Ajali ZNZ: Vodacom waanza kugomewa

Ajali ZNZ: Vodacom waanza kugomewa

Nimeandika makala hii nikiwa katika Benchi la Hospitali ya Mnazi Mmoja hapa Zanzibar. Mniwie radhi kama kuna spelling mistakes kwani nilitaka hisia zangu ziwe as raw as possible - Zitto Zitto and not Zitto a Politician).

Jana asubuhi tarehe 10 Septemba 2011 Taifa liligubikwa na habari za kushtusha za maafa. Mwanzoni taarifa zilisambaa kwamba zaidi ya watu 2000 walikuwa kwenye Boti MV Spice Islander lililopinduka na kuzama mbele kidogo ya Nungwi likielekea kisiwani Pemba. Habari hazikuwa za uhakika sana kwani vyombo vyetu vya habari na hasa Televeshini ya Taifa havikuwa vikitoa habari juu ya ajali hii.

Habari zilisambaa kupitia mitandao ya intaneti na kufuatia uchu wa habari nilianzisha #ZanzibarBoatAccident katika mtandao wa twitter ili tuweze kufuatilia kwa karibu habari zote za ajali hii.

Habari zilisambaa kuwa Televisheni ya Taifa ilikuwa inaonyesha muziki wa Taarab na Baadaye vipindi vingine vya kawaida bila kutoa habari kwa Umma kuhusu msiba huu.

Watanzania waliokoa wakiwasiliana kupitia twitter na facebook walikuwa na hasira sana na kituo cha TBC1 kutoonyesha au kupasha habari juu ya ajali hii. Mpaka saa moja jioni kituo hiki cha Televisheni ya Taifa kilikuwa kinaonyesha watu wakicheza muziki wa Kongo, wanawake wakikatika viuno na hata ngoma za asili.

'Hallo, washa TBC1 uone Televisheni yenu inachoonyesha' yalikuwa ni maneno ya Mwakilishi Ismael Jussa Ladhu aliponipigia kuonyesha kusikitishwa kwake na kituo hiki. Mpaka jioni tulikuwa tumepata taarifa kuwa Watanzania wenzetu 198 walikuwa wamepoteza maisha. 570 hivi walikuwa wameokolewa.

Binafsi nilipotembelea Hospitali ya Mnazi Mmoja niliweza kumwona Binti aliyeitwa Leyla, akisoma darasa la Nne huko kisiwani Pemba. Leyla alipona, aliokolewa. Nilimwambia leyla atapona na kurudi Shuleni. Mpaka ninapoandika tumeambiwa kuwa Watanzania 240 wamegundulika kupoteza maisha na zaidi ya 600 wameokolewa.

Napenda kuwapongeza sana waokoaji wetu, wavuvi wa kijiji cha Nungwi na vijiji jirani, wamiliki wa mahoteli waliojitolea vifaa vyao kwenda kuokoa watu na wanajeshi wetu wa majeshi ya ulinzi na usalama kwa kazi hii kubwa ya kuokoa. Kwa kweli tumeokoa watu wengi kuliko ilivyotarajiwa. Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imejitahidi sana, ilitulia na kuonyesha uongozi dhabiti katika juhudi za uokoaji.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akafuta ziara yake huko Canada, ziara iliyokuwa imeandaliwa muda mrefu na kwa gharama. Lakini Rais aliona ni vema kupata hasara kuliko kuwa nje ya Nchi kipindi hiki. Hakutaka hata kumtuma Makamu wa Rais au Waziri Mkuu. Alifuta. Akatangaza siku 3 za kuomboleza.

Hata hivyo waandaaji wa Miss Tanzania waliona hasara kubwa kuahirisha shindano la Urembo usiku huo. Wangepata hasara! Hata wafadhili wao Kampuni ya simu za mkononi ya vodacom ambao miongoni mwa waliofariki wamo wateja wa vodacom, waliendelea na shindano hili. Jumatatu, tarehe 12 Septemba 2011 ni siku ya khitma ya kuwaombea marehemu wetu.

