Ajali ya Dr. Mwakyembe na yatokanayo

Ajali ya Dr. Mwakyembe na yatokanayo

Mkuu FMES, you are more than right! Lakini tatizo hapa si Dk. Mwakyembe: ni mimi, wewe na wao. Tunakaa kimya as spectators tukiacha watu wazuri wakipigwa below the belt. Hatusimami kutetea haki. What do we expect from our ill-informed public? Tunaponyamaza wananchi wanaamini udaku unaosambazwa na hawa mafisadi! Hivyo akina Mwakyembe wanalazimika from time to time to stand up and fend for themselves! Hii Bongo bwana, bla bla bla za solidarity nyingi, lakini vitendo sifuri!

- Mkuu wangu heshima mbele sana, nimekusikia sana record yangu iko very clear na kusimamia viongozi ninaowaminia, DK ninamuaminia sana ndio maana hata alipokuwa na matatizo majuzi nilijipiga na kumtumia kidogo na kichache nilichokuwa nacho, ni kwa sababu ya kuheshimu mchango wake kwa taifa,

- Pamoja na uchache wake wa hapa na pale kiuongozi, bado ninamuaminia sana, ila tu tatizo siwezi kuwaongelea wengine humu, maneno yako ni kweli sana wananchi tunaoelewa mchango wake kwa taifa tunahitaji kusimama kidete wanapochafuliwa kwa makusudi viongozi wa aina yake, hilo umesikika sana mkuu, ila again naomba umwambie kama uko karibu naye kwamba ya defensive yametosha sasa, abadili message na kuanza kushambulia tena,

- Lakini heshima sana kwa maneno yako mazito, naamini ujumbe umefika unapotakiwa.

Respect.

FMEs!
 
Si ameingia katika siasa mwenyewe ? Si alitaka uwaziri mkuu huyu baada ya mwandosya kushinda uraisi kama angepata ? Si ndio huyu huyu alimtibua sana kikwete wakati yuko katika mchakato kule dodoma si anajua siasa mchezo mchafu ?

Shy, I feel like puking! This is extremely cheap talk ambayo haitujengi Watanzania! "Si alitaka uwaziri mkuu huyu .... si ndio huyu alimtibua sana Kikwete..." Ni porojo, uzushi, upuuzi, upuuzi mtupu, hata kama ni kweli. Kwa nini hatuangalii mbele? Kuna mtu katukanwa kama Obama? Umemsikia akilalama usiku kucha kuwa alichafuliwa? Hawezi, kwa sababu na yeye alichafua wengine kama Kikwete alivyochafua wenzake. Huu ndom chezo wa politics! Badala yake, Obama kawakumbatia wapinzani wake, Marekani inasonga mbele. Watanzania leo hii bado tunazungumzia uchaguzi wa 2005 na kutafuta wachawi! Hatufai kuwepo kwenye ramani!
 
It is unfortunately that we are losing our country in this manner;
  1. The Presidency - SOLD in 2000
  2. The Government - SOLD in 2000
  3. The Law Enforcement Units - SOLD in 2009 or earlier
  4. The Judicial System - Bids awaiting, but mingling the good and the ugly already in progress
  5. Legislative - Majority SOLD
  6. The Fourth Estate (Media) - SOLD or Strangled Absolutely
  7. The Army - SOLD to the politicians (Chief of Staff is a multmilionair fundraiser nowdays)
Were is Tanzania Going? Cry My Country, Cry.

makaa ya mawe sold in 2005!
 
