Ajali ZNZ: Vodacom waanza kugomewa

Ajali ZNZ: Vodacom waanza kugomewa

Mbona sisiem waliendelea na shamrashamra za uzinduz wa kampeni igunga.kuweni na fikra pevu.

Mkuu is Mwamvita not one of the alter ego of the company? Kwa hiyo wakati Vodacom wanamtumia wakati wa mema, kwa nini asitumiwe wakati wa mabaya?

Kulikuwa na sponsors 5

jiulize kwanini watu wameamua kuwabebea bango vodacom?

Siwalaumu Vodacom sana ila hawa TBC wanaoendeshwa na kodi yangu walishindwa nini kutuwekea uzi hata chini kuhusu msiba huu mkubwa? Nina hakika tangu saa kuminamoja asubuhi taarifa walikuwa nazo, na wanajiita 'UKWELI NA UHAKIKA '
Mimi nadhani JF nayo ianzishe ka-utaratibu ka kuweka breaking news kwa mtindo huu wa kupitisha habari kwa chini, kunakuwa na toolbar then news zinapita ziki-scroll

wa kulaumiwa ni:
1. CCM
2. TBC
3. TFF

Lkn pia SMZ wasitake msaada toka Tanganyika pale wanapokuwa na shida tu. Siku zote wanasema hawautambui muungano. Huo ni unafiki mkubwa sana wa hawa jamaa zetu. Kila kitu cha utaifa wanacho: bendera, wimbo wa taifa, rais, etc, etc

Kulikuwa na sponsors 5

jiulize kwanini watu wameamua kuwabebea bango vodacom?

Mkuu kunaweza kuwa na sababu nyingi tuu. Mojawapo Vodacom ni kampuni kubwa na maarufu sana Tanzania, so watu wanafikiri it should lead by examples. Nafikiri kati ya hao sponsors watano, Vodacom ilikuwa ndio kampuni kubwa. Sababu nyingine Vodacom imekuwa sana mstari wa mbele ku champion corporate social responsibility. Kwa sababu hii tuu yenyewe watu wengi wanadhani Vodacom ingekuwa mstari wa mbele kama walivyokuwa kwenye mabomu ya gongo la mboto. Kumbuka hii coporate social responsibility ni mojawapo ya sababu inayoifanya vodacom kulipa kodi ndogo zaidi ya Airtel japokuwa vodacom ina wateja wengi zaidi ya Airtel. Watu wanauliza where was vodacom corporate social responsibility kwenye hili janga?

Wapo wengine wanasema Vodacom haina wateja wengi Zanzibar ndio sababu waliamua kuendelea na Miss Tanzania. Sidhani hata vodacom wataikubali hii sababu b'se kibiashara haijakaa vizuri. Vipi kama janga lilikuwa limetokea Tanzania bara? Unafikiri haya mashandano yangeendelea? This event was not Miss Tanzania Mainland. It was Miss Tanzania. Kama alivyosema Mh Zitto hili janga lime test umoja na utu wetu. Kwa hili janga tumejua umoja, ushirikiano na utu wetu upo wapi.

Ku sponsor tuu Miss Tanzania itself ni corporate social responsibility. Pia kwa kampuni kusaidia watu watu waliokubwa na janga ni part ya corporate social responsibility. Na haya mambo yanapotokea kwa wakati mmoja inaweza kuwa ngumu ku make a right decision. But as a company, you will have to make a bold decision. Na katika maamuzi ya kampuni lazima itake into account its business interests presently and in future.

Lakini kama nilivyosema kwenye post yangu ya nyuma, this is problem rooted in our society. Kumbuka jana kulikuwa sio tuu na Miss Tanzania. Kulikuwa pia na ufunguzi wa kampeni za kisiasa huko Igunga. Kulikuwa pia na michezo ya mbalimbali. Tunachukulia issues very lightly. All go down kuwa kama serikali ingekuwa imetoa tamko tokea mapema haya yasingetokea. Hata hivyo vyombo vya habari hasa vya bara vimechangia sana haya kutokea. Nilishangaa Zanzibar disaster was trending worldwide on Twitter lakini kwenye vyombo vyetu vya habari vya ndani ilikuwa kama halikuwa janga kubwa.

