Ajali ya Dr. Mwakyembe na yatokanayo

Ajali ya Dr. Mwakyembe na yatokanayo

Wataalamu wa saikolojia ya utetezi wanasisitiza ukweli(plain truth) huwa ni short, simple and clear, Utetezi wa Dr ulivyo mrefu na maswali mengi yanayothibitisha ubobeaji wake kwenye taaluma ya sheria na uandishi wa kiuandishi wa habari, kunapelekea wenye busara kutilia mashaka na kujiuliza, "kunani?".
 
Hivi Mwakyembea mbona muongo hivi huyu Mbunge? Leo anadai alisema toka awali hii ni ajali, na hiki nini:
wewe hujamuelewa.....
``...Mimi ni Mkisto, nimemuachia Mungu hayo, nimesema Mungu....
hio ndio kauli yake ya kwanza......wewe umerukia kauli yake ya pili
kama hiyo, kilichotokea leo, ni binadamu alikipanga basi namshitakia yeye, na kama kilichotokea ni ajali, basi tumuachie Mungu.
uwe unaelewa mkuu..
 
Wataalamu wa saikolojia ya utetezi wanasisitiza ukweli(plain truth) huwa ni short, simple and clear, Utetezi wa Dr ulivyo mrefu na maswali mengi yanayothibitisha ubobeaji wake kwenye taaluma ya sheria na uandishi wa kiuandishi wa habari, kunapelekea wenye busara kutilia mashaka na kujiuliza, "kunani?".

Pasco, what would have been your version of "...short, simple and clear..."?

Mimi si mtaalamu wa taaluma ya sheria na uandishi wa Dr. Mwakyembe (na saikolojia ya utetezi imenipita kushoto) hivyo nakubali maelezo yake kwa jinsi alivyoyatoa bila kujiuliza "kunani?" kwa sababu moja kuu: Alikuwapo kwenye ajali inayomhusu yeye.
 
Yale yale ya Wafanyabiashara wa madini....sasa naanza kuona sababu ya Mzee mengi kuamua kutumia vyombo vyake kutoa hukumu, vyombo vya dola ni corrupt period. We huwezi kusema vitu kama umechanganyikiwa. Polisi wa bongo bwana: wanaacha kuzuia uhalifu wao ndo wanakuwa wahalifu wenyewe. Naona safari hii wamegongana na kisiki cha mpingo, tunakata watu kama nyinyi msiogopa kusema kweli lakini kwa kuzingatia sheria maana mabwana fulani wangesema Mafisadi Gaidi.
 
Haya madudu ya mapolisi bila shaka yameaagizwa na yule Mkubwa wao Masha -- ambaye ametokea kuwa mtetezi mkubwa sana wa mafisadi. Siku hizi anaonekana kuachana na tabia ya yeye mwenyewe kutoa statement, kutoa vitisho kwa wafanyabiashara n.k. na sasa anafanya shughuli hiyo nyuma ya pazia ya hao wakuu wa polisi.

Matokeo yake ni kwa hao wakuu wa polisi kuonekana kujikanganya hovyo kama vile mahayawani. Mkuu wa kaya anayaona haya lakini ana udhaifu mkubwa kuyakemea kwa sababu zinazoeleweka -- mafisadi walimsimika.

Watanzania tumeuvaa mkenge wa msimamo kweli kweli!
 
Duh, na huyu ni mbunge wao.
Heri Dr. kapona na aweza kujitetea -
masikini wasio na bahati hiyo, listi yao ni kubwa
wote hivi sasa wanapumzikia ahera.
Nawafikiria marehemu akina Wangwe, Kabuye na wengineo.
Kama hawapatikani kwa ajali, sumu ipo -
Nawakumbuka marehemu akina Balali, Amina na wengineo.
Mungu walaze mahali pema peponi.
Mafisadi hawana dogo
 
Haya madudu ya mapolisi bila shaka yameaagizwa na yule Mkubwa wao Masha -- ambaye ametokea kuwa mtetezi mkubwa sana wa mafisadi. Siku hizi anaonekana kuachana na tabia ya yeye mwenyewe kutoa statement, kutoa vitisho kwa wafanyabiashara n.k. na sasa anafanya shughuli hiyo nyuma ya pazia ya hao wakuu wa polisi.