Shy, I feel like puking! This is extremely cheap talk ambayo haitujengi Watanzania! "Si alitaka uwaziri mkuu huyu .... si ndio huyu alimtibua sana Kikwete..." Ni porojo, uzushi, upuuzi, upuuzi mtupu, hata kama ni kweli. Kwa nini hatuangalii mbele? Kuna mtu katukanwa kama Obama? Umemsikia akilalama usiku kucha kuwa alichafuliwa? Hawezi, kwa sababu na yeye alichafua wengine kama Kikwete alivyochafua wenzake. Huu ndom chezo wa politics! Badala yake, Obama kawakumbatia wapinzani wake, Marekani inasonga mbele. Watanzania leo hii bado tunazungumzia uchaguzi wa 2005 na kutafuta wachawi! Hatufai kuwepo kwenye ramani!


May be true, lakini dola kama polisi, jeshi, uwt n.k visiusishwe kwenye siasa jamani!
 
Si ameingia katika siasa mwenyewe ? Si alitaka uwaziri mkuu huyu baada ya mwandosya kushinda uraisi kama angepata ? Si ndio huyu huyu alimtibua sana kikwete wakati yuko katika mchakato kule dodoma si anajua siasa mchezo mchafu ?

''NANGA MKUBWA WEEE'',hii sentensi huwa anatumia mzee wangu kwa watu wenye uvivu wa kufikiri,kupambanua....mwenye kusema ''mbona fulani alifanya hukumchapa ndio maana nami amefanya''kwi kwi kwi
 
Inanikumbusha mambo ya waziri mkuu majivuno wa Kusadikika "Weusi wa nyweli za mshitakiwa waonyesha kwa kiasi gani hana busara"

Mkuu Mtanzania, achana na Kusadikika, hapa ni Tanzania. Nimefurahia hiyo statement ya msomi aliyebobea na hana wasiwasi. Mimi na Kombe tumesoma certificate in law pamoja na mwalimu wetu alikuwa Mwakyembe. Unataka Mwakyembe aseme nini kwa hawa abc wa sheria wanapoamua kumfanyia dharau?
 
Mwakyembe leo alalamikia ``natural justice``? Mwakyembe? Huyu mwalimu wa wanafiki alimhoji Lowassa?

Mkuu naomba nichangie kama mwanafunzi mzoefu wa sheria. Suala la Lowassa na suala la sasa la Mwakyembe ni tofauti kama usiku na mchana! Katika suala la Lowassa, Kamati Teule ya Bunge haikumhukumu Lowassa ila ilimshauri "AJIPIME MWENYEWE"! Lowassa alikuwa na uhuru wa kujipima kwa kuendelea na kazi yake au kwa kujiuzulu. Akaamua yeye mwenyewe, pengine kwa ushauri wa Regina, kujiuzulu! Lakini kwa maafisa wengine wote ambao kamati iliwahukumu, nafasi ya kusikilizwa ilitolewa! Zaidi ya yote, Lowassa as Prime Minister and leader of government business in the House, alikuwa na uhuru chini ya Kanuni za Bunge, kulihutubia Bunge wakati wowote kujitetea na kuiponda taarifa ya Kamati ya Dk. Mwakyembe. Hakuweza kutumia fursa zote hizo! Akaishia kulalama na analalama mpaka leo! Faida pekee ya njia aliyotumia Lowassa ni kwamba amekubali kuchukua political responsibility kwa makosa yaliyofanyika chini yake, hivyo anajiuzulu with full benefits of an x-Prime Minister!

Lowassa angeweza kabisa kusema amejipima na anafaa kuendelea as PM! Lakini Lowassa hakuchukua njia hiyo kwa kuwa akina Mwakyembe, Selelii, Manyanya, Mntangi na Mnyaa, walikuwa wameandaa hoja ya kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu chini ya ibara ya 53A ya Katiba. Walikuwa wameandaa ushahidi ambao ungemtaka Lowassa ajitetee mbele ya Bunge!

Lakini katika suala hili la sasa, Mwakyembe hajaambiwa na Kamati ya Kombe ajipime! Kamati ya Kombe imeenda mbele zaidi na kumhukumu kuwa ni mwongo na dereva wake mwongo bila kuwapa nafasi ya kuwasikiliza! Itakuwa vigumu kesi hii kuendelea mahakamani maana Polisi, badala ya kukusanya tu ushahidi na kuuleta mbele ya mahakama kwa uchujaji, imefanya uchujaji yenyewe kadamnasi ya watu!

