kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 18,154
- 17,491
Wote tunafahamu kuwa baada ya kumaliza kula chakula kingi kizito mtu huanza kusinzia muda mfupi baada ya kumaliza kula.
Tunafahamu wote kuwa muda mfupi baada ya kumaliza kula na chakula kuanza kusagwa na kuvyonzwa mwilini mishipa ya damu inaelekeza damu nyingi kutoka sehemu zote za mwili kwenda kwenye tumbo na utumbo kwaajili ya kuchukua chakula kukitawanya kwenye viungo vingine vya mwili kwa matumizi mbalimbali ya mwili.
Katika zoezi hili la kuchepusha damu ielekee kwenye utumbo ili kubeba chakula kukisambaza mwilini kunasababisha upungufu wa damu wa muda kwenye viungo vya mwili ukiwemo ubongo. Upungufu huu wa damu kwenye ubongo utasababisha pia upungufu wa glucose na oxygen kwenye ubongo, hivyo kusababisha mtu kusinzia baada ya kula msosi mzito.
Baada ya kumaliza kula msosi mzito lazima upate muda mrefu kidogo usiopungua dk 45 hadi 60 hivi ili kupisha mchakato huu wa mwili baada ya kula upite salama.
Tatizo liko kwa madereva na wafanyabiashara wa hoteli kando ya barabara kuu (hiways). Wenye hoteli hizi wanaingia makubaliano na madereva kusimamisha/kuingiza magari yao ya abiria kwenye hoteli zao kwa malipo ya chakula na fedha kwa maderefa watakaosimamisha magari yao hapo na abiria kushuka kuchimba dawa na kula hapo. Kondakta wa basi anatangaza abiria kushuka na kutumia dk 7 kula na kuchimba dawa kwenye hotel husika.
Dereva na wafanyakazi wanashuka haraka na kupewa misahani ya chakula ikiwa imejaa pomoni, wanafakamia harakaharaka na baada ya dk 7 hadi 10 dereva anaingia kwenye gari na kupiga honi kuita abiria wake waendelee na safari. Ajali nyingi zinatokea kuanzia hapo. Dereva anasinzia kipande kirefu cha barabara hasa pale anapokosa mtu wa kumsemesha njiani ili asilale. Ghafla uso kwa uso au kuligonga gari nyuma, ajali tayari tena sehemu nyeupe iliyonyooka kabisa.
Pamoja na chakula kuna kuchoka, kuumwa na kutolala vizuri siku iliyopita kabla ya safari.
Tufanye nini kuzuia ajali zinazotokana na kula chakula kingi njiani?