Ajali ya gari Morogoro usiku wa kuamkia Machi 4

Damaso

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2018
Posts
3,978
Reaction score
6,739
MOROGORO: WATU watatu wamefariki dunia kwa kuungua moto baada ya magari mawili ya mizigo ,moja likiwa limebeba shehena ya mafuta yaliyotambuliwa kuwa ni dizeli kugongana uso kwa uso wakati yakipishana kwenye tuta la kupunguza mwendokasi eneo la Nane Nane, Manispaa ya Morogoro kwenye barabara kuu ya Morogoro - Dar es Salaam na yote kuteketea kwa moto.
IMG-20250304-WA0001.jpg

Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, Alex Mkama amesema tukio hilo limetoea usiku wa kuamkia Machi 4, 2025 katika eneo la Nane Nane, kata ya Tungi katika manispaa hiyo kwenye barabara kuu ya Morogoro- Dar es Salaam.

Mkama amesema magari hayo baada ya kugongana uso kwa uso yalishika moto na kutekebea na kusabisha vifo vya madereva wote wawili na abiria mmoja.
 
Hizi ajali za malori zitchunguzwe, last week kuna lorry liligongana na jingine maeneo ya Dakawa nalo liliteketea kwa moto inasadikika dereva hakutoka alifia humohumo,

Juzi kati kuna lorry jingine limeteketea kwa moto Sekenke na kuua watu wanne wote waliungua beyond recognition

Leo tena haya malori mawili yameteketea kwa moto na sijui kama yametambulika ni ya nani
 
Milango inajifunga mpaka wahanga waungue humo kwa kushindwa kutoka?.
 
Hizi ajali za malori zitchunguzwe, last week kuna lorry liligongana na jingine maeneo ya Dakawa nalo liliteketea kwa moto inasadikika dereva hakutoka alifia humohumo,

Juzi kati kuna lorry jingine limeteketea kwa moto Sekenke na kuua watu wanne wote waliungua beyond recognition

Leo tena haya malori mawili yameteketea kwa moto na sijui kama yametambulika ni ya nani
Biashara za kafara
 
Ila hii nchi bwana Zima moto wamekuja na maji machache wakarudi Tena kuleta maji 😀 daah ila nimeogopa maana nilikuta wanatoa mifupa ya marehem
Mwandishi ongezea ni gar tatu na boda moja
Gari tatu zote zimeshika moto kwa pamoja?
 
Ila hii nchi bwana Zima moto wamekuja na maji machache wakarudi Tena kuleta maji 😀 daah ila nimeogopa maana nilikuta wanatoa mifupa ya marehem
Mwandishi ongezea ni gar tatu na boda moja
Sasa nini kimekufurahisha we zuzu
 
Kwenye tuta mgongano unatokeaje...au mmoja alivamia tuta bila tahadhari...?
 
Ila hii nchi bwana Zima moto wamekuja na maji machache wakarudi Tena kuleta maji 😀 daah ila nimeogopa maana nilikuta wanatoa mifupa ya marehem
Mwandishi ongezea ni gar tatu na boda moja
Sehemu gani hqpo nane nane hapo, kona ya kwenda kola au kona ya old Dar roads.
 
Back
Top Bottom