Tusirush kwenye conclusions kwenye mambo ya kitaaluma. Tunahitaji kusikiliza kwa makini, kuuliza, kubukua na kuelewa!

Ijabu
 
Mkuu naomba nichangie kama mwanafunzi mzoefu wa sheria. Suala la Lowassa na suala la sasa la Mwakyembe ni tofauti kama usiku na mchana! Katika suala la Lowassa, Kamati Teule ya Bunge haikumhukumu Lowassa ila ilimshauri "AJIPIME MWENYEWE"! Lowassa alikuwa na uhuru wa kujipima kwa kuendelea na kazi yake au kwa kujiuzulu. Akaamua yeye mwenyewe, pengine kwa ushauri wa Regina, kujiuzulu! Lakini kwa maafisa wengine wote ambao kamati iliwahukumu, nafasi ya kusikilizwa ilitolewa!



Wenzako hilo somo haliingii kabisa kichwani; bado wanafikiri kuwa Lowassa alijiuzulu kwa sababu ya Mwakyembe!!
 
Hivi Wabongo tumerogwa? Tunafikiri nini sisi watu?

Yani unakubali kwamba Mwakyembe alichemsha kutokumpa mwenzake hiyo ``natural justice`` halafu akaja baadae kuwa na moral authority ya kufundisha mapolisi kuhusu ``natural justice`` wewe unaona ni sawa?

Ni ushabiki shabiki wa kufuata upepo au ni kwamba wananchi hatuna a smidge of civic education na uelewa?

LeoKweli, are you serious?

Mkuu Dilunga, hili si suala la kujua civic education, ni suala la kujua applied constitutional and administrative law na uwe na subira kujifunza mzee! Ukiwa na muda rejea hansard za Bunge uone Lowassa alivyojibiwa alipoingia na hoja hiyo wakati wa kuachia ngazi. Ni maji marefu kidogo; usiyaingie kichwa kichwa mzee!
 
Wenzako hilo somo haliingii kabisa kichwani; bado wanafikiri kuwa Lowassa alijiuzulu kwa sababu ya Mwakyembe!!
[/SIZE]

Mkuu M Mwanakijiji, heshima zako kwanza. Naliona hilo tatizo, lakini sana sana ni la uelewa tu!
Niruhusu Mkuu nitumie fursa hii kukupongeza sana kwa ile master-piece ya Jumatano kwenye Tanzania Daima: UJUMBE WA WAZI KWA EDWARD LOWASSA: UCHAGUZI NI WAKO. I wish akina Dilunga and co. wangeisoma hiyo piece, ni somo kubwa kwetu sote. Hongera sana!
 
Si ameingia katika siasa mwenyewe ? Si alitaka uwaziri mkuu huyu baada ya mwandosya kushinda uraisi kama angepata ? Si ndio huyu huyu alimtibua sana kikwete wakati yuko katika mchakato kule dodoma si anajua siasa mchezo mchafu ?

Mkuu, huu ni udaku! Of all the people, wasomi waliobobea kama Prof. Mwandosya na Dk. Mwakyembe, tena wanaotoka eneo moja, wasingeweza kuchukua ofisi zote za uongozi wa nchi wenyewe! Hivi udaku wa aina hii JF unawasaidia nini akina Shy?
 
Mkuu M Mwanakijiji, heshima zako kwanza. Naliona hilo tatizo, lakini sana sana ni la uelewa tu!


ndugu yangu hata mimi mwanzoni nilifikiria ni suala la kutokuelewa, lakini baada ya kujaribu sana kuelewesha nikagundua kuwa mtu ambaye hajui kuwa haelewi na hataki kujua kuelewa utamuelewesha vipi? Ila tutafika tu.


