Ajali ya MV Nyerere: Kangi, Jenista na Kamwelwe bado Mawaziri?

Ajali ya MV Nyerere: Kangi, Jenista na Kamwelwe bado Mawaziri?

Zitto

Former MP Kigoma Urban
Joined
Mar 2, 2007
Posts
1,562
Reaction score
10,888
Ajali ya Mv Nyerere: Kangi, Jenista na Kamwelwe Bado mawaziri?

Ni masikitiko makubwa kwamba, Serikali ya wanyonge imeokoa mtu mmoja, wakati wananchi wenyewe wameweza kuokoa watu 40..... hii ni aibu kubwa sana. Watu 225 wamepoteza maisha sababu ya uzembe.

Tuache kujidanganya na mapenzi ya Mungu. Mungu katupa akili, namna ya kuzitumia ni sisi wenyewe. Huwezi kupata Habari ya ajali saa nane mchana halafu ukaitisha Kamati ya Usalama mkoa saa 11 jioni ( yaani mwendo wa Dreamliner Dar-Mwanza mara 4 ). Rais naye hakuitisha Cabinet ya dharura wala Baraza la Ulinzi na Usalama Taifa kuratibu uokoaji. Uokoaji unasitishwa sababu ya GIZA? Tukihoji mnasema tunaleta Siasa? Nonsense!

Kwa nchi zilizoendelea Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Waziri wa Ujenzi na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu walitakiwa wawe wamekwishafutwa kazi au wamejiuzulu wenyewe.

Miaka 57 baada ya uhuru...Jeshi la uokozi linapoishia kuwa jeshi la UOPOZI, ni wakati wa rafiki nyangu Kangi Lugola kupumzika. Waziri Kamwelwe, Jenista na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza wanapaswa kufukuzwa kazi mara moja. Bahati mbaya sana Rais amechoka na hivyo hajali tena. Wazembe Ndio wameongoza mazishi ya ndugu zetu leo.
 
Mpaka sasa sijaona hata zile Amphibious Boats wanazotumia wenzetu kwenye majanga kama haya, inawezekana hatujawa na uwezo wa kuzinunua?
 
Wakati wakiendelea kumshambulia, dakika kama 3 zilizopita, Zitto kawapa ukweli watawala na kawatuhumu kwa uzembe kuanzia mkulu na wasaiidi wake wote wanaohusika.

Kaanza kumlaunu RC kwa kuitisha kikao cha kamati ya ulinzi na usalama saa 11 jioni huku ajali imetokea saa nane kamili mchana.

Pia, kamlaumu mkulu kwa kutoitisha kikao cha dharura cha ulinzi na usalama kuhusiana na tukio hilo.

Kataja na orodha ya mawaziri wanaopaswa kufukuzwa mpaka sasa.

Zitto hakuishia hapo tu, bali ameishangaa serikali kwa kuokoa mtu mmoja huku wananchi wakiokoa watu arobaini.

Kwa hakika Zitto harudi nyuma.

Kazi mnayo.

Chanzo:Ukurasa wake wa facebook.
 
..I can smell fish
..take care of your safety chief
Hakuna wa kumzuru huyu, lakini anachokifanya ni kutumia huu msiba kuiprovoke Serikali ili aakamatwe and it is for his own gain, political stunts, and nothing else, vijana wa umri wake Europe wapo busy kubuni vitu vya msingi kwa ajiri ya Nchi zao, yeye yupo busy kuitumia elimu yake na akili yake kupigania Maslahi ya tumbo lake!
 
Back
Top Bottom