Ajali ya kuporomoka kwa ghorofa Kariakoo nani wa kulaumiwa baina ya wajenzi na serikali?

Father of All

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2012
Posts
7,672
Reaction score
9,039
Japo bado tunaombeleza, tunapaswa kuanza kutafuta suluhu ya mabalaa kama haya ambayo nimekuwa nikiyasikua huko kwa majirani zetu Kenya, India na hata Nigeria.

Sasa yametufika. Kwanza, nani alaumiwe baina ya wenye nyumba na serikali? Pili, nini dawa ya tatizo hili? Je tutegemee mengine kama haya?

Soma Pia: Live Updates Kuporomoka kwa Ghorofa Kariakoo Nov 16: Watu 7 wengine waokolewa
 
Wakulaumiwa wanajulikana

Huu upepo utapita wabongo watasahau

Ova
 
Lawama hazijengi, shida ya hayo majengo ipo kwenye elimu yetu inayozalisha mazwazwa katika kila sekta.
Vinginevyo wataalam wenye elimu sahihi wangetumika katika ushauri kwa mmiliki, haya maafa yasingejitokeza
 
Ajali Haina Kinga yapo tahadhari zichukuliwe. Nchi zilizoendelea majengo yanabomoka pia , Tanzania Ina Nini mpka yasibomoke.

Nguvu ielekezwe kwenye uokoaji , watu wasiwe wazembe katika uokozi, vifaa vya kisasa lakini kulaumiana kisa kubomoka jengo hata lingejengwa kwa uimara gani, likitaka kubomoka linabomoka tu.
 
Japo bado tunaombeleza, tunapaswa kuanza kutafuta suluhu ya mabalaa kama haya ambayo nimekuwa nikiyasikua huko kwa majirani zetu Kenya, India na hata Nigeria.

Sasa yametufika. Kwanza, nani alaumiwe baina ya wenye nyumba na serikali? Pili, nini dawa ya tatizo hili? Je tutegemee mengine kama haya?
kwa Neema na Baraka za Mungu,
hili linaweza kua la mwanzo na la mwisho kutokea Tanzania...

nashindwa kueleza kwa kina kirefu kwakua ni mapema mno na kuna ndrugu zetu bado wamekwama kwenye vifusi, tuwaombee kwa Mungu wafikiwe haraka na kutoka wakiwa hai 🐒
 
Ajali Haina Kinga yapo tahadhari zichukuliwe. Nchi zilizoendelea majengo yanabomoka pia , Tanzania Ina Nini mpka yasibomoke.

Nguvu ielekezwe kwenye uokoaji , watu wasiwe wazembe katika uokozi, vifaa vya kisasa lakini kulaumiana kisa kubomoka jengo hata lingejengwa kwa uimara gani, likitaka kubomoka linabomoka tu.
Jengo huwa kuna muda linataka kubomoka? Acha upumbavu.
 
Mwenyeketi wa serikali ya mtaa, ambae ndiyo serikali yenyewe ni wakulaumiwa...

Cc: Mahondaw
 
Back
Top Bottom