Ajali ya Precision vs Ajali zingine : Serikali ya Tanzania haijawahi kumthamini Maskini

Ajali ya Precision vs Ajali zingine : Serikali ya Tanzania haijawahi kumthamini Maskini

torosi

JF-Expert Member
Joined
Aug 12, 2020
Posts
862
Reaction score
1,430
Wana JF

Kwanza nitoe salama zangu za pole kwa wahanga wote wa Ajali ya precisionairtz.com iliyotokea Bukoba.

Nimejaribu tu kuwaza kama hii ingekuwa ni ajali ya basi , tungeona haya tuliyoyaona leo . ? Thamani ya maskini wa Tanzania iko wapi.?

- Ajali nyingi zinatokea nchini hatujawahi kuona waziri mkuu kapanda Helicopter kwenda eneo la tukio

- Ajali nyingine zinatokea hatujawahi kuona ajali inapata airtime kama za ndege

- Ajali nyingi zinatokea, ubalozi wa Marekan hatujawahi kuona ukitoka pole nyingi kama za leo

- Ajali nyingi zinatokea, ila coverage ya taarifa kwa media za nchini na nje huwa sio kubwa kama za ndege

Ina maana hizi ajali nyingine hua sio ajali au wanaokufa huko huwa si binadam.
 
sasa hivi huenda watu wanapiganisha waingie kwny Tume ya uchunguzi wapige mtonyo wa posho wanajua wakimaliza uchunguzi wanakabidhi report baada ya kusomwa inawekwa kabatini halafu Lulu diva anajirekodi picha hatarishi tunahamia huko
 
Hapa tuko tunaanda budget ya kuaga miili katika mkoa wa kagera. Kikubwa fungu la maafa litumike kwa percent fulani.
 
Siokweli kwamba serikali haina mpango na maskini. Mengi sana yanafanyika kwa nia ya kubadilisha maisha ya mtu wa kawaida. Hayo madaraja yanajengwa kwa ajili ya mtu wa hali ya chini.

Mashule yanajengwa kwa ajili ya mtu wa hali ya chini, mengi sana yanafanyika kwa nia njema kabisa,

Nongwa ndio ugonjwa wetu wa miaka na miaka, yote mazuri yatasahauliwa na lawama zinageuka kuwa ni za muhimu.
 
Hakuna ajali imewahi kutokea timu ya madaktari bingwa ikatumwa kwenda kusaidia
 
Back
Top Bottom