Ajali ya Mh Regia - tuna tatizo


Nimesoma maoni mengi kuhusu mada uliyoanzisha.Wengi sana wamekuponda lakini hata mie nilikuwa na wazo la kunzisha mada kama hii, bahati nzuri nimeikita yako. Ukweli unabaki ukweli kuwa linapokuja suala la ajali kuna ajali ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. Sasa ukiangalia mazingira yenyewe kuwa alitaka kulipita gari lililokuwa mbele yake akakutana na gari lililokuwa linakuja upande mwingine. Akaingia porini. Gari likapinduka mara (wanasema) saba. Kama gari lilipinduka mara saba ina maana alikuwa mwendo kasi, jambo linalokemewa na trafiki kila leo. Hapo mambo mawili yanajitokeza. Hakuhakikisha kama hakuna gari mbele na alikuwa mwendo kasi. Hivi ni vitu viwili havina uhusiano na ulemavu wake na VINGEWEZA KUEPUKIKA. Suala la ulemavu na uendeshaji wa gari ni suala lamjadala pia ukizingatia hali ya ulemavu wake. Mamlaka zetu unazijua zaweza kumpa mhasibu kazi ya kujenga barabara.
 
Una hakika?......mimi kila weekend napishana na Dr Mwinyi akiendesha gari lake binafsi.....mbona trafiki hawamkamati? wakati mwingine binadamu huhitaji privacy bila uwepo wa devera hata kama umuhimu upo.....sasa ufisadi unatoka wapi?

privacy hiyo ndo inaashiria matendo mabaya. haya tuambie, hela za dereva anazolipwa anapeleka wapi? anafanyia kazi gani? kama ajali iliyomchukua mbunge angekuwa na dereva wake, haya tusingeyaongelea, tungemtuhumu dereva kwa kutokuwa makini kumlinda mtu wa watu. sasa yeye mwenyewe ndo kalitifua, tumlaum nani?
 


Ndugu yangu,

Nakupongeza kwa kuliona hili. Umeuliza maswali ya msingi. Tuna tatizo kubwa kitaifa. Tumegubikwa na hisia katika kila jambo na kwa makusudi au kwa bahati mbaya tumeondokana mantiki na kweli. Post kama hii itabezwa na kupuuzwa sana humu kwa kuwa hisia zimekwishawatawala. Kila siku humu ndani watu wanajifanya kuwa mstari wa mbele kuzungumzia uwajibikaji lakini inaelekea uwajibikaji huu unawahusu watu fulani fulani tu. Na si na mashaka kuwa tunachagua viongozi kwa hisia hisia hivi hivi.

Usitegemee kupongezwa kwa post hii. Utachanwa chanwa sana. Umegusa katika jambo wanaloliamini sana, HISIA.
 

pamoja sana mkuu. unajua humu jamvini tambua kuna makundi mawili. kundi la kwanza, ni la wajenzi wa taifa. hawa huwa wanasifia pale panapostahili kusifiwa. lakini kwa kiasi kikubwa ni wakosoaji wa mambo yanayofanywa na viongozi wetu bila kujali itikadi za chama. wanaongelea uhalisia wa mambo, wanaonesha udhaifu wa kiutendaji katika nyazifa zao. kamwe hawaendekezi uchama humu ndani japokuwa ni frends wa vyama mbalimbali. they are critical.

kundi la pili ni la wapenzi wa vyama, ambao hata kama kiongozi wa chama amefanya makosa katika nyendo zake, hawako tayari kuona anasemwa kwa mabaya aliyoyafanya, watamtetea as if hakukosea. hawa sio critical, kwani wameendekeza upenzi badala ya uzalendo. Ndo hawa wanaoponda uzi huu, lakini mimi naunga mkono hoja kwani Regia kaniumiza, lakini ni makosa yake yaliyopelekea mimi kuumia. sitompata tena JF. NAUMIA SANA.

Wapenzi wa vyama, kwangu mimi ni WABOMOZI kwani kusifia ujinga, means unakubali kiendelee. Huu ni ujinga
 
Kwani tumezuiwa kufanya hivyo mpaka tumtumie marehemu kama reference? Ajali ngapi zimeua watu na mbona wasitumike kama reference hapa? Polisi hawajatoa ripoti rasmi ya chanzo ajali sasa tunajifunza kutokana hadidu rejea ipi?

wangapi tunawasema wamekufa? kila siku tunawataja akina Herbert Spencer, Karl Marx, Emile Durkheim, Max Weber na wengine kibao kwani wapo? kila siku tunamkumbuka nyerere, tunamtaja katika matamshi yetu, kwani yupo? yaani kutaja kuboronga kwa Regia Mtema ndo unaona kitu cha ajabu? acha ushabiki, kuwa critical, changia uzi kwa kuangalia mantik yake na sio kuendekeza uchama hapa, hautusaidiii. wengi tumehuzunishwa na kifo chake, lazima tuhoji mazingira ya kifo chake na tuchukue somo ili wengine wasiendelee kufa kwa mtindo uleule
 

Wengine kufa na ajali haifanyi tuhalalishe vifo vya namna hii, ndiyo maana kupitia hili tunaweza kuchukua hatua ambazo zitapelekea kupunguza hizo ajali. Basi ikiwa hivyo tusingekuwa na kampeni za kumaliza malaria, maana wengi wamekufa kwa malaria na tungeacha tu vifo viendelee. Inawezekana kupitia hii ikiwa tatizo lilikuwa ni kutokufunga mkanda basi tukaanzisha kampeni ya kuhamasishana kufunga mkanda katika gari.
 
