WakuluNimesukumwa kuandika haya baada ya kufuatilia tukio zima la ajali ya Mh. Mbunge ambaye sasa ni marehemu.Mh. Regia alikuwa mlemavu wa mguu wa kulia.Gari aliyokuwa anaendesha kwa mujibu wa taarifa za jeshi la polisi lilikuwa halijafanyiwa -modification kwamba ni gari maalumu kwa ajili ya walemavu.Sasa swali, ni mamlaka gani ilitoa leseni kwa Marehemu? wakati anajulikana kwamba ni mlemavu...... (ukizingatia kwamba kwa mujibu wa sheria zilizopo, hata ukiwa na makengeza huruhusiwi kupewa leseni) Nauliza hili kwa uchungu tukizingatia kwamba Regia alikuwa ni hazina ya taifa...... mpaka lini tutaendelea kupoteza vijana wenye uwezo mkubwa wa kulisaidia taifa hili ...kwa kuruhusu uzembe,kutoheshimu sheria na mambo yanayofanana na hayo? Ilikuwaje mfumo mzima kuanzia serikali kupitia vyombo vyake vya TRA, Trafiki polisi, ndugu, chama chake, marafiki zake, abiria aliokuwa nao kwenye gari kwa nyakati mbalimbali hawakuliona hili kwamba ni tatizo kwa marehemu kuendesha gari wakati yu mlemavu ? kwa nini hawakumkemea, hawakumshauri ....n.kSheria , kanuni na taratibu zipo kutulinda.....naamini TUNA TATIZO KUBWA KULIKO TUNAVYODHANI.....Naomba tujadili objectively...bila jazba...
Mkuu Wayne Heshima Mbele
Nadhani ulikuwa na hoja nzuri lakini ukuifanya kikamilifu kwa kuweka ushahidi wa baadhi ya lawama/Shauku zako
1) Swali lako la pili unauliza ni mamlaka gani iliyotoa leseni kwa Marehemu
Nadhani kwanza ungetuwekea hiyo leseni ya Marehemu na tukaiona imetolewa ikiwa kwenye Category gani, maana najua leseni zote zinakuwa na sehemu ya kuonyesha mwenye leseni ana ugumu gani wa kuendesha gari, (Mlemavu, anavaa miwani nk)
2) umesema Polisi walilikagua gari na kuthibitisha kuwa halikufanyiwa marekebisho ya kuendana na mlemavu
hapa point kumbe sio tatizo kwa mlemavu kuendesha gari (na ndio maana wana leseni za kuendeshea), maana hata polisi wanalijua hilo na Marehemu sio Mlemavu wa kwanza kuendesha gari, kumbe tatizo ni gari alikuwa kwenye kiwango staili kwa mlemavu
Mimi nakubaliana na wewe kuwa ukiukwaji wa kanuni na sheria ulifanywa na MArehemu, kwa kutumia leseni yake kuendesha asichoruhusiwa, ni uvunjwaji wa sheria unaoonekana ni wa kawaida machoni pa watu, ni kama mtu mwenye leseni ya gari ndogo kuitumia kuendeshea malori nk
Pamoja na hayo yote, kwa mujibu wa waliopona hiyo ajali, ni kuwa hiyo ajali haihusiani na ulemavu hata kidogo, kama alikuwa anataka kuovertake na likatokea gari lingine mbele, hapo hata kama hakuwa mlemavu hali ingekuwa ni hiyohiyo tu,
Pamoja na kuwa na hoja ya kuwa kwa nini watu wa kwenye gari hawakumkemea kwa kuendesha gari, lakini nadhani wangemkemea zaidi kwa speeding, umakini wa kuangalia kabla ya kuovertake na vitu kama hivyo