Hivi anayeandaa miss tz ni voda? Yeye sio mdhamini tu kama ilivyo kwa ligi kuu ya soka tz?

napenda sana. Unasema ukweli, tusilaumu bila reasoning. Voda wao hatakama wangeambiwa miss tz ni baada ya mwezi wangekuwa poa. Tuwe makini wa TZ, tujenge taifa linalojali hoja ndipo uzembe wa vyombo vinavyohusika na kulinda maisha yetu tutaweza kuutamka na kuuanika hadharani. Ama sivyo tutaendelea kupotea kwa kulinda ukweli usiwekwe wazi na kumpaka matope asiyehusika.

As critical thinker nahitaji mda kutafakari kabla sijaongea kuhusu ili.

Lakini kama nilivyosema kwenye post yangu ya nyuma, this is problem rooted in our society. Kumbuka jana kulikuwa sio tuu na Miss Tanzania. Kulikuwa pia na ufunguzi wa kampeni za kisiasa huko Igunga. Kulikuwa pia na michezo ya mbalimbali. Tunachukulia issues very lightly. All go down kuwa kama serikali ingekuwa imetoa tamko tokea mapema haya yasingetokea. Hata hivyo vyombo vya habari hasa vya bara vimechangia sana haya kutokea. Nilishangaa Zanzibar disaster was trending worldwide on Twitter lakini kwenye vyombo vyetu vya habari vya ndani ilikuwa kama halikuwa janga kubwa.

Comrade, Your last paragraph is the penultimate shell explaining the reasons ya kujikuta kwenye hili "bonde la kashfa!"

I am gonna say it once more; one phone call kusimamisha shughuli zote hizo ingelitosha. Lakini ndo' hivyo tena, yule tuliyemchagua na kuamini anaweza kufanya hivyo - hajui kama anaweza kufanya hivyo, au amesahau, au basi kwa sababu tusizozijua, hawezi kufanya hivyo!!

Kulikuwa na sponsors 5

jiulize kwanini watu wameamua kuwabebea bango vodacom?

kwa sababu VODACOM wanaaminiwa zaidi ya Serikali

kwa sababu Vodacom ndio waliokuwa wadhamini wakuu wa hili shindano

kwa sababu kila likitokea janga Vodacom hujitia mstari wa mbele kuonyesha they can do better than wengine

kuna mtu anazo twitter feeds za Mwamvita?

I'm curious kujua anasema nini

vodacom hawa wanadhamini tu mashindano mengi yakiwemo premier league, miss tz, mashindano ya ngarawa nk. Wenye miss tz jamani sio voda ni lino agency. Tusilaumu tuu, voda hapa hangeweza ahirisha hili shindano ila tu mwenye nalo yaani LINO

kuna mtu anazo twitter feeds za Mwamvita?

I'm curious kujua anasema nini

Her latest tweet: "yes we are, first thing tomorrow. Giving much needed medicals in Znz today"

Sawa,,,uungwana haukuoneshwa na voda wala ccm walofanya kampen

Ubepari ni kama unyama, Vodacom as any Capitalist venture ni li dude fulani lipo kutafuta faida hata kwa kunyonya damu. Hiyo CSR ya capitalist ventures ni njia tu ya kujikosha tu kutusahaulisha njisi wanavyotukamua

Katika matukio kama haya wako makampuni makubwa yanakuwa smart sana huwa wanaangalia upepo wa serikali; wakiona serikali ina msimamo huu basi yanaegemea huko huko. Sasa kamaa serikali walikuwa kimya, CCM(chama chenye serikali) walikuwa wanaendelea na shughuli zao, wao Voda wasimamishe maonyesho kwa ajili gani?. After all si watapeleka misaada kwa survivors baadaye na itapokewa na kiongozi wa SMZ kwa mbwembwe kibao?

Utashangaa huenda hata Voda walicontact authorities kuhusu kusitisha hayo mashindano huenda waliambiwa endeleeni tu. Ombwe la uongozi ni kubwa sana, ni kama watu hawajui nani afanye nin. Kama baada tu ya tukio angetokea kwenye TV waziri mkuu na kutangaza kusimamisha shughuli zozote za burudani kama Muziki, mpira, maonyesho na kampeni za Igunga (hii nayo ni burudani, mana kama mtu aliyeita chama uchwara halafu leo anakaa jukwani) si ni burudani tosha kuliko hata hiyo beuaty pageant.

