Ajibu: Bado kidogo tu walionibeza watanishangilia

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
1644313528946.png

NYOTA wa zamani wa Simba na Yanga anayekipiga Azam FC, Ibrahim Ajibu amesema bado kidogo tu wale waliokuwa wakimbeza wataanza kumpigia makofi. Fundi huyo wa mpira alisema anaamini kupewa nafasi ya kucheza kila mara ndani ya timu hiyo mpya kwake, atafanya vizuri zaidi na kumsaidia kufikia malengo yake.

Akizungumza na Mwanaspoti, Ajibu alisema anaamini katika kila jambo Mungu yupo nyuma yake, hivyo atafanya makubwa akiwa na timu yake mpya kwa kushirikiana na wenzake.

“Namshukuru sana Mungu napata nafasi katika maisha yangu mapya, mimi kama mchezaji nafurahi na nafarijika kwa kuwa naonesha kitu kupitia wao walivyoniamini na kuniona nafaa kuwa katika timu yao,” alisema staa huyo aliyewahi kuwa nahodha wa Yanga.
 
Ajib, wapenzi wa soka la bongo ndio wanachokitaka na wanachokisubiria. Watu hawakubezi bure. Wangekua wanajua wewe ni mchezaji average wasingekua na habari na wewe, sio kwa kukusifia wala kukubeza. Wangekuacha tu kama wanavyowaacha wachezaji wengi tu wa kawaida

Lakini watu wanajua wewe ni tofauti. Una kitu cha ziada katika miguu yako. Unakipaji cha hali ya juu cha kucheza soka. Bahati mbaya kwa muda mrefu hasa ukiwa Simba umeshindwa kuonyesha thamani yako kwa sababu ambazo zipo ndani ya uwezo wako

Fanya jambo hapo Azam na watu watakushangilia na kukukaribisha tena katika nyoyo za wapenda soka na makocha watakuita timu ya Taifa. Ongea kwa vitendo Ibrahim Ajib Migomba
 
NYOTA wa zamani wa Simba na Yanga anayekipiga Azam FC, Ibrahim Ajibu amesema bado kidogo tu wale waliokuwa wakimbeza wataanza kumpigia makofi. Fundi huyo wa mpira alisema anaamini kupewa nafasi ya kucheza kila mara ndani ya timu hiyo mpya kwake, atafanya vizuri zaidi na kumsaidia kufikia malengo yake.

Akizungumza na Mwanaspoti, Ajibu alisema anaamini katika kila jambo Mungu yupo nyuma yake, hivyo atafanya makubwa akiwa na timu yake mpya kwa kushirikiana na wenzake.

“Namshukuru sana Mungu napata nafasi katika maisha yangu mapya, mimi kama mchezaji nafurahi na nafarijika kwa kuwa naonesha kitu kupitia wao walivyoniamini na kuniona nafaa kuwa katika timu yao,” alisema staa huyo aliyewahi kuwa nahodha wa Yanga.
Shida yake ni kufanta mazoezi

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
Apambane asongembele kama umri bado atakua nao.aachane na wanaomcheka na kumbeza kama kipaji anacho tena kikubwa.
 
Back
Top Bottom