Nimeamua kutotumia simu ya ngu ya Voda kwa siku nzima, sina njia ya kuiadhibu Kampuni hii isipokuwa kugoma kutumia simu yao japo kwa siku moja kuonyesha kutoridhishwa kwangu na uamuzi wao wa kutojali msiba huu kwa Taifa.


Misiba huweka jamii pamoja. Msiba huu uliotokea Zanzibar ni jaribio kubwa kwa Umoja wa Taifa letu. Shirika la Utangazaji la Taifa limeshindwa jaribio hili la kudhihirisha Umoja wetu katika kipindi hiki. Nataraji wakubwa wa Shirika hili linaloendeshwa kwa kodi watawajibika au kuwajibishwa!

Jumla ya Majeruhi na marehemu sasa inafikia zaidi ya Abiria 800! Asubuhi ya jana 10 Septemba 2011 tuliambiwa na Serikali kwamba uwezo wa Boti la MV Spice Islander ilikuwa ni abiria 500 na wafanyakazi 12. Pia tumejulishwa kuwa boti hili lilikuwa la Mizigo na sio la Abiria.

Natumai mara baada ya kumaliza maombolezo haya ya siku tatu Wakuu wa Mamlaka zinazohusika na usafiri wa Majini wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar watawajibika au kuwajibishwa. Mkuu wa Bandari ya Zanzibar Mustafa Aboud Jumbe na Waziri wa Miundombinu Hamad Masoud wanapaswa kufukuzwa kazi mara moja kama hawatawajibika wenyewe kwa kujiuzulu.

Kufukuzwa kwao kazi hakutarudisha ndugu zetu duniani bali itakuwa ni somo kuwa hatutarudia tena kufanya makosa yaliyoleteleza ajali kama hii.

Mwenyezimungu atupe subira wakati huu wa msiba mkubwa katika Taifa letu. Alaze roho za marehemu wetu mahala pema peponi na awape unafuu wa haraka majeruhi wetu.

Zitto Kabwe.

source: Wavuti - Habari


Huyu Zito hana lolote l alikua Znz kusighn madili na Ako yake Kina Mkono, asijifanye kuwa na uzuni,
 
Zitto Kabwe kumbe huko cynical kiasi kaka mkubwa, jaribu kufikiri kuhusu mikataba na gharama zilizotumika siku hiyo, tunataka tuone uzembe uliofanyika huko zanzibar unachukuliwa hatua, hebu kumbuka ishu ya uwanja wa taifa na meneja mpaka leo kuna nini? mikataba mibovu ya umeme, trl, hizo meremeta na nyingine zishughulikiwe kwanza kabla ya kuanza kukurupuka na kulaumu watu wengine.
 
hakuna jinis ya kukutofautisha kama zitto au zitto politician, hii inamaana ukiwa kama mwanasiasa huwakilisha hoja za uongo mahali unapokuwepo ndo maana unataka jamii ikutofautishe.
 
Hizi ni njama za usalama wa taifa kuziepusga Serikali za CCM na aibu hii, VOdacom kama mdahamini nahusika vipi? Mbona ukumbi ulijaa waliojaa humo walitoka Afrika Kusina au Tanzania? Kama kweli watanzania wangekuwa na majonzi viti vyote ukumbini vingekuwa vitupu. Tujadili chanzo cha ajali na namna uokoaji ulivyofanyika kiasi cha kupoteza uhai wa watu wengi sana. Boati zilizoenda kuokoa watu ni za watu binafsi na watalii wapi zilikuwa boti za jeshi, Polisi na Serikali za pande zote tokea saa saba usika hadi boti za watu binafsi zinze kuokota watu. Haya ndio mambo ya msingi amabyo Mhe Zitto kwa kutumiwa na uslama wa taiafa anataka tusiyajadili na kuyatafakari.
 
Zitto Kabwe kumbe huko cynical kiasi kaka mkubwa, jaribu kufikiri kuhusu mikataba na gharama zilizotumika siku hiyo, tunataka tuone uzembe uliofanyika huko zanzibar unachukuliwa hatua, hebu kumbuka ishu ya uwanja wa taifa na meneja mpaka leo kuna nini? mikataba mibovu ya umeme, trl, hizo meremeta na nyingine zishughulikiwe kwanza kabla ya kuanza kukurupuka na kulaumu watu wengine.

