Ajali ya Precision Air: Ripoti yabaini hakuna Control Tower, Boti za Uokozi zilichelewa, Mhudumu na Abiria ndio waliofungua mlango

Ajali ya Precision Air: Ripoti yabaini hakuna Control Tower, Boti za Uokozi zilichelewa, Mhudumu na Abiria ndio waliofungua mlango

Hivi black box kazi yake ni nini? Na hyo ripoti imengalia vitu gan mpak kuja na majibu ya hvyo , duniani kote ripoti za ajali ya ndege primary data ni black box , kwenye hii ya kwetu hata black box haitajwi
Huku kwetu tunatumia white box hiyo black box hua kwa wazungu .....sisi tunasikiliza abiria basi hicho kibox na rekodi zake hakina muhim[emoji41]
 
Msichokijua wewe na nani? mmeo? mlikuwa mnajua kwamba ndege ilikuwa ikielekea kutua kwenye run way ghafla kukatokea mtikisiko na ndege kugeua na kuangukia ziwani?

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
Sasa wwe unataka kusingizia nguvu za giza ndiyo ziliisukuma Ndege kuelekea Ziwani japokua ilitua kwenye run away yake!!
 
Based on this report, I suspect the aircraft encountered windshear on final approach. The worst nightmare for every pilot.
 
Msichokijua wewe na nani? mmeo? mlikuwa mnajua kwamba ndege ilikuwa ikielekea kutua kwenye run way ghafla kukatokea mtikisiko na ndege kugeua na kuangukia ziwani?

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
Na Mama yangu, mtikisoko wewe ulikuwa kwenye ndege sasa nani asiyejuwa ndege inaenda kutua kwenye runaway au kuna mtu alisema wanaenda kutua kwenye maji. ondoa ujinga wako humu
 
6m anarudisha au?
kama mlango ulifunguliwa na mhudumu kwa nn yeye hakujiokoa.ni kweli katika mazingira ya kawaida ufungue mlango halafu wewe mwenyewe ukubali ufe kwa kuwaokoa kwanza wengine?tusaidiane hapo.mm siko kinyume na taarifa lkn kuna maswali yanahitaji majibu ya kina.
 
kama mlango ulifunguliwa na mhudumu kwa nn yeye hakujiokoa.ni kweli katika mazingira ya kawaida ufungue mlango halafu wewe mwenyewe ukubali ufe kwa kuwaokoa kwanza wengine?tusaidiane hapo.mm siko kinyume na taarifa lkn kuna maswali yanahitaji majibu ya kina.
Wapi umeambiwa muhudumu alikufa? wahudumu wote wawili walipona.
 
Watu wanavyong'ang'ana na majaliwa despite the report kwakweli hii ni nchi ya mazombie!!!
 
Ripoti ya kitaalamu ya ajali za ndege haichukui wiki au mwezi, hii kwenye aviation wanaita preliminary report, (taarifa ya awali) ambayo inatolewa kufuatia mahojiano na mashuhuda, waokozi, n.k.

Ripoti ya kitaalamu ni hadi watakaposoma vifaa maalumu toka ndani ya ndege (black boxes) ili ndio vitakavyobaini nini kilitokea kwa ndege tangu inatoka Dar hadi inapata ajali.

Hii inaweza kuwa miaka.
Hiyo unayoitaka ww ni ile Ripoti ya kujua hasa chanzo cha ajali kwa kina, lkn kwa uharaka na kwa mahojiano ya Manusura wale, tunakaa hapo kwa yule MAJALIWA na mchongo.
 
black box?Kwani hivi Vindege vya kutumia propella havinaga BLACK BOX?
 
Kwa hapa Tanzania anga si inamilikiwa na serikali, itakua kweli isipokua international flights.
Mamlaka ya anga ya Tanzania TCAA ipo huru sana na inafuata sheria au taratibu strict za mamlaka ya anga duniani ICAO.

Ukirusha ndege inaonekana kwenye mifumo ya kusimamia usafiri wa anga duniani kote wanaona taarifa zako.
Ndege ili ipewe kibali cha kuruka angani lazima ipate Airworthiness certificate na lazima kuwe na bima n.k.
Kama serikali ya Tanzania ikiingilia kati na kuruhusu ndege ziendeshwe bila bima siku ikitokea ajali waliotengeneza ndege lazima watume mwakilishi kwenye uchunguzi, na wachunguzi wengine wa kimataifa wahusushwe. Ikionekana hakukuwa na bima itakuja kutufanya tushitakiwe sababu tumeweka saini kwenye mikataba ya kimataifa.

