wa kupuliza
JF-Expert Member
- Jun 15, 2012
- 15,216
- 37,757
Ni meya wa mkoa wa ZanzibarHuyu Assimi Goita ni nani mkuu na amefanya nini??
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ni meya wa mkoa wa ZanzibarHuyu Assimi Goita ni nani mkuu na amefanya nini??
Yeah ni kweli kwa muktadha wa kuto entertain kitu kama hicho. Ila huyu duh inatakiwa ahojiwe atoe mbinu na ikiwezekana itengenezewe documentary walau apige pesa katika hilo.Watakwambia, ^He's setting a very bad precedence for others to follow! So, he should receive the severest punishment to warn those who may be of likeminded.^
Ndivyo ECOWAS wanavyomfanya Assimi Goïta wa Mali.
shujaa wa january 2022Polisi wa Uholanzi wanasema wamempata mtu akiwa hai katika sehemu ya gurudumu la ndege iliyotua katika uwanja wa ndege wa Amsterdam wa Schiphol kutoka Afrika Kusini.
Safari za ndege kutoka Johannesburg hadi Amsterdam huchukua takriban saa 11, huku ndege ya mizigo ikiaminika kusimama mara moja, jijini Nairobi, Kenya.
Si jambo la kawaida sana kwa wanaopanda ndege kimagendo kuishi, kutokana na baridi na oksijeni kidogo kwenye miinuko ya juu.
Umri na utaifa wa mwanaume huyo bado haujabainishwa, polisi wanasema.
"Mwanaume huyo alipatikana akiwa hai katika sehemu ya gurudumu upande wa pua ya ndege na alipelekwa hospitalini akiwa katika hali nzuri," msemaji wa Polisi wa Kijeshi wa Uholanzi Joanna Helmonds aliambia shirika la habari la AFP.
"Inashangaza kwamba mtu huyo bado yuko hai," alisema.
Kwa mujibu wa mtangazaji wa Uholanzi NOS, joto la mwili wa mtu huyo liliongezeka katika eneo la tukio na wakati gari la wagonjwa lilifika, aliweza kujibu maswali ya msingi.
Msemaji wa idara ya shehena ya mizigo Cargolux alithibitisha katika barua pepe kwa Reuters kwamba mtu huyo alikuwa kwenye ndege inayoendeshwa na Cargolux Italia.
Kulingana na data ya ndege, ndege pekee ya Cargolux ya mizigo kutoka Johannesburg hadi Schiphol Jumapili pia ilisimama Nairobi.
Haijulikani iwapo mwanaume huyo alipanda ndege hiyo nchini Afrika Kusini au Kenya.
BBC Swahili
Polisi wa kijeshi nchini Uholanzi leo wameshangazwa kumkuta mtu aliyekuwa amejificha chini ya ndege kwenye eneo la tairi la mbele kuwa yuko salama.
Ndege hiyo ilisafiri kwa saa 11 kutokea Afrika mpaka Ulaya.
Ndege hiyo ya mizigo ilitokea Afrika Kusini na kutua Kenya kwa muda mfupi kabla ya kuelekea Amsterdam, Uholanzi.
Mtu huyo ambaye uraia wake, jinsia na umri bado havijatajwa sasa yuko hospitali na hali yake inaendelea vizuri.
Uchunguzi kuhusu tukio hilo bado unaendelea lakini Polisi hao wamesisitiza kuwa "hii ni ngumu kuielewa, ukizingatia baridi ya sehemu alipokuwa amejificha na urefu kutoka usawa wa bahari ndege hiyo aina ya Boeing 747 ilipokuwa".
Inaonenakana wasauzi magwiji kwenye hii fani..inabidi "mastolowei"new generation wakajifunze ma mbinu huko si mchezo!Sasa watu wanashangaa nini wakati hii siyo mara ya kwanza! Mbona kuna Waafrika Kusini wawili walishawahi kudandia ndege kutoka Afrika Kusini hadi Uingereza na walikaa kwenye magurudumu safari nzima!
Sema kwa bahati mbaya mmoja alifariki yaani wakati ndege inakaribia kutua akaangukia juu ya paa la jengo moja karibu kabisa na Heathrow Airport London na kufariki hapo hapo! Yule mwingine ndiyo alipona!
Ila wakati ndege inataka kuland kwenye runway ilipokunjua tu magurudumu akaanguka akiwa hoi! Wakamchukua wakampeleka hospitali alipopona wakamuachilia mitaani akapata msamaria mwema akamsaidia!
Huyu Assimi Goita ni nani mkuu na amefanya nini??