Kila mtanzania ni hazina ya Taifa, wazima na walemavu

Mbona huulizi walemavu wanahudumiwa vipi kwenye hii nchi?

usisahau kuwa nchi yetu ulikuwa inaongozakwa kua ALBINO sasa jiulize wenye ulemavu mwingine wakoje hali zao?

Vitu vilivyoulizwa ni vingine kabisa, wewe unaleta vingine kabisa. Unanshangaza!
 

Tatizo kubwa ni pale watunga sheria wanapoziona kuwa sheria hizo wao haziwahusu. The said case is typical.

Ukweli ni kwamba, ajali yoyote ya gari husababishwa na uzembe wa fulani (source: BP nenda kwa usalama).
 
Tulishajadili hili toka jumamosi.........mwacheni apumzike na ile ilikuwa ni ajali tu......hata Sokoine alikufa kwa ajali japo hakuwa na ulemavu

mlisema watu waache kujadili kwa sababu wana majonzi na msiba. Sasa msiba umeisha kwa hy ndo muda muafaka wa kujadili..
 
HAYA BWANA AJALI ZOTE NCHI HII ZINASABABISHWA NA MADEREVA WALEMAVU SIO??

ACHA UZAYUNi WEWE

Mkuu, hii kitu ina maswali mengi yasiyojibika. Sio kweli kuwa ajali nyingi husababishwa na walemavu. Kama unajua gari, pedal ziko tatu kwa manual vehicles na mbili kwa automatic transmition. Peda ya moto na brake kwa mguu wa kulia na ya clutch kama gari ni manual transmitiion. Kwa hali ya kawaida mpendwa wetu sote asingeweza kuendesha yoyote kati ya hizo mbili. Angalau kama police wamekagua na kukuta ilikuwa special car inayoweza kuendesheka kwa mtu wenye hali kama hiyo, zipo na ni special order. Ujaribu kama una gari kukanyaga padel ya mafuta kwa mguu wa kushoto uone kama utakuwa na balance na hasa kama utakata kona ukiwa speed kali. Hutakuwa na balance kwa kusema ukweli. Hapa kuna uzembe japo inauma sana kumpoteza binti mdogo na mwenye kutegemewa sana.
 

Sijaelewa jibu lako .... Mkuu
 
Tatizo kubwa ni pale watunga sheria wanapoziona kuwa sheria hizo wao haziwahusu. The said case is typical.

Ukweli ni kwamba, ajali yoyote ya gari ni husababishwe na uzembe wa fulani (source: BP nenda kwa usalama).

mama wewe ni kati ya watu ninaowatambua kama wajenzi wa utu wetu kama taifa japokuwa kuna kipindi unajisahau na kuegamia U-CCM. Lakini nakubaliana na wewe kuwa uzembe ndio ulitugharimu mpaka hapa tulipo. Kama Bi Regia angekuwa makini, asingeendesha gari tena kwenye road ya route, inayoshawishi mwendo kasi, asingejaribu kulipita gari bila kuhakikisha usalama kuzingatiwa, yawezekana pia kwa ukiburi wa kuwa mbunge, hata mkanda hakufunga.
 

Haya mawazo yako ndipo pale inapokuja tofauti ya mzungu na mwafrika
 
may be barabara zinahitaji kupanuliwa kuwa na njia nne, mbili zinakwena na mbili zinarudi at least iwe mpaka chalinze kama si Morogoro. Ajali nyingi zitapungua wajameni
 

mtazamo wa Kiafrika, uliopata nguvu kutoka katika Uislam, kuwa Mungu ndiye anayepanga kila kitu.
I wonder kwanini Mungu apange Wajapan wafike miaka 90 wakati kusini mwa Sahara watoto wanapukutika kabla hawajafika miaka 5.
Jameni?
 
Wandugu,Nilianzisha thread hapa na watu wakajadili kidogo ila ikafa. Ngoja nirudie nilichotuma wakati huo......


Hii ni video maalumu kwa wale wote walioanza kuweka vimaneno vya kishamba humu ndani.

Sintawataja ila wanajijuwa na wanafahamu kabisa hayo maneno wameyaandika wapi.

Wamekuja na vijiswali vya kujifanya wanafahamu sana kumbe hawajui kitu.

Haya sasa, angaalieni hii video na tusikie mtasema nini....... Anaitwa Barbara Guerra.


Ukisiliza 1:40, inasemwa wazi kabisa kuwa, gari halina modifiication yoyote kwa ajili ya Vilema (Disabled).


Mwingine huyu hapa, now what????


https://www.jamiiforums.com/habari-...hana-mikono-miguu-lakini-anaendesha-gari.html
 
Last edited by a moderator:

Hapo kwenye red mpenzi ni uongo, marehemu alifunga mkanda!!! nenda kwenye website ya global publishers habari za jana uone picha.....alikufa amekaa kwenye kiti cha gari, mkanda haukufunguka na wanahisi huenda mkanda ndo ulimfanya azidi kusukwa sukwa wakati gari ilivyokuwa inapinduka na hvo kusababisha maumivu makali hadi kifo chake.....
 

Unajua alifariki siku gani weye? Yaani madereva wasipumzike na kuwa na familia zao kisa ubosi? Wewe kila uendapo unatumia dereva?

Hiyo sentensi in red hata hueleweki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…