"Matokeo yake ni kwa hao wakuu wa polisi kuonekana kujikanganya hovyo kama vile mahayawani. Mkuu wa kaya anayaona haya lakini ana udhaifu mkubwa kuyakemea kwa sababu zinazoeleweka -- mafisadi walimsimika.

Watanzania tumeuvaa mkenge wa msimamo kweli kweli!"

____________________________

Zak: Umenena. Siku hizi akina Masha, Mkuchika et al wanatembeza tu scripts kwa wale wa chini yao watangaze. Kama ulivyosema wameanza kujificha nyuma ya mapazia kwa kuogopa kuandamwa, na hii ni dalili tosha kwamba wameanza kuogopa -- ku-retreat kutokana na nguvu za umma. Wachache hawawezi kuhimili nguvu za umma.

Mkuchika leo kamtuma yule mtumishi wake wa Maelezo kuitangaza script yake kuhusu kile kinachoitwa marekebisho ya sera ya habari -- lengo la hiyo ni Mzalendo Mengi, kupunguza kasi ya vita dhidi ya ufisadi inayofanywa na vyombo vyake vya habari.

Mimi naona watunge tu sheria ya kuwakamata na kuwatia ndani wote wale wanaonekana kupinga ufisadi -- hapo wataeleweka vyema, kuliko kufanya mambo ya kichinichini.
 
- Shujaa wangu Mwakyembe, achana na haya malumbano lumbano yasiyo na faida,rudi kwenye ku-focus na ishu muhimu za taifa kama zamani ulivyokuwa,

- Hivi nyinyi mlio karibu naye mmegundua kuwa ni muda mrefu sana sasa mafisadi wamemuondoa kwenye focus ya taifa na kumuweka kwenye ulingo wa kuji-defend defend tu all the time kwa muda mrefu sasa, please Mwakyembe next press release au Conf. iwe ya kumkoma nyani waambie likizo imeisha,

- Ninakuombea kwa Mungu upone haraka, lakini please usijibishane tena na mafisadi maana katika miezi sita iliyopita umeruhusu mafisadi kukupangia agenda za kujitetea tetea bila ya ishu muhimu kwa taifa, please wake up DK yanayokutoea sio bahati mbaya wala amri ya Mungu, ni amri ya mafisadi huwa hatupendi ksuema sana, sasa it is about time ukawatandika where it hurts the most kama ulivyofanya bungeni siku ile na kuwakimbiza mafisadi watatu kwa mpigo, that was wasup! Sio hizi blah! blah! na yada! yada!

- Hit them back na ufisadi wao, si kuna mengine hukusema bungeni yamwage sasa unaona faida ya kuwaonea huruma wao hawana huruma hao mafisadi! na sasa hivi you are where they want you to be! yaani on defensive! Wangu ni ushauri wa bure tu!

Mungu Aibariki Tanzania na Akubariki Upone Sasa.

FMES!
 
Si ameingia katika siasa mwenyewe ? Si alitaka uwaziri mkuu huyu baada ya mwandosya kushinda uraisi kama angepata ? Si ndio huyu huyu alimtibua sana kikwete wakati yuko katika mchakato kule dodoma si anajua siasa mchezo mchafu ?
 
Pasco, what would have been your version of "...short, simple and clear..."?

Mimi si mtaalamu wa taaluma ya sheria na uandishi wa Dr. Mwakyembe (na saikolojia ya utetezi imenipita kushoto) hivyo nakubali maelezo yake kwa jinsi alivyoyatoa bila kujiuliza "kunani?" kwa sababu moja kuu: Alikuwapo kwenye ajali inayomhusu yeye.
Ukweli plain truth ni short, simple na clear na direct to the point, kama Masia alivyosulubishwa bila kosa lolote
Hakuwa na maelezo mengi zaidi ya kusema 'wewe wasema'.
Dr ambaye yu mgonjwa, hakuhitaji kujisafisha kwa maelezo yote hayo na kuingia kwenye technicalities
Za kisheria kwa andiko safi la kiuandishi wa habari.
Angetulia tuu kwanza apone ndipo alonge.

