Ajificha kwenye tairi la ndege kutoka Afrika Kusini mpaka Uholanzi

Ajificha kwenye tairi la ndege kutoka Afrika Kusini mpaka Uholanzi

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
Polisi wa kijeshi nchini Uholanzi leo wameshangazwa kumkuta mtu aliyekuwa amejificha chini ya ndege kwenye eneo la tairi la mbele kuwa yuko salama.

Ndege hiyo ilisafiri kwa saa 11 kutokea Afrika mpaka Ulaya.

Ndege hiyo ya mizigo ilitokea Afrika Kusini na kutua Kenya kwa muda mfupi kabla ya kuelekea Amsterdam, Uholanzi.

Mtu huyo ambaye uraia wake, jinsia na umri bado havijatajwa sasa yuko hospitali na hali yake inaendelea vizuri.

Uchunguzi kuhusu tukio hilo bado unaendelea lakini Polisi hao wamesisitiza kuwa "hii ni ngumu kuielewa, ukizingatia baridi ya sehemu alipokuwa amejificha na urefu kutoka usawa wa bahari ndege hiyo aina ya Boeing 747 ilipokuwa".

===
Polisi wa Uholanzi wanasema wamempata mtu akiwa hai katika sehemu ya gurudumu la ndege iliyotua katika uwanja wa ndege wa Amsterdam wa Schiphol kutoka Afrika Kusini.

Safari za ndege kutoka Johannesburg hadi Amsterdam huchukua takriban saa 11, huku ndege ya mizigo ikiaminika kusimama mara moja, jijini Nairobi, Kenya.

Si jambo la kawaida sana kwa wanaopanda ndege kimagendo kuishi, kutokana na baridi na oksijeni kidogo kwenye miinuko ya juu.
Umri na utaifa wa mwanaume huyo bado haujabainishwa, polisi wanasema.

"Mwanaume huyo alipatikana akiwa hai katika sehemu ya gurudumu upande wa pua ya ndege na alipelekwa hospitalini akiwa katika hali nzuri," msemaji wa Polisi wa Kijeshi wa Uholanzi Joanna Helmonds aliambia shirika la habari la AFP.

"Inashangaza kwamba mtu huyo bado yuko hai," alisema. Kwa mujibu wa mtangazaji wa Uholanzi NOS, joto la mwili wa mtu huyo liliongezeka katika eneo la tukio na wakati gari la wagonjwa lilifika, aliweza kujibu maswali ya msingi.

Msemaji wa idara ya shehena ya mizigo Cargolux alithibitisha katika barua pepe kwa Reuters kwamba mtu huyo alikuwa kwenye ndege inayoendeshwa na Cargolux Italia.

Kulingana na data ya ndege, ndege pekee ya Cargolux ya mizigo kutoka Johannesburg hadi Schiphol Jumapili pia ilisimama Nairobi.
Haijulikani iwapo mwanaume huyo alipanda ndege hiyo nchini Afrika Kusini au Kenya.
 
Hii inawezekana vp
Mtu mpaka anaingia kwenye tair ya ndege watu wa ulinzi wanakuwa wapi
 
Hii inawezekana vp
Mtu mpaka anaingia kwenye tair ya ndege watu wa ulinzi wanakuwa wapi
Hilo cha mtoto
Sehemu alipojificha kuna hydraulics piping za kutosha na lile tairi linapozama linaacha gap ndogo sana kwa binadamu kuishi, wengi huwa wakifanya hivyo wanabanwa na landing gears.

Kingine ni feeezing point temperatures kwenye altitude ndege hizo inazosafiria, 40000 feets hakunaga oxygen

Kuna mengi sana yanashangaza kwenye tukio hilo , ila, all in all he is a very lucky man.
 
Polisi wa kijeshi nchini Uholanzi leo wameshangazwa kumkuta mtu aliyekuwa amejificha chini ya ndege kwenye eneo la tairi la mbele kuwa yuko salama.

Ndege hiyo ilisafiri kwa saa 11 kutokea Afrika mpaka Ulaya...

Cha maana wasimrudishe Africa; Kwa kweli siasa mfano Za Tanzania Na Masimango yake unaweza Zamia tu Kwenye ndege!
 
Polisi wa Uholanzi wanasema wamempata mtu akiwa hai katika sehemu ya gurudumu la ndege iliyotua katika uwanja wa ndege wa Amsterdam wa Schiphol kutoka Afrika Kusini.

Safari za ndege kutoka Johannesburg hadi Amsterdam huchukua takriban saa 11, huku ndege ya mizigo ikiaminika kusimama mara moja, jijini Nairobi, Kenya.

Si jambo la kawaida sana kwa wanaopanda ndege kimagendo kuishi, kutokana na baridi na oksijeni kidogo kwenye miinuko ya juu.

Umri na utaifa wa mwanaume huyo bado haujabainishwa, polisi wanasema.

"Mwanaume huyo alipatikana akiwa hai katika sehemu ya gurudumu upande wa pua ya ndege na alipelekwa hospitalini akiwa katika hali nzuri," msemaji wa Polisi wa Kijeshi wa Uholanzi Joanna Helmonds aliambia shirika la habari la AFP.

"Inashangaza kwamba mtu huyo bado yuko hai," alisema.

Kwa mujibu wa mtangazaji wa Uholanzi NOS, joto la mwili wa mtu huyo liliongezeka katika eneo la tukio na wakati gari la wagonjwa lilifika, aliweza kujibu maswali ya msingi.

Msemaji wa idara ya shehena ya mizigo Cargolux alithibitisha katika barua pepe kwa Reuters kwamba mtu huyo alikuwa kwenye ndege inayoendeshwa na Cargolux Italia.

Kulingana na data ya ndege, ndege pekee ya Cargolux ya mizigo kutoka Johannesburg hadi Schiphol Jumapili pia ilisimama Nairobi.

Haijulikani iwapo mwanaume huyo alipanda ndege hiyo nchini Afrika Kusini au Kenya.

BBC Swahili
 
Sasa watu wanashangaa nini wakati hii siyo mara ya kwanza! Mbona kuna Waafrika Kusini wawili walishawahi kudandia ndege kutoka Afrika Kusini hadi Uingereza na walikaa kwenye magurudumu safari nzima!

Sema kwa bahati mbaya mmoja alifariki yaani wakati ndege inakaribia kutua akaangukia juu ya paa la jengo moja karibu kabisa na Heathrow Airport London na kufariki hapo hapo! Yule mwingine ndiyo alipona!

Ila wakati ndege inataka kuland kwenye runway ilipokunjua tu magurudumu akaanguka akiwa hoi! Wakamchukua wakampeleka hospitali alipopona wakamuachilia mitaani akapata msamaria mwema akamsaidia!
 
Back
Top Bottom