Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,897
- 6,925
Ushabiki unatuharibu, na ukweli unaonekana kupotoshwa. Kifo cha Regia kwa vyo vyote kimechangiwa kwa vikubwa na Regia mwenyewe kwa hoja zifuatazo:
- Kuendesha gari akiwa mlemavu akitumia mguu mmoja alio nao tena wa kushoto
- Kutovaa ukanda wakati akiwa behind the wheel, maana yake alichomoka toka kwenye kioo cha mbele
- Kutokuwa na gari ambalo ni maalum kwa ulemavu wake
- Kutofuata sheria za usalama barabarani ikiwa ni pamoja na usalama wa over take, mwendo kasi nk
- Kutokuwa mfano wa kuigwa kutokana na wajibu wake kuwa mtunga sheria za nchi nii na kisha kuwa ndiye mvunjaji
- Kutomheshimu mwajiriwa wake (dereva wake) ni dalili ya ubinafsi
- Kupuuzi sheria za bima
- Hakuna hakika kama alikuwa na leseni ya kuendesha gari kihalali kutokana na utata wa ulemavu wake
- Kupuuzi utaratibu wa viongozi kuwatumia madereva wao
- Kujiona yuko juu ya sheria kwa hoja ya kuwa mbunge