Niruhusu Mkuu nitumie fursa hii kukupongeza sana kwa ile master-piece ya Jumatano kwenye Tanzania Daima: UJUMBE WA WAZI KWA EDWARD LOWASSA: UCHAGUZI NI WAKO. I wish akina Dilunga and co. wangeisoma hiyo piece, ni somo kubwa kwetu sote. Hongera sana!

Shukrani lakini pasipo mwenyewe kujua impact yake, nadhani ni makala iliyonitengenezea maadui wengi zaidi kuliko yoyote ile na wakati huo huo labda kusema kitu ambacho wengine walikuwa wanakifikiria kwa muda mrefu na hawakupata nafasi au mahali pa kukisemea. Thanks.
 
...Uongo upi kausema Mwakyembe? ...Mimi hapa nina Majira ya Jumamosi Mei 23 ...inasema ukurasa wa nne wa gazeti hili, mwandishi anaripoti kuwa: "Bw. Mwakyembe alipotakiwa kueleza kama kuna hujuma kwenye ajali hiyo, alisema ni ajali ya kawaida na kwamba anamwachia Mungu".

Sasa Mkuu utamwitaje Mwakyembe muongo anaporudia maneno hayo leo?

Mungu wangu weee...!

Fataki, Fataki, sikia bro. Hayo uliyoweka hapo yanaitwa reported speech, yani maneno ya mwandishi! Sio direct speech kutoka mdomoni kwa Mwakyembe neno kwa neno. Masikini weeee! Duuuu! Usibishe wewe umekuja katikati ya thread unadandia dala dala kwa mbele wewe, utadedi wewe! Mwakyembe kaongopa.

[ame="http://www.youtube.com/watch?v=ZoVSS9qh4kU"]YouTube - Kulikoni ajali ya Dr. Mwakyembe[/ame]

``...Mimi ni Mkisto, nimemuachia Mungu hayo, nimesema Mungu kama hiyo, kilichotokea leo, ni binadamu alikipanga basi namshitakia yeye, na kama kilichotokea ni ajali, basi tumuachie Mungu. Lakini kama kilichotekia kilipangwa basi huyo aliyepangwa kufanya hivyo ni mtaalam wa hali ya juu sana maana jinsi alivyoigonga ile gari, kupoteza mwelekeo, mimi kwa kweli nimeiona hiyo, hayo matukio, kwenye sinema tu.``
 
can somebody please teach him about conditional clauses kwenye sentensi.... maana kama huu ndiyo uandishi wenyewe wa kutukosoa wengine.. inasikitisha!
 
[I said:
Mzee Mwanakijiji;470941]can somebody please teach him about conditional clauses kwenye sentensi.... maana kama huu ndiyo uandishi wenyewe wa kutukosoa wengine.. inasikitisha![/I]

Who are you referring to? Dr Mwakyembe or Dilunga?
 
Si ameingia katika siasa mwenyewe ? Si alitaka uwaziri mkuu huyu baada ya mwandosya kushinda uraisi kama angepata ? Si ndio huyu huyu alimtibua sana kikwete wakati yuko katika mchakato kule dodoma si anajua siasa mchezo mchafu ?

Kuliko Rostam na kina Mkuchika? mimi naona Shy una ajenda ya siri twambie basi ili tuwe makini tunaposoma articles zako.
 
Mwakyembe atoa kauli nzito
Thursday, 28 May 2009 16:34

*Asema Polisi wanahaha kuficha ukweli
*Ahofu ajali aliyopata Iringa kupangwa
*Akerwa uchunguzi kuendeshwa kisiasa

Na Reuben Kagaruki

Majira

SIKU mbili baada ya Jeshi la Polisi kumtaka Mbunge wa Kyela, Dkt. Harrison Makyembe, kuacha kutoa taarifa zisizokuwa za kitaalam kuhusiana na ajali aliyoipata wiki iliyopita, mbunge huyo machachari amelishukia jeshi hilo akisema limeonesha jeuri na kiburi kisichokuwa na tija na ni kielelezo kuwa baadhi ya viongozi kwenye vyombo vya dola wamelewa madaraka.