UZEMBE ULIANZA HAPA HAP DAR SUMATRA WASITAKE KURUKA
[h=1]Zanzibar ferry disaster: Scores die, many more rescued[/h]
_55279964_55279963.jpg
Click to play






Captain Neels van Eijk from Whirlwind Aviation flew out over the ocean to help search for survivors and describes what he saw to the BBC

Continue reading the main story[h=2]Related Stories[/h]
At least 187 people have died after an overloaded ferry sank off the Tanzanian island of Zanzibar with at least 800 people on board.
A government spokesman said 620 survivors had been rescued. Three days of mourning have been declared.
The MV Spice Islander was travelling between Zanzibar's main island, Unguja, and Pemba, the archipelago's other main island - popular tourist destinations.
It is thought to have capsized after losing engine power.
Rescue efforts were hampered by the fact that the overloaded boat had capsized at night.
The ship had been bringing people back from holiday after Ramadan, and had reportedly stopped earlier in Tanzania's commercial capital, Dar es Salaam.
The authorities are struggling to cope and have asked for foreign help.
The Zanzibar government has set up a rescue centre and called upon all reserves to join the rescue effort. It has also called for support from other countries, such as South Africa and Kenya.
Washed ashoreThe survivors were ferried by privately owned fast ferries and brought back to the main harbour in the historic Stone Town, Zanzibar police commissioner Mussar Hamis said.
"We are still receiving many bodies by truck loads," Dr Karim Zah of the Mnazi Mmoja Hospital in Zanzibar told Reuters news agency.
_55279298_erbh6z50.jpg
Those rescued were brought back to the main harbour in Stone Town

"The death toll will likely be much higher."
Dozens of soldiers carrying bodies to shore dotted the white sand beaches at the northern tip of Zanzibar island where thousands of people anxiously awaited news of survivors, the agency adds.
Catherine Purvis, a British tourist in Zanzibar who was waiting for a ferry to take her to Dar es Salaam, says she saw lots of bodies being brought out of the water.
"I'm standing at the port in Zanzibar with about 10 other British and American tourists," she said.
"Our ferry has been delayed as they're using all ferries to rescue the people from the ship.
"People are being carried across in front of us on a drip. There are lots of body bags."
Holding onLocal helicopter pilot Captain Neels van Eijk flew over the disaster area.
"We found the survivors holding on to mattresses and fridges and anything that could float," he told the BBC.
_55277002__54271182_zanzibar-1.gif

"By then, there were a few boats that had made their way out. They were looking for survivors, but although the sea wasn't so rough, the waves were high so it was difficult for them to spot them.
"We flew to the boats and guided them to the survivors so that they could pick them up. There were also quite a few bodies in the water."
The ferry left Unguja at around 21:00 (19:00 GMT) and is said to have sunk at around 01:00 (23:00 GMT).
One survivor, Abdullah Saied, said the ferry had been heavily overloaded when it left Dar es Salaam, and some passengers there had refused to board, the Associated Press news agency reports.
 
Acheni hizo.. Voda hawana kosa.. Hao wazenji wameacha kuwakamata SUMATRA wameamua kupigia promo Zantel!
 
dah! Inackitisha sana, yaani TBC walikuwa wanaonesha muziki? Habari zenyewe nlizipata Aljazeera na PressTV. Badala tv ya taifa itumie pesa za walipa kodi kuprovide habari wanafanya upuuzi tu. Yaani nlikasirika kupita kiac.
 
That was an accident, albeit manmade, but an accident all the same. It's not unique to Zanzibar and it could have happened at any place that doesn't have any regulations or that doesn't enforce its existing regulations.

As to what other folks would think about it, if they choose to believe in a 'curse' so be it, that's their prerogative. Why judge from a far and write off the entire country or region based on an accident? That to me is ignorant. I would recommend that visit and see what VTL has to offer then form an opinion about it based on facts. Or better yet, why don't you school them on the great things VTL have already financed and sponsored. Be an ambassador for your country!!!!
 
Back
Top Bottom