Damaso
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 3,978
- 6,739
MOROGORO: WATU watatu wamefariki dunia kwa kuungua moto baada ya magari mawili ya mizigo ,moja likiwa limebeba shehena ya mafuta yaliyotambuliwa kuwa ni dizeli kugongana uso kwa uso wakati yakipishana kwenye tuta la kupunguza mwendokasi eneo la Nane Nane, Manispaa ya Morogoro kwenye barabara kuu ya Morogoro - Dar es Salaam na yote kuteketea kwa moto.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, Alex Mkama amesema tukio hilo limetoea usiku wa kuamkia Machi 4, 2025 katika eneo la Nane Nane, kata ya Tungi katika manispaa hiyo kwenye barabara kuu ya Morogoro- Dar es Salaam.
Mkama amesema magari hayo baada ya kugongana uso kwa uso yalishika moto na kutekebea na kusabisha vifo vya madereva wote wawili na abiria mmoja.