Ajinyonga baada ya mzozo wa chapati na shangazi yake

Ajinyonga baada ya mzozo wa chapati na shangazi yake

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Binti wa miaka 20, ajulikanaye kama Sharon, mkazi wa Kisumu, Kenya, amejinyonga hadi kufa baada ya majibizano baina yake na shangazi yake kuhusu chapati.

Inaelezwa kuwa Sharon aliachiwa fedha kwa ajili ya kununua chakula na kupika kwa ajili ya familia na badala yake alinunua chapati cha maharage na kula mwenyewe.

Kwa mujibu wa jirani wa familia hiyo, Jane Auma, shangazi yake aliporudi nyumbani na kuuliza kwanini binti huyo hakupika chakula cha familia nzima na badalayake akajinunulia chapati, wawili hao walianza kujibiza na baadaye, msichana huyo aliamua kujiua kwa kujinyonga.

Auma anasema ni ngumu kuamini kuwa msichana huyo angeweza kujinyonga kwa mzozo wa chapati, lakini hatahivyo ujumbe wa alioacha ameuandika tayari umefikishwa polisi.

Mwili wa marehemu umeshapelekwa kuhifadhiwa kwenye hospitali ya Jaramogi Oginga na upelelezi unaendelea.

Malunde1 blog
 
Kuna watu wenye hulka ya kujinyonga hata kwa vitu vidogo vidogo, huko Tanzania kuna makabila yanafahamika kwa watu wake kujinyonga.
Huko tanzania nani kakwambia mimi nipo tz? Sipo tz na wala sio mtz
 
Kuna watu wenye hulka ya kujinyonga hata kwa vitu vidogo vidogo, huko Tanzania kuna makabila yanafahamika kwa watu wake kujinyonga.
Point hapo ni kwamba pesa inayotosha kununua chakula cha familia nzima watu wote wale washibe kumbe ni pesa ya kununua chapati ya mtu mmoja tu

Therefore huu ni udhibitisho wa wazi wazi kwamba chapati Kenya ni expensive and luxury wala hauhitajiki kutumia nguvu kulijua hili.
 
Simply wengi hawajui kupika.
 
Kuna watu wenye hulka ya kujinyonga hata kwa vitu vidogo vidogo, huko Tanzania kuna makabila yanafahamika kwa watu wake kujinyonga.
Ulisikia wapi watu au mtu kajinyonga Tz ? Nina muongo mmoja sijasikia mtu kujinyonga
 
Ss hapo umesikia kuna mtu kajiua kisa msosi ? MK254 Hahahaha iv una dada yako unipe jaman nimchumbie nimuwowe

Watu wa kujinyonga hujitoa uhai kwa sababu zozote, yaani kumgombeza kidogo tu basi kitanzi.
Kwa matukio ya kujinyonga Tanzania, ni vigumu kwa mimi kufuatilia kisa cha kila mmoja, ukizingatia media zenu huwa ovyoo sana likija suala la kutoa habari, wao wapo wapo tu kazi kusifia wakuu serikalini.
 
Back
Top Bottom