Kiini hasa cha hili ni tatizo ni kukosekana coordination na maadili ndani ya serikali, TBC1 wamezoea kuamrishwa (micromanagement) ya viongozi wa juu , maana kama Ikulu/ waziri anapiga simu studio ya TBC! kusimamisha kipindi si zaidi sana atapiga simu kuwaambia wapige tu nyimbo za maombolezo, kwa hiyo TBC1 walikuwa wanasubiri maelekezo kutoka juu kama inavyokuwa siku zote

Ni hayo tu kwa mtazamo wangu

Lakini kama nilivyosema kwenye post yangu ya nyuma, this is problem rooted in our society. Kumbuka jana kulikuwa sio tuu na Miss Tanzania. Kulikuwa pia na ufunguzi wa kampeni za kisiasa huko Igunga. Kulikuwa pia na michezo ya mbalimbali. Tunachukulia issues very lightly. All go down kuwa kama serikali ingekuwa imetoa tamko tokea mapema haya yasingetokea. Hata hivyo vyombo vya habari hasa vya bara vimechangia sana haya kutokea. Nilishangaa Zanzibar disaster was trending worldwide on Twitter lakini kwenye vyombo vyetu vya habari vya ndani ilikuwa kama halikuwa janga kubwa.

Ni kweli mkuu tatizo limeanzia kwa serikali kushindwa kushughulika vema katika kutoa taarifa na mwongozo katika wakati muafaka. Tunaweza kuilaumu Voda (na sponsors wengine) ama waandaji wa shindano lenyewe (au hata wengine walioendelea na starehe zao kama kawaida kwa siku ya jana), kwa kutokuwa 'sensitive' lakini kuwaadhibu nadhani itakuwa ni kuwaonea. Kwa mfano ni vigumu kwa kampuni kufanya maamuzi kama ya kujitoa kudhamini fainali ya mashindano katika siku ya mwisho bila ya kuwepo kwa tamko/taarifa rasmi ya serikali.

• Thanks
Reactions: EMT
VODACOM ndiye mdhamini mkuu na Mkuu wa masuala ya misaada ya Kijamii Mwamvita Makamba alikuwepo jukwaani, hawawezi kwepa lawama hizi they/you know this better...Being a main sponsor moja kwa moja unajivika FULL RESPONSIBILITY za kuwajibika na hiyo shughuli...

Rafiki wa kweli ni yule anayekujali wakati wa shida. Vodacom ndiye mwenye sauti ya mwisho kwenye haya mashindano. Wateja wake wanazama yeye anaendelea na shughuli kama kawaida. Halafu watatokeza na madawati huku wakidai wanajali watu. Vodacom hawafai kabisa.

Lakini yote tisa, kumi TBC, leo hii Taifa tukiwa kwenye maombolezo ya siku 3 bado wanandelea na programming za kawaida! Na hakika Tido Mhando angekuwepo tungeona TBC kinakuwa chombo cha kutuongoza wakati huu wa msiba.

Ni kweli mkuu tatizo limeanzia kwa serikali kushindwa kushughulika vema katika kutoa taarifa na mwongozo katika wakati muafaka. Tunaweza kuilaumu Voda (na sponsors wengine) ama waandaji wa shindano lenyewe (au hata wengine walioendelea na starehe zao kama kawaida kwa siku ya jana), kwa kutokuwa 'sensitive' lakini kuwaadhibu nadhani itakuwa ni kuwaonea. Kwa mfano ni vigumu kwa kampuni kufanya maamuzi kama ya kujitoa kudhamini fainali ya mashindano katika siku ya mwisho bila ya kuwepo kwa tamko/taarifa rasmi ya serikali.

Pamoja na hayo nafikiri waandaaji wa Miss Tanzania na masponsor wao walikamatwa pabaya. Namini katika kuandaa hiyo event hawakufikiria watafanya nini kama in the process a national disaster ikitokea. Walikuwa na plan B? In fact, the whole country was caught red handed na hili janga. Na hili lilitokea usiku wa kuamkia weekend ambapo ofisi nyingi zilikuwa zimefungwa. Kama walivyosema Aljazeera, as a nation, pamoja na majanga mengine kama haya kutokea hivi karibuni huko Zanzibar, we were not prepared to handle an event like this.

Sidhani kwa kutokuwepo kwa tamko/taarifa rasmi ya serikali kuli justify Miss Tanzania kuendelea. Wrong plus wrong does not make it right. Inawezekana kisheria ilikuwa sawa kuendelea na Miss Tanzania, but was it a right thing to do? Nafikiri argument ya watu wengi ni kuwa it was wrong kuendelea na mashindano ya Miss Tanzania wakati taifa liko kwenye msiba mkubwa. Serikali ipo responsible, local media iko responsible, na pia waandaji wa Miss Tanzania wako responsible for the aftermath. In fact the whole country is responsible. We responded very irresponsibly kwenye hili janga na inabidi tukubali.

Back
Top Bottom