Sisi ni wanachama wa ICAO (International Civil Aviation Organization).
 
Hivi niulize jamani, ndege ina milango miwili?

Maana mm sijawahi panda ndege, kama jibu ni ndio basi tugawe mlango mmoja Majaliwa alifungua kwa nje na mlango wa pili mhudumu wa ndege na abiria walifungua mlango wa upande wa pili wa ndege kwa ndani, kama jibu ni hapana basi mlango ule mmoja mhudumu na abiria walipokua wanaufungua kwa ndani Majaliwa alikua anaupiga kwa kasia kwa nje ndio maana maana majaliwa alipoona pamefunguka akawafuata marubani ndani ya maji (nahisi hapa stori imebalance atakaeuliza tena sijui blaa blaa tumtafutie jina)
 
Ripoti ya Wizara kuhusu ajali ya ndege ya Precision imetoka. Baadhi ya mambo muhimu ni:

1. Bukoba airport haina control tower. Ndege zote zinazotua Bukoba marubani hujiongoza wenyewe.

2. Rubani alijua anatua kwenye runway wa uwanja, sio kwenye maji. Haikuwa water landing kama ilivyoelezwa na baadhi ya watu.

3. Kuna uwezekano ndege ilisukumwa na upepo (wind shear) kwenda ziwani, wakati rubani akijaribu kutua.

4. Landing gear haikua na tatizo na sio kweli kwamba tairi zilikataa kuchomoka kama ilivyoelezwa na baadhi ya watu.

5. Abiria hawakuwa na life vests/jackets.

6. Mlango ulifunguliwa na mhudumu mmoja wa ndege (wa kike) kwa kusaidiana na abiria mmoja (wa kiume) ndani ya ndege, na sio Majaliwa kama ilivyovumishwa. Abiria huyo ndiye aliyeshikilia mlango hadi watu wote wakatoka. Alipouachia ulijifunga na haukufunguka tena.

7. Kikosi cha polisi wa majini (Marine) kilikuwa nje ya Bukoba na kilifika masaa 4 baada ya ajali kutokea. Na hata kilipowasili, meli yao haikua na mafuta wala hawakua na mitungi ya oxgen, hivyo hawakuweza kufanya lolote.

8. Ukiondoa abiria wachache waliofariki papo hapo baada ya ndege kuanguka, abiria wengi walifariki kwa kuzidiwa maji, wakiwemo marubani wote wawili ambao hadi dakika 5 baada ya wavuvi kufika walikua hai. Juhudi za haraka zingefanyika abiria wengi waliofariki wangeweza kuokolewa.

9. Wavuvi hawakufungua mlango, bali walisaidiana kuwavusha abiria kutoka kwenye ndege kwenda ufukweni kwa kutumia mashua zao.

10. Kukosekana kwa control tower kwenye uwanja wa ndege wa Bukoba (freequency 118.2MHz ) kunaweza kusababisha ajali mbaya ya ndege kugongana angani (mid air crash) ikiwa ndege nyingi zitatumia uwanja huo kwa wakati mmoja.!View attachment AIB BULLETIN ACC 6-22 5H-PWF 21 November 2022 (1_221122_122008.pdf
 
Nimeishia kusoma hapo namba tatu nimeacha, kwahio mara rubani alidhani maji ndio runway, mare ndege ilisukunwa, n.k. njia ya uwongo fupi tu, visingizio havina mashiko.

2. Rubani alijua anatua kwenye runway wa uwanja, sio kwenye maji. Haikuwa water landing kama ilivyoelezwa na baadhi ya watu.

3. Kuna uwezekano ndege ilisukumwa na upepo (wind shear) kwenda ziwani, wakati rubani akijaribu kutua.
 
FE35BCCE-6E5F-49B1-8FAF-8B67F47856EA.jpeg
 
Samia anadanganywa kila mara nae anarukia fasta fasta tu
 
Hata kama majaliwa hakufungua mlango,ikumbuke wao ndio waliowaokoa kutoka majini.Maana bila mitumbwi ya akina majaliwa sijui tungesemaje.

"""MAJALIWA NA KUNDI LAKE KWENYE SUALA LA UWOKOZI HALIEPUKIKI""
20221121_095618.jpg
 
Back
Top Bottom