Mengi alipowatukana mafisadi papa, kuna wenye busara walimuona ni mjinga fulani, Rostam alipomjibibisha na kumuita fisadi nyangumi, wale wenye busara wanamuona RA ndio mjinga wa wajinga. Jeethu pamoja na ufisadi wake, hajajibu, hajaitisha press conference, hajatoa statement yoyote na hatajibu chochote, huyo ndio wakumuogopa.
Ili Dr alinde heshima yake, hana haja ya kusema saana na andiko refu. Yeye tayari ni mheshimiwa na anaheshimiwa hata akikaa kimya.
 
Si ameingia katika siasa mwenyewe ? Si alitaka uwaziri mkuu huyu baada ya mwandosya kushinda uraisi kama angepata ? Si ndio huyu huyu alimtibua sana kikwete wakati yuko katika mchakato kule dodoma si anajua siasa mchezo mchafu ?

kwahio siasa ya kuuana inayoendeleza serikali ya ccm miaka nenda rudi ni powa au?
 
- Shujaa wangu Mwakyembe, achana na haya malumbano lumbano yasiyo na faida,rudi kwenye ku-focus na ishu muhimu za taifa kama zamani ulivyokuwa,

- Hivi nyinyi mlio karibu naye mmegundua kuwa ni muda mrefu sana sasa mafisadi wamemuondoa kwenye focus ya taifa na kumuweka kwenye ulingo wa kuji-defend defend tu all the time kwa muda mrefu sasa, please Mwakyembe next press release au Conf. iwe ya kumkoma nyani waambie likizo imeisha,

- Ninakuombea kwa Mungu upone haraka, lakini please usijibishane tena na mafisadi maana katika miezi sita iliyopita umeruhusu mafisadi kukupangia agenda za kujitetea tetea bila ya ishu muhimu kwa taifa, please wake up DK yanayokutoea sio bahati mbaya wala amri ya Mungu, ni amri ya mafisadi sasa it is about time ukawatandika where it hurts the most kama ulivyofanya bungeni siku ile na kuwakimbiza mafisadi watatu kwa mpigo, that was wasup! Sio hizi blah! blah! na yada! yada!

- Hit them back na ufisadi wao, si kuna mengine hukusema bungeni yamwage sasa unaona faida ya kuwaonea huruma wao hawana huruma hao mafisadi! na sasa hivi you are where they want you to be! yaani on defensive! Wangu ni ushauri wa bure tu!

Mungu Aibariki Tanzania na Akubariki Upone Sasa.

FMES!

Ninakuunga Mkono. Kile kitendo tu mwakyembe kupona ni ishara tosha kwamba Mungu bado anataka awe hai ili awamalizie mafisadi, na haisadii kuendela kupigizana nao kelele, wewe chapa tu bakora malizia kusukuma hiyo agenda ya usafi.

Anaogopa siasa za kyela sijui siasa za wapi, anasahau kwamba hata akigombea kinondoni anaweza kuuchukua ubunge ki urahisi , kama kule kawe ndio peeupeeee, crebillity tu ndio inkutosha mengine waachie watoto wa mjini.

Nazani kuna watu watamfikishia huu ujumbe,
 
Chenge alipopata ajali dereva (chenge) alipelekwa eneo la tukio na kutoa maelezo au kusaidia uchunguzi wa chanzo cha ajali. Mbona dereva wa Mwakyembe hakupelekwa eneo la ajali??? HII SIO DOUBLE STD KWELI????????????????
 
chenge ndio alikuwa dereva, sasa sijui unamaanisha dereva gani?
 
Chenge alpopata ajali dereva (Chenge) alipelekwa eneo la ajali kutoa maelezo au kusaidia uchunguzi wa ajali. Mbona dereva wa Mwakyembe hajapelekwa eneo la tukio kutoa maelezo???? HII SIO DOUBLE STD KWELI??????????
 
- Hit them back na ufisadi wao, si kuna mengine hukusema bungeni yamwage sasa unaona faida ya kuwaonea huruma wao hawana huruma hao mafisadi! na sasa hivi you are where they want you to be! yaani on defensive!

