McLaren
JF-Expert Member
- Feb 19, 2025
- 1,170
- 3,743
Watu 43 wamefariki dunia na wengine 44 kujeruhiwa katika ajali mbali za magari zilizotokea Wilayani Same mkoani Kilimanjaro na Manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa.
Tukio la kwanza ni la basi la Channel One kugongana uso kwa uso na Toyota Costa iliyokuwa imebeba watu waliokuwa wanakwenda kwenye 'Send Off' mjini Moshi,kisha magari hayo kuwaka moto.
Katika ajali hiyo hadi jana usiku miili ya watu 37 ilitolewa ndani ya magari hayo ikiwa imeungua moto,huku 23 wakiokolewa wakiwa wamejeruhiwa sehemu mbalimbali.
Ajali ya Sumbawanga ilihusisha Toyota Hiace na Bajaji na ilitokea katika Mlima Ulinji na kusababisha vifo vya watu sita huku 21 wakijeruhiwa.
Source: Nipashe