupisha mtu atakutana na tusi.

Muhimu usimfanyie mtu kitendo ambacho usingetaka wewe ufanyiwe na mtu yeyote.
 
Wakuu August na Mtanzania, hebu tusaidiane kuelewa huo "ustaarabu" wa hicho kitu mnachosema "kupisha."

Nikiwa mbele yako, naendesha 18 wheeler upande wangu wa barabara, mwendo 80km/saa. Eneo hilo, kikomo cha mwendokasi ni 80km/saa. Wewe uko nyuma, unawasha mataa na kupiga mahoni, unataka "nikupishe."

Maana yake nini "nikupishe"? Natakiwa ni pull over nikasimame au niongeze mwendo, au natakiwa nifanye nini?

Nikupishe niende wapi?

Kwa bongo ambapo sheria za barabarani ni ku keep left,basi ukitaka kumpisha mwenzako unawasha indicator ya kushoto ama unaaashiria kwa kutoa mkono nje kuwa aliyeko nyuma yako anaweza kupita,na mara nyingi ni pale ambapo yule aliyeko nyuma yako hawezi kuona kama kuna gari linakuja kwa mbele....Na kama kuna gari linakuja kwa mbele,basi mwene gari lililoko mbele atawasha indicator ya kulia ikimaanisha kuwa aliyeko nyuma hawezi kupita,either kwasababu kuna gari inakuja kupishana ama ni kwenye kona ambapo hawezi kuona kama kuna gari inakuja.

Kwa jinsi walivyoleta picha hapo sioni kama kuna sababu yoyote ya dereva wa lori kuwazuia wasipite kwani hakuna kona,sana sana labda aliwazuia kwasababu ya basi/coaster inayosemekana ilikuwa ikija kwa mbele.
Natumaini umeelewa kwenye kuhusu "Kupisha"
 
Nikupishe niende wapi?

Kupisha si lazima uende mahali.
Hata hivyo ni lugha tu, "Kupisha" kwa maana ya "Kuruhusu" Barabara zetu pia zilivyokuwa nyembamba mara nyingine ni kama kupisha kwani lazima ubane upande wa kushoto zaidi ili mwenzako apite kwa urahisi zaidi upande wa kulia.....Kwetu traffic ni "Kupishana pishana" tu...Nadhani ni lugha tu mkuu,huna haja ya kwenda mahali "Ukipisha" ni "Rhuksa" tu.
 
Kumbe kupisha ni ``kuruhusu.``

Akuruhusu, kwani alikuwa amekuzuia kupita?

Ndiyo,ni kuruhusu kwa kutumia indicator ama mkono,ndiyo sawa mkuu..."Kupisha" Na usipopata hizo indications ina maana hujaruhusiwa kupita ama to be more specific kama ukitaka...Huja "Pishwa" ndo taratibu hizo za uendeshaji bongo.
 
Mkuu Dilunga,

...Maana ya ustaarabu niliokuwa naongelea ni kwamba, huyo dereva wa lori angepunguza mwendo ili huyo aliyekuwa anataka kumpita kwa nguvu zote apite.

Kwa hiyo ``kupisha`` hapa unamaanisha kupunguza mwendo.

Ukitaka kulipita gari la mbele maana yake unaweza kukimbia zaidi yake. Kwani lazima apunguze ili wewe upite?
 
Wewe Dilunga na weye umeanza maswali kama ya mzee Mwanakijiji? Acha hizo!
 
Back
Top Bottom