Hii babu yake Nyani alikuwa anasema " we have them exactly where we want them to be"

Ninachofurahi kwamba JF ni source of intellectual power, ukiangalia alichoandika Dr Mwakyembe kinaonesha kabisa kuwa vijana humu walifanya kazi nzuri sana ya kuichambua ajali na yaliyojili.

Unajua sasa hivi Tanzania inabidi tuangalie alama za nyakati ule utamaduni wa mtu kuwekwa sehemu nyeti kama Kombe bila kufanya uchambuzi yakinifu wa upeo wa mtu ku deal na situation complex umepitwa na wakati. Kuongoza kitengo kinachohitaji public relation kama traffic hivi sasa kunahitaji zaidi ya uzoefu wa muda mrefu. Kunahitajika pia uwezo wa mtu kufiria kabla ya kutenda. Kamati ya IGP imelidhalilisha sana jeshi la polisi na kulishushia hadhi kwa watu makini ilipokuja na statement za kisiasa zaidi ya kitaalam. Ingekuwa kwa wenzetu huyu Kombe sasa hivi angeshaandika barua ya kukaa pembeni saa nyingi.
 
kombe ! umelipwa kiasi gani na rostam ili kupindisha ukweli? roho zetu na ziwe sadaka kwako ewe mwakyembe mpaka umalize vita dhidi ya ufisadi
 
OFISI YA MBUNGE WA JIMBO LA KYELA
Kwa kuwa sheria za nchi zinataka vyombo vya kiutawala vya maamuzi (quasi-judicial bodies) vizingatie kanuni za haki za asili (principles of natural justice), ni nini kiliizuia Kamati hiyo maalum kunihoji mimi na dereva wangu ili kukidhi matakwa ya kanuni za haki za asili na kupata picha iliyo kamilifu zaidi ya ajali hiyo? Laiti mimi na dereva wangu tungelisikilizwa...
Mwakyembe leo alalamikia ``natural justice``? Mwakyembe? Huyu mwalimu wa wanafiki alimhoji Lowassa?
``Mheshimiwa Dk. Mwakyembe ni Mwanasheria, tena Daktari alikuwa anafundisha Chuo Kikuu. Moja ya vitu alivyokuwa anafundisha ni "Natural Justice".

Mheshimiwa Spika, wewe ni Mwanasheria unafahamu suala la Natural Justice. Kwamba Kamati Teule imesikiliza watu wengine wote pamoja na wanaoita minong'ono ya mitaani, wamesafiri mpaka Marekani kutafuta mashahidi, lakini mimi ambaye ni mmoja kati ya watuhumiwa mle hawakunihoji hata siku moja.

Mheshimiwa Spika, nimesimama kueleza masikitiko yangu. Ofisi ya Bunge mpaka ofisini kwangu hata kama wangeniita ningekwenda kwa miguu kama hamna gari na nilikuwa tayari kufanya hivyo.

Hawa ni watu makini sana siwezi kuamini kwamba wanaweza wakafanya oversite kama hiyo. Kulikuwa na shida gani kuja kuniuliza Waziri Mkuu wanasema uliotoa dokezo hili ni sawa sawa kweli?

… Hapa ndipo tunategemea tuwaonyeshe umakini wetu, umahiri wetu katika mambo ya demokrasia. Kwa nhiyo nilichofanyiwa napenda kuweka kumbukumbu sawa kwamba naona si sahihi, nimefadhaika sana, nimedhalilishwa sana, nimeonewa sana katika hili.

Maana zimechukuliwa tuhuma zikaelezwa hapa kwamba hivi ndivyo ilivyo. Mimi sijaulizwa. Kulikuwa na shida gani kuniuliza, kwa nini muamini minong'ono ya mitaani kuliko maelezo yangu. …Hatuwezi, Tume imepewa muda wa kutosha lakini inashindwa kumuona mtu ambaye wanamtuhumu...``
 
Last edited:
watu kama lowasa hawahitaji kuhojiwa na kupewa haki ya kusikilizwa kwa kuwa ni madikteta na wanaweza hata wakaigeuza forum ya wanaowahoji kuwa butcher
 
Back
Top Bottom