Dkt. Mwakyembe kupitia taarifa yake aliyoitoa kwa vyombo vya habari Dar es Salaam jana, alisema purukushani zinazofanywa na Jeshi la Polisi kuficha ukweli zinamfanya aingiwe wasiwasi kuwa ajali yake haikuwa ya kawaida.

Alielezea kushangazwa na kitendo cha Kamati Maalum iliyoundwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Said Mwema, kuchunguza ajali hiyo kushindwa kumhoji yeye na dereva wake ili kupata picha halisi na kamilifu kuhusiana na ajali hiyo.

"Kama mimi na dereva wangu tungesikilizwa nina uhakika taarifa ya Kamati Maalum isingelisomwa kulidhalilisha Jeshi la Polisi kwa kukosa umakini na viwango," alisema Dkt. Mwakyembe.


Alisema uamuzi wa Kamati hiyo kumkamata dereva wake na kumshitaki wakati huo huo ikiwa tayari imemhukumu kuwa ni mwongo na mzembe hivyo afunguliwe mashitaka mahakamani, hauendani na utawala wa sheria na misingi inayolindwa na Katiba na inageuza Mahakama kama chombo cha kupiga muhuri maamuzi ya Polisi.

Alifafanua kuwa hatua ya Jeshi la Polisi ina mwelekeo wa kisiasa kuliko utaalam na upelelezi wa uendeshaji mashitaka.

Alisema linapotokea kosa, kazi ya Polisi ni kupeleleza na kukusanya ushahidi kwa lengo la kufikisha suala husika kwenye chombo cha kutoa haki ambacho ni Mahakama kwa kuwa ndiyo yenye utaalam wa kuchuja ushahidi na kutenganisha uongo.

Aliongeza kuwa inashangaza kwa Kamati hiyo kupitia maelezo aliyoyatoa na yale ya dereva wake na kisha kukusanya ushahidi wa ziada na baadaye kutoa uamuzi wenye mchakato wa kimahakama.

Alipinga vikali kauli ya Kamati hiyo kuwa wakati ajali hiyo inatokea alikuwa usingizini. "Ningetegemea madai hafifu kama hayo yangetolewa na mganga wa kienyeji anayetumia ramli kufanya maamuzi na sio Jeshi la Polisi lenye wataalam," alisema.

Alisisitiza kuwa ajali hiyo aliiona kwa macho yake na asingeweza kusinzia kwa kuwa safari yake ilianzia Makambako na wakati inatokea ilikuwa ni mwendo wa saa moja hivyo kwa mazingira ya kawaida asingekuwa amelala.

Dkt. Mwakyembe alisema kitendo cha Polisi kutumia vyombo vya habari kukejeli ushahidi wa wahusika wakuu kwenye ajali, ni kielelezo cha ujeuri wa jeshi hilo.


Alisema ajali hiyo ilipotokea, Mkuu wa Polisi Mkoa wa Iringa alinukuliwa akisema chanzo cha ajali hiyo ilikuwa shimo la barabarani na kwamba ajali hiyo haikutokana na njama zozote au hujuma.

Aliongeza kuwa kauli hiyo ya RPC inamfanya ajiulize maswali matatu. "Kwanza najiuliza ni kitu gani kilimsukuma RPC muda mfupi baada ya ajali kutokea kutoa tamko kuwa chanzo cha ajali lilikuwa shimo?" Alihoji Dkt. Mwakyembe na kuongeza;

"Ni nani alimwambia RPC kuwa ajali hiyo ilitokana na hujuma au njama kiasi cha yeye kulazimika kutoa tamko gazetini mapema?" Alisema baada ya kutoa tamko hilo Meneja wa TANROAD mkoani Iringa alinukuliwa na vyombo vya habari akisema shimo linalodaiwa kusababisha ajali lilikuwa dogo. "Kamati hiyo ilibaini sababu zipi za Meneja wa TANROAD na RPC kutofautiana?" Alihoji.

