Ajali za barabarani zinatokea muda mfupi baada ya dereva kumaliza kula chakula cha bure

LATRA hivi hawana taarifa kama hizi? Wanang'ang'ana kutaka kukata points leseni za madereva bila kufanya utafiti kuhusu visababishi vya ajali za barabarani. Hakuna mtu anaeweza kuzuia kusinzia au uchovu zaidi ya kupunzika vyakutosha
 
Kwa Tanzania, kanuni zilizopo za barabarani zinaeleza kuwa dereva wa gari la biashara, basi la abiria au gari zito hapaswi kuendesha zaidi ya saa 5 mfululizo bila mapumziko ya angalau dakika 30, isipokuwa masharti maalumu yanapotumika. Pia kuna kikomo cha saa za kuendesha kwa siku.
 
Kwa mujibu wa Traffic Regulations, Rule 36, kwa ujumla dereva wa basi anatakiwa kupata mapumziko yasiyokatizwa ya angalau dakika 30 anapofanya zamu ya kuendesha inayozidi saa 5.
 
LATRA hivi hawana taarifa kama hizi? Wanang'ang'ana kutaka kukata points leseni za madereva bila kufanya utafiti kuhusu visababishi vya ajali za barabarani. Hakuna mtu anaeweza kuzuia kusinzia au uchovu zaidi ya kupunzika vyakutosha
Ni kama viongozi Wetu wanaoenda nchi za nje wananunua suti na kurudi bila kujifunza kitu

Wasimamizi hawana habari na sisi
Na ripoti za polisi wao kila ajali eti imefeli breaks
 
Madereva hawapewi muda wa kutosha wa kupumzika.
Bus iliyopata ajali juzi Ina madereva wawili, wala hakuwa mmoja.
Ila hao wawili sehemu ya kulala hakuna.

Ufinyu wa barabara,
Nadhani kabla ya kuwalaumu madereva, tungerekebisha kwanza barabara zetu.
 
Zinafuatwa? Nani aliwahi kupewa adhabu kwa kuendesha zaidi ya masaa 5 bila kupunzika. Kutoka Dar hadi Arusha masaa 5 ni wapi?
 
Kwa mujibu wa Traffic Regulations, Rule 36, kwa ujumla dereva wa basi anatakiwa kupata mapumziko yasiyokatizwa ya angalau dakika 30 anapofanya zamu ya kuendesha inayozidi saa 5.
Mfano kutoka dsm kwenda dodoma dereva anatakiwa akapunzike wapi dk 30?
 
Zinafuatwa? Nani aliwahi kupewa adhabu kwa kuendesha zaidi ya masaa 5 bila kupunzika. Kutoka Dar hadi Arusha masaa 5 ni wapi?
Its none of my business dogo ila ndo kanuni inavyosema.
 
Ni kama viongozi Wetu wanaoenda nchi za nje wananunua suti na kurudi bila kujifunza kitu

Wasimamizi hawana habari na sisi
Na ripoti za polisi wao kila ajali eti imefeli breaks
Sio kweli, ajali nyingi ni dereva kusinzia akiwa anaendesha, hasa sehemu ndefu iliyonyooka kwelikweli. Siku moja nikiwa naenda sabasaba dereva wa lori anaenda Mtwara lakini alinigonga pale maeneo ya uwanja wa taifa. Kumuuliza akasema alisinsia.
 
Madereva hawapewi muda wa kutosha wa kupumzika.
Bus iliyopata ajali juzi Ina madereva wawili, wala hakuwa mmoja.
Ila hao wawili sehemu ya kulala hakuna.

Ufinyu wa barabara,
Nadhani kabla ya kuwalaumu madereva, tungerekebisha kwanza barabara zetu.
Ile siti ambayo staff anatakiwa kukaa anaiuza kwa abiria kisha yeye anasimama.
 
Sio kweli, ajali nyingi ni dereva kusinzia akiwa anaendesha, hasa sehemu ndefu iliyonyooka kwelikweli. Siku moja nikiwa naenda sabasaba dereva wa lori anaenda Mtwara lakini alinigonga pale maeneo ya uwanja wa taifa. Kumuuliza akasema alisinsia.
Ajali zote sio za kulala kuna za matairi vipara, dereva kuongea au kuchat , head on collision, na hizi ndio nyingi kwani dereva andhani anaweza kuvuka haraka, usingizi unachangia sana tu lakini sio zote.

Majuzi alikamatwa dereva akiwa ameuza seat ya mapumziko kwa msafiri kwa tamaa zake za hela ndogo
Safari ilikuwa nafikiri Dar- Kigoma
 
Na dereva ilisisinzie anakunywa vinywaji vya kuongeza nguvu kwa wingi na matokeo yake anaunguza Figo na kuanza kuugua baada ya kipindi fulani.
Akiianza kuumwa anapelekwa kwa waganga wa kienyeji kutibiwa kwa kuamini amerogwa na madereva wenzie
 
Kwamba madereva wa long routes kwa nchi nyingine zisizo na wingi wa ajali kama kwetu ndio hawali?

Tutafute kujua vyanzo vingine vya ajali kama ubovu wa magari, barabara mbovu, barabara nyembamba, uzembe, kukimbiza magari n.k
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…