Ajali ya gari Mkuranga

Inamaana wanalipwa chini ya kima cha chini?
 
Nafikiri kuna jambo si la kawaida kwa Dangote
 
Shida kubwa ya Dangote industries ni kuwa ameweka sub contractors wahindi.
Wanachoangalia wao ni maslahi yao tu .
Unakuta dreva mshahara analipwa laki 2, na mileage kulingana na umbali wa safari, tatizo liko kwenye mafuta, unakuta huo mshahara una kuwa ni jina tu, kwani kila safari unatakiwa kutumia kiwango fulani cha mafuta, ndio unayopewa na kampuni, sasa yasipokufikisha tena kiwandani hilo ni lako utakatwa kwenye mshahara wako!!,yaani kiwango cha mafuta kwa safari yamepunguzwa mno!! kwani magari hayana service!!yaani mwenye gari jipya anapewa mafuta sawa na mwenye mkweche!!kingine ni muda wa safari wanaotakiwa kuwa wamerudi kiwandani, makampuni mengine gari zao ikifika saa 12, jioni paki gari , lakini dangote ni msuli wako dreva, hivyo inawalazimu kuendesha muda mrefu ili kuwahi muda aliopewa!!unakuta gari halina taa usiku wanafunga tochi mbele kuna nini hapo?
 
kiongozi unaongea kitu unachokifahamu aisee!

kuna siku nilikuwa kijiji flani cha mchinga nikipata supu ya pweza. mara lilitokea lori la dangote na kupaki pembeni, aisee lilishuka vuta bangi moja hilooo, nilibaki kinywa wazi kwa mshangao. ni kijana mdogo tu, amevaa lishati likuuubwa (yale tukiyoyaita 'dog dog' kipindi kile) na likofia moja kubwa kweli. huko kutembea sasa; alikuwa anaswing flani hivi.....baada ya hatua kadhaa akalitoa lile likofia (lilifunika kila kitu kichwa chote hadi masikio) na kutuwezesha kuona rasta zake nyingi na ndefu sana huku akizitikisa kwa kutingisha kichwa chake km mzungu flani hv mwenyewe. nyuma yake alimfuatia kijana mwenzake aliyeshuka nae humo kwenye gari mwenye haiba km yake. tulishangaa na kusikitika sana.

hii njia ya mtwara - dar, ajali zinazohusisha gari za dangote zinashuhudiwa kila siku
 
Wale sio madreva ni wahuni tupu!!yaani wale madreva wa daladala za ucku, kwa dar, ndio hao wanoendesha magari ya dangote!!nashangaa sijui ni kwanini serikali isijaribu kuliangalia hili kwenye hiyo kampuni!!
 
Dah, basi Dangote bado hajapata management nzuri.
 
mbona mi sijapata hapo kwa dangote?
 
Yani comment nyingi hapa ni kana kwamba tumeshathibitisha kwamba Uzembe /ubovu uko kwenye gari la Dangote.
Kwa mfano ajali ya juzi gari la Dangote lilikuwa na kosa gani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…