Alifafanua kuwa dereva wa lori alinukuliwa na vyombo vya habari akisema hakugonga gari lao na kwamba dereva wangu alikuwa kwenye mwendo kasi na mzembe. Alisema anajiuliza ni kwa nini Kamati hiyo ilishindwa kumhoji vizuri dereva huyo wa lori?

Alihoji sababu kuendelea kuogopa kulikamata lori hilo na kulikagua ili kujua kama lina alama ya kukwanguliwa na gari lake. Aliongeza kuwa dereva wa lori alishuhudia ajali ya gari lake lakini hakusimama bali aliendelea na safari.

"Ni nini tafsiri wa Kamati hiyo kuhusiana na kitendo cha dereva huyo kuendelea na safari?" Alihoji. Kuhusu kauli ya Kamati hiyo ya kumtaka asitoe kauli zisizo za kitaalam kuhusiana na ajali, Dkt. Mwakyembe alionekana kushangazwa na hatua hiyo.

"Najiuliza ni utaalam gani unahitajika kueleza kitu kilichomsibu mtu! Mathalani nyumba yangu ikiungua moto kwa hiyo kamati hiyo inanikataza nisizungumze kuwa chanzo cha moto kilikuwa ni kibatari au mshumaa hadi nimsubiri Kombe (Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani na Mwenyekiti wa Kamati Maalum ya kuchunguza ajali, Bw. James Kombe)!"Alisema na kuongeza;

"Kwa hiyo watanitaka niwasubiri waje wapige ramli kama walivyofanya kwenye ajali yangu?" Alisema ajali nyingi zimetokea hapa nchini abiria na madereva huwa wanahojiwa lakini iweje taratibu hizo zikiukwe kwenye ajali yake.

Alihoji hamasa ya Jeshi la Polisi kudodosa kila analosema na kulitafutia maelezo mbadala inachochewa na nini na kwa faida ya nani? Alisema mtu yeyote mwenye akili timamu hawezi kutetea uzembe wa dereva kwani kufanya hivyo ni kujichimbia kaburi mwenyewe.

Alilitaka Jeshi la Polisi kutambua kuwa ni chombo kinachosimamia usalama wa raia wote bila ubaguzi hivyo kamwe lisiingizwe kwenye siasa.
 
ndugu yangu hata mimi mwanzoni nilifikiria ni suala la kutokuelewa, lakini baada ya kujaribu sana kuelewesha nikagundua kuwa mtu ambaye hajui kuwa haelewi na hataki kujua kuelewa utamuelewesha vipi? Ila tutafika tu.




Shukrani lakini pasipo mwenyewe kujua impact yake, nadhani ni makala iliyonitengenezea maadui wengi zaidi kuliko yoyote ile na wakati huo huo labda kusema kitu ambacho wengine walikuwa wanakifikiria kwa muda mrefu na hawakupata nafasi au mahali pa kukisemea. Thanks.

Pole na hongera, usiogope kuonekana an enemy of the people kwa jambo ambalo hatimaye litakuja kuthibitika you are the best friend of the people, and you wish all the best to the people you sarve. Tuliokuelewa hata kama tuu wachache, tumekuelewa vizuri na amini usiamini EL atakutafuta na kukushukuru, kama ni kati ya wasio kuelewa, then he is doomed!.
 
lakini kwa nini jamani baadhi ya magazeti yanaingia katika kushabikia mambo halafu yakiguswa yanawaka kama vile wao ni Miungu watu 🙁
 
Back
Top Bottom