Ajinyonga baada ya kujifungua mtoto mlemavu

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,336
Reaction score
4,731
Mwanamke mmoja mkazi wa Njombe, amejinyonga baada ya kujifungua mtoto mwenye ulemavu, ambapo Kamanda wa Polisi mkoani humo Khamis Issah, akawasihi wanawake kuwa na huruma na watoto na kuhoji kama mzazi amejinyonga mtoto aliyemuacha atalelewa na nani.

Kamanda Issah ameongeza kuwa kama kuna mtu ana mpango wa kujinyonga basi haina haja ya yeye kushika ujauzito na kisha kujinyonga na kuacha mtoto, na kuwasihi wazazi kujilinda kwa ajili ya watoto wao.

“Wewe unayejinyonga na una watoto, unajinyonga kwa sababu gani, watoto bado wadogo watamtegemea nani, kama wewe una mawazo ya kujinyonga basi usiwatafute hao watoto wewe ujinyonge peke yako, kama wewe usingewatafuta wasingekuwa na wazazi,” amesema ACP Issah
 
🤣🤣🤣
Dah, asante kwa kitia moyo ACP, lakini wakati tunatafuta hao watoto huwa hatuwazi kujinyonga, mawazo yanakuja na stress za maisha, tusaidiane tu mkuu ACP
 
Kujiua ni mwanzo wa matatizo mengine mengi
 
Ni kweli mkuu, lkn watu wana mizigo mingi akili na mioyoni mwao, maisha nayo yanachapa, saa nyingine mtu hana wa kuongea naye, wamevurugwa hawako sawa, bora ACP angeshauri kuhusu tiba za kisaikolojia kwa watu walioelemewa na maisha/mawazo na sio hiyo mipasho aliyotoa kwa marehemu
 
Ni kweli mkuu, lkn watu wana mizigo mingi akili na mioyoni mwao, maisha nayo yanachapa, saa nyingine mtu hana wa kuongea naye, wamevurugwa hawako sawa, bora ACP angeshauri kuhusu tiba za kisaikolojia wa watu walioelemewa na maisha/mawazo na sio hiyo mipasho aliyotoa kwa marehemu
Kuna siri nzito, ila usiwe miongoni mwao waliokata tamaa
 
Aisee! Utakuta huyo Mama aliwaza kila kibaya juu ya huyo mwanae akasahau kwamba mbali na yote mtoto mlemavu naye ni binadamu kama binadamu wengine.

Pole kwa ndugu jamaa na marafiki, japo amemuachia mwanae wakati mgumu sana, sababu siku zote ambaye anaweza kuzipokea na kuzivumilia changamoto za huyo mwanae kwa 100% alikuwa ni yeye mzazi.
 
Ni kweli mkuu, lkn watu wana mizigo mingi akili na mioyoni mwao, maisha nayo yanachapa, saa nyingine mtu hana wa kuongea naye, wamevurugwa hawako sawa, bora ACP angeshauri kuhusu tiba za kisaikolojia kwa watu walioelemewa na maisha/mawazo na sio hiyo mipasho aliyotoa kwa marehemu
Ukikosa wa kuongea nao in real life kuna watu online kama hivi, ongea utoe ya moyoni.

Kufika stage ya kujinyonga ni mbaya sana.
 
kusema ukweli me huwa nashangaa watu wanaoandika online, siwezi kubandika shida zangu online hata kama sionani na mtu, huku watu napo wamevurugwa tu,
 
Online kumesaidia sana watu kupunguza mizigo yao, siku hizi watu wanaona bora kuwa na vijiwe jf,twitter, fb kuliko mitaani.

Sasa wewe ukiniambia shida yako tukazungumza hadi ukapata ahueni wakati hata hatujuani unapata hasara gani.
 
najua aina hiyo ya watu, ni kama wale watu huku uraiani hawawezi kukaa na shida lazima akamsimulie mtu. Binafsi siko kundi hilo, mi ni wale nikiwa na shida nakaa kimya na halmashauri ya kichwa changu, nafikiri ni jambo la kiroho zaidi, mambo mengi yanauoumiza watu ni mambo "madogo" lakini hawajui hilo na huwezi kumuambia mtu hivyo kama hajafikia hiyo level ya utambuzi, na wengi kiukweli hawajafika, so tunasaidiana hivyo hivyo
 
Nakuelewa sana mkuu!
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Dah, asante kwa kitia moyo ACP, lakini wakati tunatafuta hao watoto huwa hatuwazi kujinyonga, mawazo yanakuja na stress za maisha, tusaidiane tu mkuu ACP
Hahah
 
Back
Top Bottom