Ajali yaondoa Uhai wa Mwana hipHop "Shawty Lo"

Ajali yaondoa Uhai wa Mwana hipHop "Shawty Lo"

Umofia Kwenu Wana JF,

Mwanamziki wa hip-hop Carlos walker aka Shawty Lo amefariki dunia kwa ajali ya gari iliyotokea ATL,Georgia,Usiku wa kuamkia jumatano.

Shawty Lo alikuwa akiendesha gari Audi ya Mwaka 2016 ilipoteza muelekeo na kugonga miti ya pembeni na kupinduka kisha kuungua,gari imearibika vibaya upande wa mbele na tyre ya nyuma ilichomoka na kuuingia kwenye buti.

Shawty Lo ndio aliyekuwa anayeunda kundi la D4L ambayo walitamba na kibao cha laffty taffy kilichotoka mwaka 2005.Kibao kilichompatia umaarufu ni "Dey know" ambacho alikitoa mwaka 2008.

Shawty Lo ameacha watoto 11.

Shawty Lo Enzi za Uhai wake.
View attachment 410875

Shawty Lo Akiwa na Wake zake(Waliosimama) na watoto.(waliokaa -Ke 8 ,Me-3)
View attachment 410877

Picha ya gari/ajali aliyopata.
View attachment 410878
Baadhi ya Kazi zake zilizompatia Umaarufu.(Dey Know)


Hapa Akishirikishwa na Soulja Boy-Gucci Bandana

Nadhani ni [emoji471] [emoji481] [emoji485] [emoji482]
 
Hello dey know, huyu jamaa namfananishaga na jamaa mmoja hivi jina limenitoka kidogo, huwa nawachanganya kidogo, RIP SOLDIER
 
Yani huyu jamaa kafariki toka tarehe 21 mwez uliopita me mwenyewe nimekuja kupata taarifa zake jana, Daaah Namkumbuka sana na sauti yake ile kwenye Foolish na Dey Know, Anajiitaga KING WA BANKHEAD, RIP Shwaty Lo
 
Back
Top Bottom