^War-who-knee^ watakwambia eti huko ni kuwa-entertain mabaradhuli na kushabikia villains badala ya heros.Yeah ni kweli kwa muktadha wa kuto entertain kitu kama hicho. Ila huyu duh inatakiwa ahojiwe atoe mbinu na ikiwezekana itengenezewe documentary walau apige pesa katika hilo.
Uholanzi wanaweza kuwa na huruma lakini atume pesa nyumbani wafanye tambiko la shukranYeah ni kweli kwa muktadha wa kuto entertain kitu kama hicho. Ila huyu duh inatakiwa ahojiwe atoe mbinu na ikiwezekana itengenezewe documentary walau apige pesa katika hilo.
Tena wa gharisaHuyu atakuwa Mkenya[emoji1787][emoji1787][emoji91]
Sure mkuu na huyo pamoja na kwamba alipona ila pia wakati anaanguka alivunjika mguu. Akakaa hospitali zaidi ya miezi sita na nahisi hiyo pia ni sababu mojawapo kwanini mapolisi waliamua kumuachilia tu mitaani hawakumfunga wala hawakumrudisha kwao.uwezi fika kanan hivi hivi bila kuwa lesso ya kufuata machozi na jasho.
Sure kabisa huyu mi nilijisemea tu ilikuwa bahati yake. Lakini pia sababu mojawapo iliyofanya wamuonee huruma na kumuachilia mitaani ni kwa vile alipoanguka alivunjika mguu akakaa hospitali zaidi ya miezi sita alipopona na kuwaelezea historia ya maisha yake ndiyo wakamuonea huruma wakamuacha.Ni kwere joh. Huyo anatakiwa atunukiwe na cheti cha heshima kabisa.
Simple,WALIPEWA RUSHWAHii inawezekana vp
Mtu mpaka anaingia kwenye tair ya ndege watu wa ulinzi wanakuwa wapi
Hahaaa maisha ya afrika siyo kabisa. Hao majamaa unaambiwa kabla ya kudandia lile dege la British Airways ilibidi watafute material za kutosha kuhusu structure ya ndege na namna ya kujibanza vizuri kwenye magurudumu.Inaonenakana wasauzi magwiji kwenye hii fani..inabidi "mastolowei"new generation wakajifunze ma mbinu huko si mchezo!
Ila, huyo mtasha aliyemsaidia mwamba plus na mamlaka Mungu awape pepo wallahi safi sana. Afrika jamani maisha magumu ooh
Mie kuna anko namkumbuka mpumbavu sana ati alishangaa kwanini sikupata kazi enzi hizo kana kwamba ajira ni rahisi sana bongo. Nikimkumbuka huwa namtukana kimyakimya.
Hatari ilibidi nikatafute hiyo habari nimepatana na article moja the guardian jamaa anaishi Liverpool siku hizi ana hustle kwenye mambo ya hip-hop.Sure kabisa huyu mi nilijisemea tu ilikuwa bahati yake. Lakini pia sababu mojawapo iliyofanya wamuonee huruma na kumuachilia mitaani ni kwa vile alipoanguka alivunjika mguu akakaa hospitali zaidi ya miezi sita alipopona na kuwaelezea historia ya maisha yake ndiyo wakamuonea huruma wakamuacha.
Ni kamandooo huyoHilo cha mtoto
Sehemu alipojificha kuna hydraulics piping za kutosha na lile tairi linapozama linaacha gap ndogo sana kwa binadamu kuishi, wengi huwa wakifanya hivyo wanabanwa na landing gears.
Kingine ni feeezing point temperatures kwenye altitude ndege hizo inazosafiria, 40000 feets hakunaga oxygen
Kuna mengi sana yanashangaza kwenye tukio hilo , ila, all in all he is a very lucky man.
Sijanywa cha mtuliwalo na liwe
Maisha ya Afrika ni nusu jehanamu.Sure kabisa huyu mi nilijisemea tu ilikuwa bahati yake. Lakini pia sababu mojawapo iliyofanya wamuonee huruma na kumuachilia mitaani ni kwa vile alipoanguka alivunjika mguu akakaa hospitali zaidi ya miezi sita alipopona na kuwaelezea historia ya maisha yake ndiyo wakamuonea huruma wakamuacha.
Huyo tayari ni kivutio Cha utarii watamlinda Sana maana kumuona tu lazima utoe kwanza kutokana na uajabu aliouonyesha usifikili wao hawaoni fulsa tayar wamemuandalia makaziPolisi wa kijeshi nchini Uholanzi leo wameshangazwa kumkuta mtu aliyekuwa amejificha chini ya ndege kwenye eneo la tairi la mbele kuwa yuko salama.
Ndege hiyo ilisafiri kwa saa 11 kutokea Afrika mpaka Ulaya...